Wagombea wawili wa urais nchini
Venezuela wamehutubia umati mkubwa wa wafuasi wao katika siku ya mwisho
ya kampeni kabla ya uchaguzi utakaofanyika Jumapili.
Rais Hugo Chavez ambaye amekuwa madarakani kwa
takriban miaka kumi na minne amewaambia maelfu ya wafuasi wake huko ,
Caracas kuwa anahitaji muhula wa tatu kuimarisha marekebisho ya kijamii
na kutokomeza umaskini.Aliahidi kuimarisha uchumi na uongozi bora na kisha aliwahimiza wapiga kura kujitokeza kwa wingi Jumapili.
Aliwataka wapiga kura kumuunga mkono ili waweze kumshinda bwana Chavez kwenye uchaguzi huo siku ya Jumapili.
Wadadisi wanatabiri ushindani mkubwa kwenye uchaguzi huo dhidi ya Rais Chavez ukiwa ndio wa kwanza tangu aingine mamlakani mwaka wa 1999
No comments:
Post a Comment