NJOMBE

NJOMBE

Friday, May 11, 2012

Kukosa mwangaza wa jua hatari

Utafiti uliofanywa hivi karibuni juu ya kupungua kwa nuru ya macho kumeonyesha kua hadi asili mia 90 ya wanafunzi wanaohitimu masomo huathiriwa na tatizo la kuona

Jua muhimu kwa macho Macho yahitaji kutunzwa vizuri.

Wataalamu wanasema kua ongezeko hili la kutisha juu ya tatizo la macho limesababishwa na wanafunzi kusoma sana na kukosa mwangaza wa jua.
Wataalamu wameliambia jarida la kiafya la Lancet kua mmoja kati ya wanafunzi watano anaweza kukabiliwa na mapungufu ya macho na hata kupofuka macho.
Kulingana na Professor Ian Morgan wa Chuo Kikuu cha Australian National University, aliyeongoza utafiti huu,asili miaka 20-30% waliwahi kua watu wa kawaida wasiokua na matatizo huko Bara Asia kusini mashariki.
Idadi ya wagonjwa wa maradhi haya ya macho imepanda kutoka asili mia 20 waliopungukiwa na nuru ya kuona na kuzidi asili mia 80 na kuelekea asili mia 90 miongoni mwa vijana na watakapoingia umri wa watu wazima maradhi hayo yataenea zaidi miongoni mwa jamii nzima.Bila shaka hili ni tatizo kubwa la kiafya.
Wataalamu wa masuala ya macho wanasema kua una mapungufu ya macho ikiwa unachotazama hukiona vizuri kutoka umbali wa mita 2 yaani futi sita.
Tatizo hili husababishwa na kurefuka kwa mboni ambako hutokea mtu akiwa na umri mdogo.
Kwa mujibu wa utafiti, tatizo hili husababishwa na masuala kadhaa- kusoma kwa kupindukia na kukosa mwangaza wa jua.
Professor Morgan anasema kua watoto wengi huko Asia ya kusini mashariki hutumia mda mrefu wakisoma shuleni na baadaye kudurusu nyumbani. Hili huwazidishia shinikizo kwenye macho yao, lakini wangeweza kutoka nje kwa mda wa saa mbili hadi tatu ili kurekebisha mapungufu na umuhimu wa mwqangaza inawezekana kulinda afya ya macho yao.
Jicho
Jicho bandia

Wataalamu wana imani kua aina ya kemikali ijulikanayo kama dopamine ambayo huenda ina mchango katika hili. Kukaaa katika mwangaza wa nje huongeza viwango vya kemikali hii ya dopamine ndani ya jicho na hilo huzuia kurefuka kwa mboni.
Nyenzo za kitamaduni nazo zinachangia. Watoto wengi wa Bara Asia kusini mashariki, hupenda sana kupumzika nyakati za adhuhuri. Kulingana na Professor Morgan tabia hii huwakosesha mwangaza wa jua la mchana ambao ni muhimu katika kuzuia maradhi haya ya kupungua kwa nuru ya macho, myopia.
Pamoja na shinikizo za kutaka kufanikiwa katika elimu na kupangiwa siku kwa watoto, mda ambao mtoto hukaa nje kunufaika kwa mwangaza wa jua unapunguwa. Wasiwasi mkubwa ni idadi ya wanafunzi ambao wanazidi kupatwa na maradhi ya myopia.
Kwa miongo kadhaa wataalamu wameamini kua kuna uhusiano mkubwa wa jeni au urithi kutoka kwa wazazi kuhusiana na hali hii ya ugonjwa wa macho.Ikiaminika kua watu kutoka Uchina,Japan,Korea na nchi nyingine wanaweza kukumbwa na myopia.Lakini utafiti huu unaonyesha mtazamo tofauti.
Hili litahitaji utafiti zaidi lakini la muhimu ni kuwatia moyo watoto watumie mda mwingi nje ya nyumba jua linapochomoza. Huenda likapunguza madhara ya macho.

No comments:

Post a Comment