NJOMBE

NJOMBE

Wednesday, May 9, 2012

JAMANI HIVI HATUJUI MAZINGIRA YETU : Ubaya na Uzuri wake…

Jamii zetu zinazoendelea zinahitaji sana Elimu.  Elimu itakayotusaidia kupambana na maadui kama : kutojua kupanga muda (Time Management) tatizo linalotufanya tuchelewe, tusiwe na mpangilio wa maisha ; halafu, kutoyajali mazingira yetu (vyoo vichafu na kutupa taka ovyo).Uchafu wa mazingira DarWataalamu wameshatuonya kuwa makaratasi ya plastiki tunayoyaacha kiholela kila mahali (yenye madawa hatari) yanaharibu rutuba na uhai ; yatakaa ardhini miaka 500 !!!
Bougainvillea -Silversands
Si mbali  na palipotupwa plastiki hizi pana hoteli hii marufu na nzuri ya Silversands ambapo watalii na wenye uwezo wanakaribishwa kwa maua  mazuri yenye asili ya Kimarekani yaitwayo Bougainvillea.  Ikiwa tunaweza kuyapamba mazingira ki-azizi,  hatushindwi kuyaacha safi…
Madafu
Nilishangazwa nilipoelezwa na muuza madafu mmoja Dar kuwa kinywaji (chakula) hicho muhimu siku hizi hakipatikani kirahisi. “Minazi inakatwa ovyo…” akalalama.
Minazi ya Dole
Nilipokuwa kitongoji hiki cha Dole, Unguja, nikawa nawaza lile balaa la minazi kukatwa bandari  ya Dari Salama. Minazi imesimama dede mithili ya twiga au mbuni malishoni.  Je, itadumu?
Matunda ya Afrika  Sehemu nyingi Zanzibar bado vyakula asilia vinathaminiwa. Cheki  matunda, mboga na makulaji : mjini na vijijini. Ama kweli inatia moyo…maana chakula ni utamaduni wa nchi; kama huna au unaiga (huthamini chako) huna jicho…
Chakula cha Zanzibar
Huku unakula huku unafikiria namna ambavyo bado wananchi wengi tunatupa chupa za maji ovyo nje; tunavyofungia bado vyakula vyetu kwa magazeti badala ya mifuko isiyokuwa na sumu na madawa…
Chupa ya maji- uchafu
Kinamasi hiki kimejaza si tu plastiki  na dawa zenye sumu bali pia wadudu kama mbu. Kila anayeweza (kutumia mtandao na kompyuta ni uwezo na nafasi) kuelemisha watu wetu ajitahidi na kujaribu…maana hizi blogu hazisomwi na wengi.
Silversands-2
Hapa natia tizi katika moja ya bichi za Dar…ukweli si rahisi siku hizi kupata ufukwe msafi mjini hapa. Na hata zile safi baada ya kuogelea unahisi macho yakikuwasha washa. Watalaam wameonya kuhusu kutupa taka ovyo baharini, kunya (na kukojoa) ovyo ufukweni, kuchafua michanga kwa vyupa vya vinywaji tunapostarehe kando ya bahari mama ya Hindi.
Jani la Mnazi
Pwani ya Dar

No comments:

Post a Comment