NJOMBE

NJOMBE

Thursday, May 31, 2012

Kuvuja kwa nyaraka za siri za papa

Papa Benedict
Papa Benedict
Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican, amesema kuvuja kwa nyaraka za siri za kiongozi wa kanisa hilo duniani ni kitendo cha kikatili dhidi ya Papa Benedict.
Afisa huyo ambaye ni naibu waziri wa mambo ya nje wa Vatican Angelo Becciu, amesema nyaraka hizo ni pamoja na fikra binafsi, na pia shutuma kali kutoka kwa watu waliomwandikia Papa barua za siri kutokana na nafasi yake ya kipekee.
Nyaraka hizo zinashutumu vitendo vya rushwa na kushindania madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki.
Mwandishi wa BBC mjini Vatican amesema hii ni kashfa kubwa kuliko zote dhidi ya Papa Benedict tangu apate wadhifa wake huo miaka saba iliyopita, na ni tukio lililochafua Kanisa Katoliki nyakati hizi.
Mhudumu mkuu wa Papa, Paolo Gabriele, amekamatwa na tume ya Vatican inachunguza watu wengine ambao wamehusika katika kashfa hiyo.

No comments:

Post a Comment