Rais Jakaya Kikwete akiongea na Fili Karashani Mwandishi mkongwe
naambaye ameshinda tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari
mwaka 2011, katika tuzo za (EJAT) zilizoandaliwa na Baraza la Habari
Nchini Tanzania (MCT) na washirika wake, hafla hiyo inafanyika kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu, katika picha kushoto ni Mwandishi
wa siku nyingi Khamis Ben Kiko.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Nevil Meena cheti cha ushindi wa jumla kwa katika tuzo hizo mara baada ya kutangazwa rasmi.
Kikundi cha Ngoma za asili cha Simba Thietre kikitumbuiza katika tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy
Mapunda akikabidhi tuzo kwa mwandhishi wa habari wa Mlimani Radio Tuma
Dandi mshindi wa habari za watu wenye ulemavu- Redio
Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda akikabidhi tuzo kwa
Abdallah Majura Mkurugenzi wa Radio Sports FM ya Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya bia ya
Serengeti Graham Anderws akimkabidhi cheti na zawadi yake Nevil Meena
kutoka gazeti la Mwananchi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Executive Solution Agrey Maleale akimkabidhi
zawadi yake Khamis Hamad kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo.
Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga akizungumza katika hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi walipkutana katika hafla hiyo.
NATHAN MPANGALA MCHORAJI BORA WA KATUNI, ASHINDA TUZO YA (EJAT)
.Nathan Mpangala Kwa wiki kadhaa sasa yuko mafunzoni nchini Mexico, akihudhuria kozi fupi
ya waandishi wa habari, inayohusu Civil Resistance and Non violence
Conflict. Hapa akiwa na baadhi ya washiriki wenzake toka sehemu
mbalimbali duniani, wakiandaa michoro kwa ajili ya video itakayotumika
kwenye kampeni ya familia zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana
na mauaji ya kila siku yanayohusishwa na biashara ya dawa za kulevya.
Nathan Mpangala
pia usiku huu ameshinda tuzo ya wachoraji bora wa katuni katika tuzo za
(AJET) zilizoandaliwa na Baraza la Habari (MCT) zinazofanyika usiku huu
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Hapa wakiendelea na kazi yao ya kuandaa katuzi hizo zinazohusu mauaji yanayotokana na madawa ya kulevya nchini Mexico.
No comments:
Post a Comment