kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo kunafanyika hafla
kubwa ya utoaji wa tuzo ya Umahili wa uandishi wa habari kwa mwaka wa
2012 zinazoandaliwa na Baraza la Habari MCT na washirika wake ambapo
mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya
Kikwete.
Wamejitokeza wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wasomi na waandishi wa
habari wakongwe kama picha ya kwanza inavyoonekana kutoka kulia ni
Profesa Aisha Yahya Othman mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Jenrrali
Ulimwengu, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliyesimama na Profesa Shivji
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika hafla hiyo usiku huu.
Hawa ni miongoni mwa majaji kulia ni Itillio Tagalile, Afisa Uhusiano
wa Tanesco Badra Masoud na Wenceslaus Mushi wakijadili jambo.
Kushoto ni Awaichi Mawala kutoka Zantel na Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT Haika Mawala
Wageni waalikwa kutoka mashirika mbalimbali nao wamehudhuria katika hafla hiyo.
Majaji wakiwa katika meza yao.
Mwenyekiti wa bodi ya TANAPA Modestus Lilungulu kushoto na mjiumbe wa
bodi Dk.Marcelina Chijoriga kulia wakiwa katika hafla hiyo.
Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi
akizungumza na Katibu mtendaji wa Baraza la Habari MCT Kajubi
Mukajanga.
Mhariri kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo Jaquiline Liana akizungumza na Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo Juma Pinto kulia.
Clement Mshana Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji TBC akizungumza na
Profesa Helmasi Mwansoko Mkurugenzi wa Utamaduni Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wadau kutoka Shelutete kutoka TANAPA na Geofrey Tengeneza kutoka TTB nao wapo katika hafla hiyo.
Wanaharakati kutoka taasisi mbalimbali nao wamejongea katika hafla hiyo.
Kutoka kulia ni Mbunge wa Kondoa Kusini akiwa katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Leonard Thadeo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda
akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi
wa Fedha wa Kampuni ya bia ya Serengeti Graham Anderws
Bendi ya Msondo ikitumnuiza katika hafla hiyo.
Mzee wa Kammbi popote Antonio Lugas akiwa na mdau Abel Onesmo kutoka Clouds FM
No comments:
Post a Comment