Ni
Uwanja mdogo wa ndege wa Mtemere uliopo pembezoni mwa geti la Mtemere,
geti la kuingilia kwenye pori la akiba la Selous huko Mloka Rufiji. Ni
uwanja ambao unatumika zaidi na ndege ndogo ambazo huleta wageni ukanda
wa Mtemere. Selous kuna viwanja kama hivi kadha wa kadha vingiwe vikiwa
chini ya usimamizi wa hotel ambazo ndio watumiaji wakuu. Picha hizi
zilipigwa wakati wa kumalizia game walk ambapo tulikuwa tunarudi kwenye
geti la mtemere ili tuendelee na mambo mengine. unayoiona kwenye picha
ya juu ni njia ya kurukia na kutua ndege - runway - ya uwanja huu.
Mashirika
kadhaa ya ndege ndogo yana safari za kila mara (scheduled) kwenda
Selous kupitia kiwanja hiki. Coastal Air ni mojawapo.
Eneo la maegesho ya ndege wakati wa kushusha na kupakia abira.
Magari ya hoteli na makampuni mengine yakiwa pembe ya uwanja yakisubiri ndege ya coastal ili wapokee wageni wao. Coastal hupeleka ndege mara mbili kwa siku ktk kiwanja cha Mtemere. Ya kwanza hutua saa nne asubuhi na ya pili (mwisho) hufika majira ya saa kumi jioni.
No comments:
Post a Comment