Mbudya
ni Moja ya visiwa vilivyopo katika pwani ya Kaskazini mwa jiji la Dar
Es Saalam, Maeneo ya Kunduchi. Ni eneo ambalo ni tengwa kwa lengo la
kulinda na kuhifadhi viumbe wa baharini wanaopatikana eneo hilo. Hii
haizuii wageni kwenda na kupumzika kisiwani hapo. Wadau wengi hivi sasa
wamekuwa wakikitumia kisiwa hiki kama eneo la mpumziko ya weekend na
siku nyingine za wiki huku wengine wakienda mbali hadi kupiga kambi
ndani ya kisiwa - tented camping. Kipo chini ya Wizara ya Uvuvi (Sio
Utalii na Maliasili). Kimsingi kuna njia moja kuu ya kuweza kufika hapo
ambayo ni kwa njia ya Boti. Unaweza kwenda kwa boti binafsi au kwa
kutumia boti 'za umma' ambazo zinafanya safari mara kwa mara katika siku
tokea katika hoteli mbalimbali zilizopo kwenye pwani ya kunduchi.
Huduma ya boti hizi ipo ktk hoteli za white sands na Jangwani Sea
breeze. Ubao juu unakupa taarifa kadhaa za kuzingatia kama mgeni uwapo
katika kisiwa cha mbudya.
Kuwa
ktk eneo la kina kirefu kunamhakikishia mgeni wa kisiwa hiki fursa ya
kupata maji ya kina kirefu muda wowote kwa yule ambae kuogelea ni sehemu
ya starehe na mapumziko yake awapo ufukweni. Kina pWani nzuri yenye
mchanga mweupe.
Maji
yanapokuwa yamekupwa, pwani za kisiwa cha mbudya hutoa fursa kwa wageni
kuafanya michezo kadha wa kadha kwenye mchanga. licha ya hili, maji
yenye kina cha kutosha huwepo pia hata wakati wa maji kupwa (kina
kifupi), tofauti na maeneo mengine ambako maji huwa yanakuwa kama hayapo
kipindi hiki
huu
ni upande mwingine unaojulikana kama Campsite. Kuna mwekezaji alipewa
fursa ya kuanzisha na kuendesha campsite pembezoni mwa hapa, lakini
inaelekea mipango haikuwa sawia na mategemeo hali iliyopelekea baadhi ya
vitu kuachwa kama havina mwenyewe. Sasa hivi anayekuja hapa kisiwani
yupo huru kupunga upepo upande huu. Pwani ya upande huu nayo ina mchanga
mweupe na sehemu nzuri ya kuogelea pia. Kitu kimoja cha nyongeza kwa
kisiwa cha Mbudya ni kwamba mgeni una uwezo wa kuleta vyakula na hata
vinywaji vyako kama utapenda. Japo vinywaji baridi na hata vya moto
vinapatikana.
huu
ndio usafiri tulioutumia siku hii. Unafanya safari zake kati ya kisiwa
cha Mbudya na Hotel ya White sands. Hapo nahodha alikuwa anauweka sawa
tuanze kupanda na kurudi Mjini mida ya jioni.Abiria wakijivuta kwenda kupanda boti tayari kwa safari ya kurudi. Wengi wetu tulikuwa tumeanzia safari ktk hoteli ya white sands. Unaweza kuwasiliana na Mdau Omary kupitia 0713202946 ili akupe mpango mzima wa jinsi ya kufika huko na gharama husika. hata hapa, wazawa tuna punguzo la bei kwenye kiingilio cha kisiwani.
No comments:
Post a Comment