Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo, alithibitisha kutokea kwa
mauaji hayo saa Jumamosi iliyopita saa 8:00 mchana.
Waliouawa
ni Sanyiwa Ndaya (34), Lutaya Ndala (48), Nchambi Bujiku (28), Kulwa
Luhende (48) na Shija Msheshiwa (35), ambaye alifariki wakati akipatiwa
matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Ulanga. Wote wakazi wa Kijiji cha
Mguba, kata ya Igawa.
Waliojeruhiwa
na kulazwa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga ni Nkama Jisonge (35), Zina
Msheshiwa (30), Msheshiwa Taiya (60) na MT 70328 Koplo Paulo Lawrent
ambao hali zao zimeelezwa kuendelea vizuri.
Akifafanua
kuhusiana na tukio hilo, Kamanda Chialo alisema kuwa siku ya tukio
askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Job Edward (54) Ofisa Mteule wa
daraja la pili, ambaye ni mshauri wa mgambo wilaya ya Mahenge akiongoza
timu ya watu 15 akiwemo askari mwingine wa jeshi hilo, MT 70328 Koplo
Paulo Lawrent na mgambo, walikwenda katika eneo hilo kwa ajili ya
operesheni maalum ya kuwaondoa watu waliovamia hifadhi hiyo.
Kwa
mujibu wa Kamanda Chialo, watu hao baada ya kufika walivamiwa na
wananchi waliokuwa na silaha za kijadi na walipojaribu kujitetea, Koplo
Lawrent aliyekuwa na bunduki aina ya SMG alifyatua risasi hewani ili
kuwatawanya wananchi hao ambao waliendelea kupambana nao.
“Na
yeye huenda katika kunusuru silaha ile isiporwe na wananchi, alirusha
risasi hewani zilizopoteza maisha ya wananchi wanne pale pale katika
eneo la tukio, huku mwananchi mmoja akifariki dunia wakati akipatiwa
matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mahenge,” alisema Kamanda Chialo.
Kufuatia
tukio hilo, Chialo alisema watu wanane wamekamatwa na wanahojiwa na
polisi ili hatua zaidi za kisheria dhidi yao zikuchukuliwe na kuongeza
kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Awali,
ilidaiwa kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro ilikwenda
katika eneo hilo na kuwazuia wananchi kuendelea na shughuli za kilimo
na uharibifu wa mazingira katika eneo hilo la hifadhi, lakini walikataa
kwa madai kuwa hawafahamu mipaka kati ya eneo lao na eneo la hifadhi.
Inadaiwa
kuwa mipaka hiyo iliwekwa na Serikali na wananchi hao kutakiwa kutii
mamlaka ya Serikali kwa kuacha kufanya uharibifu ndani ya hifadhi bila
mafanikio, hadi ilipofanyika operesheni hiyo katika eneo hilo ambalo ni
hifadhi ya wanyamapori linalomilikiwa na wizara ya Maliasili na Utalii.
Habari kamili na Nipashe
No comments:
Post a Comment