Kutokana
na hatua hiyo, Watanzania nao walijibu mapigo kwa kuwatimua raia wa
Zambia waliokuwa wakifanya biashara zao upande wa Tanzania na hivyo
kusababisha kuibuka kwa vurugu katika mpaka huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo, akizungumza na NIPASHE jana mjini
Vwawa alisema baada ya kujulishwa kutokea kwa vurugu hizo, Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Wilaya imekwenda mjini Tunduma ambako walijadiliana
kwa pamoja na hatimaye vurugu hizo kudhibitiwa.
“Ni
kweli nimejulishwa kuwapo kwa tukio hilo. Lakini kimsingi hazikuwa
vurugu kubwa. Kamati ya Ulinzi na Usalama imeweza kulishughulikia suala
hilo na sasa hali imetulia katika mji huo,” alisema Kimolo.
Hata
hivyo, alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimechukua hatua ya
kuimarisha ulinzi katika kila kona ya mji huo ili kusitokee machafuko
zaidi yatakayoleta athari kwa wananchi wa Tunduma na wageni kutoka nchi
mbalimbali.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji wa Tunduma, Aidan Mwashiga,
alisema vurugu hizo ziliibuka baada ya wananchi wa mji wa Nakonde Zambia
kuendesha operesheni ya kuwatimua Watanzania wanaofanya biashara
zisizokuwa za halali katika mji huo.
Alisema
kufuatia hali hiyo, Watanzania nao walichukua hatua ya kuanza kuwatimua
wafanyabiashara wa Zambia wanaofanya biashara zao katika mji wa Tunduma
na kusababisha kutokea kwa vurugu.
Hata
hivyo, alisema vurugu hizo zimedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na
usalama na kwamba askari wamewekwa tayari katika mji wa Tunduma ili kama
kutaibuka vurugu ziweze kudhibitiwa.
Mji wa Tunduma umekuwa mara kadhaa ukikumbwa na vurugu zinazosababishwa na wafanyabiashara wa pande mbili.
Mwaka
2005, mfanyabiashara wa Tanzania aliuawa na askari polisi wa nchini
Zambia na hivyo kusababisha mpaka wa Tanzania kufungwa kwa siku tatu
hadi serikali ilipomaliza tatizo hilo kwa kukaa na serikali ya Zambia.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, alipofanya ziara wilayani
Mbozi, aliagiza Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kuimarisha ulinzi katika
mji wa Tunduma kufuatia kutokea kwa matukio ya vurugu mara kwa mara
katika mji huo.
CHANZO:
NIPASHE
VEMDIMI UVE AMALANGA AGO AHUFUNDISIDZE YE NANINI?
ReplyDeleteVIPI INDONYA YITONYA SANA HUNYUMBA UHO? NDILIMNYALUKOLO VAHO ILA ISAA IDZI NDILI HUMZUMBE NDISOMA HWENUHO.ALL THE BEST!