Msanii
wa Muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpozzz akifanyiwa mahojiano mara baada
ya kuwasili kwenye tamasha la Diamond Are Forever lililofanyika ukumbi
wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya, Diamond Platinum akiwarusha mashabiki
waliohudhuria katika tamasha lake la Diamond Are Forever lililofanyika
ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Diamond akionyesha umahili wake wa kuimba.
...Kumbe jini kisilani kaingia katika utamu wa penzi langu, alikuwa akiimba
...hapa alikuwa akimwaga mauno mbele ya mashabiki waliohudhuria.
Janeth Sostenes akifanya mahojiano na Godwin Gondwe.
...Aha! madansa wa Diamond wakiwajibika nae
Mashabiki wa kutosha wakifuatilia show.
...Diambond akiwajibika vilivyo
...Madansa wakiwajibika
...Safi sana
...Utata
ulianzia hapa pale Dimond alishuka stejini na kwenda kwenye meza
waliokuwa wamekaa akina Steve Nyerere na Mboni Masimba na ndipo
alipopewa t-shirt ambayo kwa mujibu wa udadisi na uchunguzi wa udadavuzi
wa mambo wa Kajuna Blog, ilisemekana kuwa t-shirt hiyo ilikuwa inapicha
ya mwanadada ambaye alikuwa akitoa na Diamond kwa sasa. Na ilikuwa ni
maalum kwa ajili ya kumrusha roho Wema Sepetu.
...Mwanadada
Mboni Masimba akimkabidhi Diamond t-shirt huku Steve Nyerere akimtunza,
vile vile alichukua t-shirt aliyopewa na kuipeleka kwa mwanadada Jokate
Mwegelo.
...Hapa akikabidhiwa t-shirt na kupewa maelekezo mahali pa kuipeleka.
...Baada ya hapo kumaliza lile movie la kwanza aliendelea na kupita katika meza mbali mbali huku akiwasalimia wageni waalikwa.
...Akiimba na bendi ya Odama ambayo alimpa ushirikia mkubwa.
...Mauno yamekolea
...Akiendelea kutoa shukrani kwa wageni waliofika kumsapoti.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Q-chief akimpa sapoti mdogo wake Diamond
...Ehe! utata mkubwa ambao ulizuka ni hapa ambapo mwanadada huyu alimtuza dola za Kimarekani, Diamond
...Diamond aliendelea kuimba huku mwanadada huyo akimtunza huku akitoa tabasamu na kicheko
Mwadada huyo hapa alikuwa amemaliza na kuondoka kwa mikogo..
Baada
ya Diamond kurudi stejini ndipo mwanadada Wema Sepetu alienda kumtuza
na pesa zake kukataliwa. Wema alikaa akimbembeleza kwa muda wa dakika 10
japo zoezi lake halikufanikiwa.
...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza
...Bembeleza, bembeleza na wewe jamaa ndiyo aliendelea kuwajibika
...Ndipo alipochukia na kuzitupia hizo hela stejini huku akiondoka huku akiwa amenuna
...Shamim
Mwasha akilaumu kitendo alichokifanya Diamond cha kukataa hela
alizoenda kutuzwa na Wema... 'Haiwezekani hii ni aibu sana'
Pesa alizokataa kuzichukua zikiwa zimetupwa
...Hapa alipiga kitu cha 'Nimpende Nani'
...Jokate na marafiki zake wakishangilia
...Baada
ya tuio hilo kutokea Mange Kimambi alimuita mshereheshaji wa tamasha
hilo, Taji Liundi na kumuomba amuite Diamond aje amuombe msamaha na
ndipo Diamond akakataa.
...Diamond alishuka na kuelekea kwa mwanadada Jokate Mwegelo na kuanza kukata mauno.
...mwanadada Mboni Masimba akiwa amevaa t-shirt alizokuwa amevaa.
...Aha! nimependeza sana
Taji Liundi akimbembeleza Diamond ili aende nae kwa Wema ndipo Diamond akakataa.
...Mwanadada Mariam (Miss Popular) akimfuta jasho Diamond wakati Taji Liundi akimbembeleza ili aende kwa Wema.
...Diamond akiserebuka na warembo
Marafiki
wa Wema Sepetu wakijaribu kumbembeleza wakati akimwaga chozi... huku
watu wengine wakishangilia na kuimba aibu yetu au aibu yao???
...hapa mwanadada akijaribu kubembeleza bila matumaini.
Msanii wa kizazi kipya, Ommy Dimpozzz akimpa sapoti Diamond...huku akitoa ushuhuda wa maisha yake na ya Diamond walipotoka.
...baada ya ujumbe wa Ommy Dimpozz, Diamond alimwaga chozi na hapa alikuwa akijifuta.
Amini nae hakuwa nyuma kumpa sapoti
...Barnaba, Amini na Diamond wakiwajibia
Baada
ya Barnaba kuimba wimbo wa 'Napembelezwa' ndipo mwanadada Wema alienda
kumtuza na kutoa machungu yake. Kwa mujibu wa uchunguzi na maoni ya watu
mbali mbali walikiona kitendo cha Wema Sepetu kwenda mbele kumtuza
Diamond ni sawa na kujidhalilisha na kuhusishwa na mambo ya kishirikina.
Pia Justmine
Loyce Bobbie alisema: Kwanini Wema anamfatafata mtoto wa watu kila
kona? amuache na maisha yake jamani.. mbona Diamond hamfatilii lol,
YATAMSHINDA