Wafungwa nchini Chad wanawekwa katika mazingira mabaya kiasi kuwa wanaotumikia kifungo wako katika hatari ya kufa jela.
Kulingana na shirika la Amnesty
International, wafungwa wanawekwa katika magereza yaliyosongamana watu
na kukosa hewa safi. Na yote hayo waliyashuhudia wakati walipotembelea
magereza sita.Shirika hilo linasema kuwa wafungwa wanawake wanaishi katika hatari ya ubakaji na wengi wakiishi na watoto wao wenye hata miezi saba ndani ya magereza.
''Sio vyema wafungwa kuishi katika mazingira mabaya kama yale, mabaya sana kiasi cha mfungwa kuwa katika hatari ya kufia gerezani.'' alisema mtafiti mkuu wa shirika hilo Christian Mukosa.
"wafungwa wengi walikuwa na utapia mlo wakionekana wadhaifu sana. Baadhi walifungwa minyororo siku nzima wengi wakiugua maradhi ya ngozi, maradhi ya ngono, Malaria au Kifua kikuu" aliongeza Christian.
Shirika hilo limetoa wito kwa serikali kuchunguza madai hayo ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Serikali ya Chad bado haijajibu ripoti hiyo ya Amnesty.
No comments:
Post a Comment