Jeshi la Mali linasema kuwa
limewapiga risasi na kuwauwa watu 16 katika jimbo la Segou, katikati mwa
nchi, baada ya gari la watu hao kutosimama kwenye kituo cha ukaguzi.
Inaarifiwa kuwa baadhi ya wale waliouwawa ni wahubiri wa Kiislamu kutoka Mauritania, ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wa kidini nchini Mali.
Waandishi wa habari wanasema huenda kuwa jeshi liliwafikiria wasafiri hao kuwa wapiganaji wa Kiislamu ambao wanadhibiti eneo la kaskazini mwa Mali.
No comments:
Post a Comment