Ustaarabu na Ushenzi ni vitu vinavyofanana
Ustaarabu...
Ustaarabu na ushenzi ni vitu vinavyo
fanana sana. Na wala sio rahisi kupambanua upi ni ustaarabu hasa na upi
ni ushenzi. Kwa maana kile kinachoitwa ustaarabu kwa mtu mmoja kinaweza
kuwa ushenzi kwa mtu mwingine na ushenzi kwa huyu unaweza kuwa ustaarabu
kwa yule.
|
Mdada asilia |
Si ajabu wakoloni walipokuja waliuita utamaduni wetu eti ni wa
kishenzi. Tunapoishi katika jamii tunaupima ustaarabu kutokana na
kawaida (norms) ya watu wanao tuzunguka. Tatizo ni kwamba mara nyingine
huo tunaouita ustaarabu kumbe ndio ushenzi hasa kuliko ule tunaodhania
kuwa ndio ushenzi.
|
Halle Berry |
Inanishitua sana
ninaposikia kampeni za kuhimiza kukubalika kwa ndoa za jinsia moja.
Inanishangaza ninapoona viongozi wa dini na watu wanaoheshimika sana
wakisisitiza wanaume wanaojifanya wanawake na wanawake wanaojifanya
wanaume wapewe haki ya kufunga ndoa na kuheshimiwa kama wanandoa wengine
kwa sababu eti huo ndio ustaarabu. Inanisumbua ninapoona wanawake na
wanaume wakijitembeza mitaani kuuza uroda kana kwamba ni njugu kwa madai
kwamba huo ni ustaarabu...
|
Jeniffer Lopez |
Inaniuma sana ninapoona wezi wa mali ya
umma wakitukuzwa, kushangiliwa, kulindwa na kupewa nafasi zajuu zaidi
za uongozi kwa sababu eti huo ndio ustaarabu...Inanikera ninapoona
viongozi wanazidi kujilimbikizia mali, kujenga himaya za kifalme,
kutumia mabilioni ya shilingi za wavuja jasho kwa matumizi yasiyo ya
lazima huku wakiwaacha wananchi wakiteseka kwa kukosa huduma muhimu kama
afya (matibabu) umeme, maji, na usafiri wa kuaminika mijini. Inanitia
kichefuchefu kwamba madaktari wetu wanafikia kugoma kwa madai ya fedha
huku wanasiasa wakilimbikiziwa posho kiasi cha kuogopa kuzipokea kwa
aibu...huu nao ni ustaarabu.
|
Lady Gaga |
Zaidi ya yote inaniuma sana ninapoona
watoto wetu wakifundishwa ubinafsi, kutothamini utu, kutomuogopa Mungu
kwa imani kwamba hayupo (ha exist) na kupewa uhuru mkubwa kuliko mtoto
anaostahili kuwa nao kwa kisingizio cha haki za watoto, eti nao ni
ustaarabu...Wallah kama huu ndio ustaarabu ni bora turudi kwenye
kutembea uchi maana naamini watu walikuwa wastaarabu zaidi kuliko
sasa...
No comments:
Post a Comment