Zaidi ya
wakimbizi 100,000 wa Syria waliitoroka nchi yao mwezi Agosti pekee, hii
ikiwa ndio idadi kubwa zaidi ya wakimbizi kutoroka Syria tangu vita
kuanza mwezi Machi .
Msemaji wa umoja wa Mataifa nchi humo amesema kuwa watu hao wanakimbilia nchi jirani.Misaada imeanza kupungua mjini Allepo mojawapo ya maeneo ambako mapigano yanaendelea, huku ikisemekana kuwa vigumu kuweza kufikia sehemu nyingi za mji.
Watu watano waliuawa leo katika mkoa wa kaskazini , siku moja tu baada ya watu wengine 25 kuuawa katika shambulizi la angani.
Wanaharakati wa upinzani walisema kuwa watu wengi walijeruhiwa katika shambulizi la makombora lililofanywa na majeshi katika eneo la Darat Izza mjini Allepo.
Afisaa mkuu mtendaji wa shirika la msalaba mwekundu anatarajiwa kukutana na maafisa wengine wakuu wa serikali ya Syria pamoja na kuzuru baadhi ya vitongoji vya mji mkuu Damascus vilivyoathiriwa na mapigano.
Hata hivyo hakuna maelezo yoyote yametolewa kuhusu mazungumzo ya bwana Maurer na Assad lakini msemaji wa shirika hilo, Cecilia Goin aliambia BBC kuwa shirika hilo linatazamia kuongeza juhudi zake za misaada kote nchini Syria.
No comments:
Post a Comment