Namshukuru Mungu kuzaliwa Tanzania, Nchi iliyobariliwa kila aina ya utajiri
duniani, mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi kwa kila kitu ndiomana nchi kama za
mashariki ya mbali ulaya na amerika zimetajirika kupitia maliasili za watanzania
tuliolala usingizi bila kujua wapi tunaelekea na hii baiskeli yetu ya miti,
kwanza napenda kutoa pole kwa ndugu zetu wote waliopoteza maisha kwenye matukio
tofauti kama mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto,kuzama kwa meli ya MV BUKOBA,MV SPICE, MV SKAGIT, tumepoteza nguvu kazi
kubwa ya taifa, lakini yote tisa sijui ni tatizo nini ukiuliza tumeunda tume
tuwaachie tume wafanye kazi yao, yakitokea tena oooh nimakosa yakimaumbile sisi
ni ngumu kuyazuia, wenzetu
wanazidi kuteketea, nchi inaingia gizani wawakilishi
wetu wanakula rushwa wanaanza kurushia vijembe bungeni mambo yanapita hakuna
hatua zilizochukuliwa, dah inaumiza sana, hivi napenda kuuliza tunaangalia
maisha ya mjini tu au na watu wa kijijini tumewasahau, kwa sababu inasikitisha
kuniambia uchumi umekuwa wakati watu zaidi ya milioni kumi hawajui watakula nini pale
wanapofika muda husika kwa sababu hata shilingi mia moja hawana mfukoni. Mnamo
mwaka 2010 nilibahatika kufanya utafiti katika mkoa wa Rukwa wilaya ya
sumbawanga vijijini jimbo la kwela kuhusu kushuka kwa elimu katika mkoa wa
Rukwa, ni masikitiko makubwa sana pale ukiipata hiyo taarifa nafikiri serikali
ifike pahala iseme kuna maeneo tumeshindwa kufikia malengo na watoe taarifa kwa
nini wameshindwa hili hata wananchi watafute namna nyingine ya msaada hili
wajikomboe na tatizo hili la uchumi.
Madini ya Tanzanite
Tatizo lingine vijana wakitanzania
tuliowengi tunapenda mijadala ambayo haijengi nchi ni kubomoa nchi kwa sababu ya
itikadi ya chama, na pili tumeshajiwekea katabia kakutofanya kazi sijui
tunategemea nini, jamani hii nchi hawa jamaa wanaipeleka sehemu ambapo palipo
tufanya tuwaone wakoloni wabaya, na watu wa kurekebisha hayo maswala ni sisi si
wao, sasa tufike pahala jamani watanzania wenzangu tuangalie maisha haya na nchi
yetu inapokwenda. ni mtazamo wangu
No comments:
Post a Comment