NJOMBE

NJOMBE

Saturday, September 8, 2012

Wahamiaji haramu matatani Italia

Wahamiaji haramu waokolewa
Walinzi wa mwambao kutoka shirika la majeshi ya muungano ya NATO wanawatafuta manusura wa boti iliyozama ufuoni mwa kisiwa cha Lampedusa ambapo mtu mmoja alifariki na wengine wengi bado hawajulikani waliko.
Manusura wengine 56 wakiwemo wanawake wajawazito wameokolewa kutoka kwenye boti hiyo iliyozama mapema leo asubuhi.
Kisiwa cha Lampedusa ambacho kiko umbali wa kilomita 120 kutoka Tunisia, ni eneo ambalo hutumiwa na wahamiaji wengi haramu wa kiafrika kuingia barani Ulaya kwa sababu ya ukaribu wake kwa bara hilo.
Maafisa wanasema kuwa idadi ya watu waliokuwa kwenye boti hiyo heunda ikawa zaidi ya miamoja ikilinganishwa na idadi iliyokuwa imeripotiwa awali.
Baadhi ya manusura waliokolea kutoka baharini na wengine walikuwa kwenye sehemu ya kisiwa hicho ambako hakuishi watu.
Msemaji wa walinzi wa NATO, alinukuliwa akisema watu 56 wamepatikana wote raia wa Tunisia.
Mnamo siku ya Alhamisi, watu 56 walizama wengi wao wakiwa watoto baada ya boti yao kuzama Magharibi mwa pwani ya Uturuki.
Wengine 45 waliokuwa kwenye boti hiyo walinusurika.
Wahamiaji hao haramu walikuwa wairaqi, raia wa Syria na wapalestina wakikimbilia barani Ulaya.
Kulingana na shirika la kimataifa la Amnesty International, mnamo mwaka 2011, takriban watu 1,500 walizama katika bahari ya Mediterranea wakiwa njiani kuelekea barani Ulaya.
Wengi walikuwa wanatoroka vurugu nchini Tunisia na Libya,wakati wa harakati za mageuzi katika nchi za kiarabu.

No comments:

Post a Comment