Wabunge 257 wa bunge jipya
Somalia leo wanatarajiwa kumchagua rais wa nchi hiyo katika hatua ya
hivi karibuni kuleta amani nchini humo.
Wabunge hao wapya wanakusanyika katika kituo cha mafunzo kwa polisi mjini Mogadishu kuanza kupiga kura.Serikali ya mpito ambayo imedumu kwa muda wa miaka minane itakabidhi mamlaka kwa serikali mpya baada ya uchaguzi wa rais.
Rais wengi wa Somalia walilazimika kuikimbia nchi yao kufuatia hali mbaya ya usalama nchini Mwao.
Baadhi yao wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya wamekuwa na hisia mbali mbali kuhusu na mchakato wa kuleta amani na usalama pamoja na uthabiti unaoendelea nchini Somalia.
Mwandishi wa BBC mjini humo Daud Aweis anasema kuwa shughuli itachelewa kuhu wabunge wakipitia ukaguzi mkali kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi huo.
Ni Mara ya kwanza kwa miaka mingi kwa rais kuchaguliwa nchini Somalia ikiwa ni ishara ya usalama kuimarika.
Hata hivyo kundi la wapiganaji la al-Shabab, bado linadhibiti maeneo mengi ya kusini na katikati mwa Somalia.
No comments:
Post a Comment