NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, January 15, 2013

Nigeria kutwaa kombe la Afrika 2013?

SPORTS/MICHEZO

 
Kikosi cha Nigeria
Wacheza kamali wanataka kucheza karata zao vizuri kuhusu kinyang'anyiro cha ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013. Wacheza kamali hao wataelekeza karata yao katika timu ya Nigeria wakiipa nafasi ya kuwa katika timu tatu bora za juu.
Timu ya Nigeria, The Super Eagles, imeshiriki mara 16 katika mashindano ya kombe hilo na kushinda mara mbili, ikishika nafasi ya pili mara nne na mara saba katika nafasi ya tatu, ikiwa ni rekodi ya kujivunia katika kipindi cha miaka 50.
Ni katika mwaka 1963 na 1982 (ikiishia raundi ya kwanza) na 2008 (robo fainali) Eagles wakishindwa kutwaa medali na wanaonekana wamejipanga angalau kuingia nane bora katika fainali za mwaka 2013 nchini Afrika Kusini baada ya kupangwa katika kundi C pamoja na timu za Burkina Faso, Ethiopia na Zambia.
Kocha wa timu ya Nigeria, Stephen Keshi
Timu zinazoshika nafasi ya kwanza na ya pili katika makundi, husonga mbele na kuingia robo fainali. Nigeria na mabingwa watetezi Zambia wanapewa nafasi ya kusonga mbele. Kwa mshangao timu ya Nigeria, The Super Eagles, walishindwa kufuzu katika fainali za mwaka 2012zilizoandaliwa kwa pamoja kati ya Gabon na Equatorial Guinea na ilimgharimu kocha wake Samon Siasia wakati aliposhindwa kuongezewa mkataba.
Kocha wa sasa Stephen 'Big Boss' Keshi, kocha asiye na mzaha ambaye alikuwa katika kikosi cha wachezaji wa Nigeria walioishinda Zambia kwa kuilaza magoli 2-1 katika fainali zilizofanyika Tunisia, miaka 19 iliyopita. Alikuwa mchezaji kiungo imara ambaye aliongoza kwa mfano na alitumia wiki chache zilizopita kufanya mazoezi katika kambi nchini Ureno akijaribu kujenga moyo wa ushindi kwa timu yake ya Super Eagles.
Obi Mikel akidhibiti mpira
"Nataka wachezaji wenye njaa ya kusaka ushindi, wenye kujitolea na ambao wanajivunia kuchezea timu ya taifa ya Nigeria," amesisitiza kocha huyo ambaye alipambana na Togo na Mali bila kufuzu hatua ya kwanza katika mashindano yaliyotangulia ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
"Ni vizuri kuona wachezaji wakifanya jitihada kuwania namba katika kikosi changu cha kwanza. Ushindani huo unanipa changamoto nzuri. Hakuna mwenye namba ya kudumu katika timu-- ni lazima wapiganie na pia wapiganie kuhifadhi namba wanayopataKocha wa Mlinzi wa kati na nahodha wa Super Eagles, Joseph Yobo, analeta changamoto sawa katika rekodi ya mchezaji bora wa zamani wa mwaka wa Afrika Nwankwo Kanu kwa kucheza katika fainali sita za Kombe la Afrika.
"Kushinda kombe si kazi rahis lakini naahidi kutafanya kwa uwezo wetu wote kufikia lengo hilo. Nawaomba Wanaigeria kutuombea na kuwa na imani na timu hii,"anasema mchezaji huyo kiungo wa zamani wa Everton ambaye kwa sasa anacheza soka nchini Uturuki.
"Tunasafiri kwenda Afrika Kusini tayari kupeperusha bendera ya taifa letu na hatutachoka hadi tutakapotimiza lengo letu. Bahati nzuri tuna kikosi kizuri cha wakufunzi ambacho kinatufahamu vizuri na nina uhakika wachezaji wako tayari kwa hilo.

No comments:

Post a Comment