NJOMBE

NJOMBE

Friday, November 23, 2012

Wachezaji 5 watangazwa

Tuzo mchezaji Bora wa BBC 2012
Tuzo mchezaji Bora wa BBC 2012
Majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka 2012 yametangazwa.
Yaya Toure, kwa mwaka wa pili mfululizo, yupo kwenye orodha hiyo.
Mwenzake katika timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba pia yumo.
Wachezaji wengine ni pamoja na Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na nahodha wa timu ya Zambia, Christopher Katongo.
Huu umekuwa ni mwaka wa ufanisi kwa wachezaji hao, na timu za wachezaji wanne zikionyesha ustadi kwa kupata vikombe.
Bofya Ukitaka kupiga kura unaweza kufungua anwami hii ya mtandao na kumbuka maagiza yametolewa kwa lugha ya Kiingereza.
Inaelekea Drogba aliondoka Chelsea wakati muwafaka, mara tu baada ya timu yake kukamilisha msimu kwa ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya, hii ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya klabu, na vile vile akipata bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA.

Wanaowania tuzo la BBC

Yahya Toure Bofya Yahya Toure.Mcheza kiungo kutoka Ivory Coast, anayeichezea Manchester City ya Uingereza. Toure aliiongoza Manchestert City kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 44 iliyopita.
Demba Ba Bofya Demba Ba kwa sasa ni mmoja wa wachezaji nyota wa klabu ya Newcastle na kufikia sasa tayari amefunga jumla ya magoli 6 katika ligi kuu ya premier la England na anatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Senegal kitakachocheza katika fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika.
Didier Drogba Bofya Didier Drogba ni noadha wa timu ya taifa ya Ivory Coast, amewahi kuongoza Chelsea kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England pamoja na kombe la klabu bingwa barani ulaya.
Chrsitopher Katongo Bofya Christopher Katongo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo na aliiongoza timu hiyo kushinda fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika
Younes Belhanda Bofya Younes Belhanda ni mchezaji mwenye umri wa miaka 22, na mmoja wa wachezaji waliotia fora na kuisaidia klabu ya Montepellier, kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya karne moja tangu klabu hiyo ilipobuniwa.
Raia mwenzake wa Ivory Coast, Toure, naye akiichezea Manchester City, aliihakikishia timu yake ubingwa wa ligi kuu ya Premier kwa mara ya kwanza; kombe lao muhimu zaidi katika kipindi cha miaka 44.
Belhanda aliisaidia timu yake ya Ufaransa ya Montpellier kupata ushindi katika ligi ya Ufaransa daraja la kwanza, kwa kufanikiwa kupata magoli 12 katika msimu.
Katika mapambano ya kimataifa, Katongo, kutoka Zambia, naye akiiongoza timu kama nahodha, alifanikiwa kuiwezesha timu yake ya Chipolopolo kuishinda Ivory Coast, na kuibuka mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kuishinda Ivory Coast katika fainali, kupitia mikwaju ya penalti.
Ba hakung'ara katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya Senegal kuondolewa katika hatua ya makundi, lakini binafsi aliweza kuifanyia timu yake ya Newcastle kazi nzuri, na msimu uliopita alitangazwa kuwa mshambulizi bora zaidi, kwa kufunga jumla ya magoli 17, na kuiwezesha timu kumaliza katika nafasi ya tano.

No comments:

Post a Comment