NJOMBE

NJOMBE

clock

Thursday, November 15, 2012

Nani kasema uaminifu hakuna siku hizi,Tusikate Tamaa…Uaminifu bado UPO!

Wengi tumekata tamaa ati uaminifu haupo tena. Nikutie moyo kuwa UAMINIFU bado upo. Usipoupata ama kuuona pembeni yako pengine ukisafiri mahali fulani utaukuta.
Kijiji cha mwisho cha mkoa wa Njombe kilichoko kwenye barabara kuu ya kwenda Ruvuma utakuta kijiwe cha mzee mmoja mstaafu wa JWTZ (Jeshi la Wakurya Tangu Zamani!) akiuza miwa, matunda na asali mbichi.
Kilichoshangaza kwangu mimi ni tangazo lilopo hapo kwenye kibao na birika ambalo linatumika kama KIBUBU.
IMG_0782
Kibao kisemacho Angalia Bei-Kama Hatupo Fedha weka kwenye Birika
IMG_0787
Mzee wa Boma.

No comments:

Post a Comment