NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, November 27, 2012

Hivi ndivyo alivyosema kamanda wa Polisi juu ya kifo cha Sharoo

Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe

GARI NA MAHALI ALIOPOKATIA ROHO SHARO MILIONEA


Hili ndilo gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T278 BVR ilipinduka na kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha msanii Sharo milionea USIKU WA JANA MIDA YA SAA MBILI USIKU
VIDIO AMBAZO SHAROO ANAHUSIKA
  
HIVI NDIVYO MWILI WA MAREHEMU SHARO MILIONEA ULIVYO BAADA YA KUPATA AJALI ** TUNAOMBA RADHI KWA PICHA UTAKAYOONA **

No comments:

Post a Comment