NJOMBE

NJOMBE

clock

Thursday, November 15, 2012

Isikilize hii kutoka kwa Rah P.Inasikitisha na inafundisha

Fredinah Peyton a.k.a Rah P


Fredinah Peyton a.k.a Rah P ni msanii wa Hip Hop wa kike kutoka Tanzania.Wengi walijiuliza kuwa dada huyo amepotelea wapi.Rah P yupo Marikani kwa sasa akifanya maisha yake mwenyewe.Je unajuwa ni nini kilimpeleka Marekani,Rah P alienda Marekani kwa lengo la kusoma na alisoma takribani miaka miwili na alikuwa akipata msaada toka Tanzania yani nyumbani na alikuwa akifanyakazi zahapa na pale.Lakini kwa kipindi kifupi hakupata tena hayo mahitaji yake toka nyumbani.Rah P akashindwa kuendelea na shule,Lakini kwa kipindi kifupi alipata mchumba ambaye walikuwa kipendana sana aliyemuahidi kuendelea kumlipia shule na hivyo kabla ya kujuwa mengi zaidi juu ya huyo mpenzi wake alipata ujauzito na kupata mtoto wa kwanza na hivyo jamaa akashindwa na hakutaka kusikia habari ya shule sababu yakuwa na majukumu mengi,Hivyo Rah P akawa ni mama wa nyumbani na akiwa anasoma tu kupitia mtandao (online school) hakuwa anajisikia vizuri kaa tu nyumbani na kuwa mtu wa kulea watoto sababu alijuwa kama kitu chochote kitatokea juu ya huyo mchumba wake atakuwa na kitu cha kumsaidia.Kulingana na maisha livyokuwa jamaa alikwa ni mtu wa kwenda huku na kule akipiga dili zake hivyo Rah P akaendelea na maisha na akapata ujauzito wa pili na wakati huo anapata ujauzito yule jamaa alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.Kwakuwa huyo jamaa alikuwa ni mfanyabiashara ya madawa ya kulevya.Rah P akawa amepatwa na msongamano wa mawazo hivyo akawa ni mlevi mlevi kupindukia iliyompeleka na yeye pia kufungwa jela na mtoto wake wakiume alikuwa na umri wa miezi mitano(5) na wakike umri wa miaka miwili(2) ila alitoka na kugunduwa nijambo gani yampasa afanye kama mungu anavyopendelea awe.Na hivi sasa ameamuwa kuendelea na fani yake ya muziki na kafanya ngoma moja aliyoshirikishwa na mshindi mara mbili wa Tursker Project Fame.Mrwanda Alpha Rwirangira na nyimbo hiyo inakwenda kwa jina la African Swagger
Alpha Rwirangira
 Msikilize hapo wewe mwenyewe umsikie anavyotoa historia yenye kutia majonzi


                            African Swagger-Alpha ft Rah P

No comments:

Post a Comment