Naam
katika mahusiano tamaduni na miiko mbali mbali huingilia kati. Vijana
hukutana na vizingiti zaidi katika hili. Dini za kigeni zinamaoni yake
katika hili wakati tamaduni na dini za kiasili nazo huwa na mitizamo
yake.
Tamaduni
nyingi za kiafrika zilipinga sana upatikanaji wa Mimba kwa binti kabla
ya kuoelewa. Katika jamii za wahaya kwa mfano, binti aliyepata mimba
katika kipindi hicho alikabiliwa na hadhabu kali ya kifo cha kikatili.
Mchumba alitafutwa na kukubaliana kati ya wazazi husika na wanandoa
kukutanishwa baadae
Dini
nyingi za kigeni kama vile ukristo na uisilamu nazo zina tamadmuni zake
kwa wachumba na wanandoa. Wale waliobahatika kupata mimba kabla ya
kufungishwa ndoa na kiongozi wa dini, hupewa adhabu Fulani Fulani za
kiimani kama kutoshiriki kiitwacho chakula cha bwana au hata kutengwa
mbali kabisa na nyumba za ibada
Katika
mahusiano ya kisasa vijana nao huja na mambo yao. Huu utumika kama
wakati wa kujifunza mapenzi yenye ashiki na hisia kali. Hapa wengi
hawaambiliki na hujiona wamefika na wanajua kila kitu katika massuala ya
mahusiano. Kumbuka tunapokua na kujijua na kutoka nje ya nyumba za
wazazi/walezi wetu, jambo kubwa huwa ni mahusiano ya kimapenzi a watu wa
jinsia tofauti na za kwetu.
Huwa
ni kipindi kigumu cha kujifunza masmuala haya magumu bila kufata
utaratibu wowote namwisho huwa ni maumivu ya kuachana na Yule ambaye mtu
aliamini ni wa milele. Hata hivyo maumivu haya huwa sio halisi kwani
huko mbeleni huja kukutana na wapenzi wengine ambao hupendani sana
kuliko wale wa zamani. Kuna wanaozunguka na kurudiana na wale wa zamani
Wazazi
wengi hawawasaidii vijana wao katika masuala ya mahusiano isipokuwa
wengi huwaingilia na kutaka kuwa tafutia wenza au hata kuwapiga mkwara
juu ya mambo haya.
Ndoa hunukia kwa mbali
No comments:
Post a Comment