Mapigano yanaendelea Syria
Idadi ya watu waliofariki
kufuatia mashambulio ya bomu inazidi kuzua masuali juu ya jukumu la
waangalizi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo.
Jukumu lao ni kusimamia na kuona kua mapigano
yanasimamishwa. Lakini ingawa hilo limetimizwa katika baadhi ya maeneo
ukweli ni kwamba mapigano bado hayajamalizika.Imani iliyokuepo ilikua kwamba endapo watatumwa wasimamizi kutoka nje huenda wakasaidia kushawishi wakuu wa serikali kutimiza ahadi zao za kukomesha ghasia.
Lakini tangu mwanzo, kuwepo kwa wasimamizi hawa kulizua suali jipya kuu: Endapo mashambulizi dhidi ya raia yataendelea Je nini kitafuata?
Umoja wa Mataifa utachukua hatua gani zaidi ya hio? Na ni mazingira gani yatafanya Umoja wa Mataifa ukubali kua mpango wake umeshindwa?
Tatizo ni kua hakukuepo mpango mbadala endapo huu utashindwa.
Mpango pekee ambao Jumuia ya kimataifa uliweza kukubaliana kwa sauti moja ni huu wa kutuma wasimamizi. Pamoja na maneno mazuri ya kuvutia ya njia za kupitia kunusuru maisha bila bughdha au njia nyingine za upatanishi, hakuna yeyote aliyetaka kuhusika moja kwa moja na matatzio ya Syria.
Mgogoro wa Syria umeanza kujenga sura ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na Umoja wa Mataifa haujajiweka tayari kutangaza ujumbe wa tume yake umeshindwa kwa sababu hakuna yeyote anayyeweza kujibu suali - Nini kitafanyika sasa.
No comments:
Post a Comment