NJOMBE

NJOMBE

Thursday, May 17, 2012

Bosco Ntaganda aingiza watoto jeshini

Jenerali mtoro Bosco Ntaganda, ambae anasakwa na mahakama ya kimatiafa ya jinai -ICC bado anajumuisha watoto katika jeshi lake.
Watoto wapiganaji wa Bosco Ntaganda

Shirika la Human Rights Watch (HRW) linasema kuwa katika mwezi uliopita watoto wapatao 150 wa kike na wakiume wamejumuisha jeshini.
Watoto hao wote wanatoka katika eno la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
wale ambao wamefaulu kutoroka wanaelezea kuwa wengi wao walichukuliwa toka shuleni na vijijini na kuamrishwa kwa bunduki kiunga na wapiganaji wa Bosco Ntaganda.
Mahakama ya ICC mwaka wa 2006 iliamuru Jenerali Bosco Ntaganda akamatwe na kushitakiwa.
Sasa Shirika la Human Rights Watch lenye makao yake New York, Marekani limesema kuwa watoto wanaolazimishwa kuingia jeshini ni wa kati ya umri wa miaka 12 hadi 20.
Uchunguzi wa Human Rights watch unasema kuwa shughuli hiyo ya kuwakamata watoto na kuwaingiza jeshini lilianza kutekelezwa pale wafuasi wa Bosco Ntaganda kuasi jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wafuasi hao walikuwa chini ya kikosi cha Ntaganda cha CNDP ambao walijumuishwa katka jeshi la Congo.
Lakini kufikia sasa Jenerali Ntaganda amekanusha kuchochea maasi katika jeshi la Jamhuri ya Congo.
Inaaminika kuwa Jenerali Bosco Ntaganda anajificha katika mbuga ya Virunga , sehemu iliyo maarufu sana kwa sokwe.
Hata hivyo serikali ya Congo imeahidi kumsalimisha Bosco Ntaganda katika mahakama ya kimatiafa ya jinai -ICC -iwapo itamtia nguvuni.

No comments:

Post a Comment