Si mbali na palipotupwa plastiki hizi pana hoteli hii marufu na nzuri ya Silversands ambapo watalii na wenye uwezo wanakaribishwa kwa maua mazuri yenye asili ya Kimarekani yaitwayo Bougainvillea. Ikiwa tunaweza kuyapamba mazingira ki-azizi, hatushindwi kuyaacha safi…
Nilishangazwa nilipoelezwa na muuza madafu mmoja Dar kuwa kinywaji (chakula) hicho muhimu siku hizi hakipatikani kirahisi. “Minazi inakatwa ovyo…” akalalama.
Nilipokuwa kitongoji hiki cha Dole, Unguja, nikawa nawaza lile balaa la minazi kukatwa bandari ya Dari Salama. Minazi imesimama dede mithili ya twiga au mbuni malishoni. Je, itadumu?
Sehemu nyingi Zanzibar bado vyakula asilia vinathaminiwa. Cheki matunda, mboga na makulaji : mjini na vijijini. Ama kweli inatia moyo…maana chakula ni utamaduni wa nchi; kama huna au unaiga (huthamini chako) huna jicho…
Huku unakula huku unafikiria namna ambavyo bado wananchi wengi tunatupa chupa za maji ovyo nje; tunavyofungia bado vyakula vyetu kwa magazeti badala ya mifuko isiyokuwa na sumu na madawa…
Kinamasi hiki kimejaza si tu plastiki na dawa zenye sumu bali pia wadudu kama mbu. Kila anayeweza (kutumia mtandao na kompyuta ni uwezo na nafasi) kuelemisha watu wetu ajitahidi na kujaribu…maana hizi blogu hazisomwi na wengi.
Hapa natia tizi katika moja ya bichi za Dar…ukweli si rahisi siku hizi kupata ufukwe msafi mjini hapa. Na hata zile safi baada ya kuogelea unahisi macho yakikuwasha washa. Watalaam wameonya kuhusu kutupa taka ovyo baharini, kunya (na kukojoa) ovyo ufukweni, kuchafua michanga kwa vyupa vya vinywaji tunapostarehe kando ya bahari mama ya Hindi.
No comments:
Post a Comment