NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, May 15, 2012

Raia wa Sudan Kusini wafika nyumbani

Raia wa Sudan Kusini

Ndege ya kwanza iliyowabeba wakimbizi waliokwama kwa miezi kadhaa nchini Sudan imewasili mjini Juba Sudan Kusini. Raia hao wapatao 164 wanatarajia kusafirishwa kwa barabara hadi katika kambi mpya wakisubiri kutafutiwa jamaa zao.
Kundi hili ni la raia laki tano ambao walipoteza uraia wao baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake mwaka jana. Nchi hizo nusura kuingia vitani kutokana na mzozo wa raslimali za mafuta na mipaka.
Raia waliofika leo wamekuwa katika jimbo la Nile ambapo walipewa hadi Mei 20 kuamua ikiwa watachukua uraia wa Sudan au kurejea Sudan Kusini.
Maafisa wa Sudan wamepinga hatua ya kuwasafirisha raia hao kwa wingi kwa hofu ya usalama.
Punde baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake maelfu ya raia wake waliofanya kazi katika iliyokuwa serikali ya taifa moja la Sudan waliachishwa kazi na utawala wa Khartoum.
Kuna kambi maalum mjini Juba ya raia hao kabla ya kutafuta maeneo yao ya asilia.
Maelfu ya raia wa Sudan Kusini walihamia Kaskazini wakati wa vita na kutafuta ajira.

No comments:

Post a Comment