Shirika la kutetea haki za
kibinadam la Human Rights watch, ambalo limechapisha ripoti kuhusu kile
kilichotaja kama sera ya serikali ya Syria, ambayo ni sawa na uhalifu na
ukatili dhidi ya binadam.
Ripoti hiyo imenakaili mahala ambako serikali ya
nchi hiyo imejenga vituo vya kuwazuia wapinzani wake na mbinu ya mateso
inayotumika.Shirika hilo limetoa wito kwa wale wanaohusika kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Haque, amesema viwango vya vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na serikali ya Syria Dhidi ya raia wake ni vya kushangaza.
Amesema wahusika wote wanapaswa kuwajibishwa.
Awali afisa mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na haki za kibinadam Navi Pillay ameonya kuwa viwango vya ukiukwaji wa haki za kibinadam vinaendelea kuongezeka nchini Syria.
Pillay, amesema ghasia nchini Syria, zinaendelea kuchochewa na kuongezeka kwa idadi ya silaha miongoni mwa wanajeshi wa serikali na upinzani.
Upinzani nao ukipewa silaha na serikali za Qatar na Saudi arabia.
Awali Muungano wa nchi za Kiarabu, ulitoa wito kwa upinzani kuungana na kuafikiana kuhusu mpango kwa kipindi cha mpito nchini humo.
Kiongozi wa Muungano huo, Nabil Al Arabi, ameliambia kongamano la wanaharakati wa upinzani mjini Cairo, Misri, kuwa Syria, inahitaji mfumo wa Kidemokrasia ambao hautabagua mtu yeyote.
Wakati huo huo, vyombo vya habari nchini Uturuki, vimesema kuwa wanajeshi 85 wa syria wakiwemo generali mmoja na maafisa wengine 7 waandamizi wamevuka mpaka na kuingia nchini humo.
Mashirika hayo ya habari yametaja kundi hilo kama kubwa zaidi la kijeshi ambalo limeasi na kuingia nchini Uturuki tangu machafuko ya kisiasa kuanza nchini Syria.
Kundi hilo linaripotiwa kutumwa katika kambi moja ya wakimbizi Kusini mwa Uturuki.
Wiki iliyopita, kundi lingine la ziadi ya wanajeshi 30 na familia zao wakiwemo maafisa kadhaa wakuu walivuka mpaka na kuingia Uturuki.
No comments:
Post a Comment