Korea Kusini imetangaza kuwa
inataka kuanza uwindaji wa nyangumi chini ya sheria inayoruhusu uvuvi wa
nyangumi kwa minajili ya utafiti wa kisayansi, kama vile serikali ya
Japan inavyofanya kwa sasa.
Serikali ya Korea Kusini, ilifichua hayo wakati
wa mkutano wa kimataifa wa baraza linalosimamia na kulinda maslahi ya
nyangumi nchini Panama, ambako walikuwa wakiwasilisha mipango yao kwa
kamati ya sayansi ili kuchunguzwa.Nyangumi hao watawindwa karibu na pwani ya Korea lakini haijulikana ni wangapi.
Uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya biashara imepigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa, lakini uwindaji wa nyangumi kwa minajili ya utafiti unaruhusiwa, hata kama nyama yake italiwa baadaye.
Korea ina historia ya ulaji wa nyama ya nyangumi kuliko eneo lolote ulimwenguni, na inakisiwa kuwa urauibu huo ulianza takriban miaka elfu nane iliyopita.
No comments:
Post a Comment