NJOMBE

NJOMBE

Monday, June 18, 2012

Ulipizaji kisasi watokea Nigeria

Mashambulio kadha ya mabomu yamefanywa dhidi ya makanisa katika jimbo la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria.
Shambulio la bomu la karibuni mjini Kaduna
Ripoti zinasema watu zaidi ya 10 wamekufa.
Miripuko miwili ililenga makanisa karibu na mji wa Zaria, wakati ibada zinaendelea.
Katika mji wa Kaduna, mashambulio ya karibuni yamezusha ulipizaji kisasi dhidi ya Waislamu, ambapo waislamu walibururwa kutoka magari yao na kuuwawa.
Wakuu wa Kaduna wameweka amri ya kutotoka nje kwa saa 24, na wanajeshi na polisi wanajaribu kurejesha utulivu.
Hii ni Jumapili ya tatu mfululizo ambapo makanisa yameshambuliwa kwa mabomu katikati mwa Nigeria.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, lilikiri kufanya mashambulio ya siku za nyuma.

No comments:

Post a Comment