NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, July 30, 2013

Dawa na njia nzuri za Kupunguza unene

-kwanza kabisa penda kufanya mazoezi ya kutembea, uwe unatembea kama dakika 30 hivi kwa siku.

-Kunywa lita ya maji ya uvugu vugu kila siku asubuhi baada ya kuamka, maji hayo changanya na kipande cha limao. Kunywa maji kabla ya kula breakfast.

-Kama mnywaji wa pombe acha kunywa pombe. 

-Penda kula matunda na mboga za majani,punguza ulaji wa red meat (nyama kama za cow au mbuzi) penda kula lean meat. Kama mlaji wa kuku usile ngozi yake.

-Vinywaji vya sukari nyingi navyo ni vizuri kuepuka kama soda, kama huwezi unaweza kupunguza ktk unywaji wake.

Kama utafuata vizuri maelekezo hayo, I hope utapunguza uzito wako.

Chakula chako kisiwe na mafuta mengi.

Usinywe maji wakati wa chakula na pia baada ya chakula ila baada ya masaa mawili.

Chakula cha usiku kiwe mapema na kidogo sana.

Green tea pia inasaidia sana weka sukari kidogo sana kama unahitaji. Kunywa green tea mara tatu kwa siku yaani kila baada mlo. Kama unapenda mayai usile ini. Kula samaki, matunda, mboga mboga hizi zote kwa kiwango kidogo sio kingi.

Kula kiwango kidogo cha chakula atleast baada ya kila masaa matatu hii inasaidia sana mwili wako kuunguza calories zaidi.

Unapokaa muda mrefu bila kula kitu chochote mwili unakuwa unapunguza process ya kuunguza calories.

Mlo wako usizidi saizi ya ngumi yako unaweza kutumia kauli hio. Na kama ni kidogo sana ni vizuri kama nilivyosema hapo juu kula kila baada ya masaa mawili au matatu.

No comments:

Post a Comment