NJOMBE

NJOMBE

clock

Monday, July 15, 2013

WAJAWAZITO WATOZWA FAINI DOLA 5 KILA WANAPOPIGA KELELE ZA UCHUNGU HOSPITALINI...

Wodi ya wajawazito hospitalini hapo.
Wanawake masikini wamekuwa wakinyonywa katika wakati wao usio salama na hospitali moja ambayo huwatoza Dola za Marekani 5 kila wanapopiga kelele wakati wa kujifungua.

Uvumbuzi huo wa kushitusha ulifanywa na kundi la Wamarekani linalofanya kampeni dhidi ya rushwa, iliposambaza ripoti yake ya kila mwaka Global Corruption Barometer.
Katika hospitali hiyo nchini Zimbabwe, moja ya nchi masikini kabisa duniani, faini hiyo ilisemekana kutozwa kwa 'kupiga king'ora kimakosa', kwa mujibu wa Transparency International.
Wanawake ambao hawakuwa na uwezo wa kulipa faini hiyo walidaiwa kufungiwa hospitalini hapo hadi familia zao zitakapokuja kulipa. Riba pia huongezwa kwenye faini hizo, kwa mujibu wa ripoti hizo.
Akinamama wengi tayari wamekuwa wanakwepa kujifungulia hospitalini katika taifa hilo la Afrika sababu ya gharama hiyo ya Dola za Marekani 50, ambayo ni takribani theluthi moja ya wastani wa kipato cha Dola za Marekani 150.
Katika nchi ambako karibu asilimia 95 ya idadi ya watu wote hawana ajira baada ya miaka kadhaa ya mtikisiko wa uchumi na rushwa chini ya Rais Robert Mugabe, na mmoja kati ya wanawake wanane hufa wakati wa kujifungua kila siku, faini hizo zinapora mshahara wa mwanamke wa mwaka.
Utafiti wa Wazimbabwe umegundua asilimia 65 inaamini huduma za matibabu nchini humo zimetawaliwa na rushwa.
Pale Transparency International ilipowasiliana na Naibu Waziri Mkuu wa Zimbabwe, aliamuru uchunguzi ufanyike na tangu hapo hakuna ripoti zozote za faini zilizopatikana.
Hatahivyo, gharama ya Dola za Marekani 50 wakati wa kujifungua imeendelea kuwapo.
Kundi hilo la kampeni sasa limeandaa warsha kashaa nchini Zimbabwe kuinua uelewa kuhusu rushwa na kuonesha wananchi jinsi maofisa rekodi wanavyotaka hongo hivyo kuweza kutoa ushahidi mahakamani.
Faini wakati wa kujifungua zilianikwa wakati kundi hilo la kampeni lilipotoa ripoti ikionesha kwamba karibu robo ya watu wote duniani imetoa hongo katika mwaka uliopita.
Ugunduzi huo, uliolenga kwenye utafiti kwa watu 100,000 katika zaidi ya nchi 100, uligundua kwamba polisi na mifumo ya mahakama ilikuwa ikiongoza kwa rushwa, kwa mujibu wa ripoti.
Karibu theluthi ya watu ambao walishiriki kwenye utafiti walisema walitoa hongo kwa polisi.
Nchi ambayo kinara wa rushwa ilikuwa Sierra Leone, ambako asilimia 84 ya watu waliohojiwa waliripoti kutoa hongo.
Nafasi ya mwisho kwa rushwa ilishikwa kwa pamoja na nchi za Australia, Denmark, Finland na Japan.
Katika nchini ya Marekani, asilimia 7 ya wote waliohojiwa walidai kuwahonga polisi, iliripotiwa.

No comments:

Post a Comment