NJOMBE

NJOMBE

clock

Wednesday, July 31, 2013

Jifahamishe kuhusu Utalii katika Nchi yetu Tanzania

UTALII
Sekta ya utalii Tanzania ni miongoni mwa sekta zenye uwezo wa kukua sana kiuchumi. Inaleta fedha nyingi za kigeni na kuajiri watu 30,000, na inahamasisha sekta nyingine kama kilimo na hivyo kukuza uchumi. Mchango wake katika Pato la Taifa ni asilimia 14, ambayo ni sehemu ndogo ikilinganishwa na uwezo wa sekta hii.

Tanzania imebahatika vivutio vingi vya utalii. Tanzania inashinda nchi nyingi kwa kuwa na wanyamapori wengi na wa aina nyingi na mandhari za kuvutia, mazingira yasiyoharibiwa, watu wakarimu na sekta za kiuchumi zenye kuweza kuhimili sekta ya utalii, kama sekta ya madini na nyinginezo.

Vivutio vingi asilia na ukubwa wa nchi unatoa nafasi ya kuendeleza shughuli za utalii kama kutazama wanyama, safari na shughuli za ufukweni, upandaji milima, kuona manthari, uwindaji, na upigaji picha.

Lengo letu ni kuendeleza utalii endelevu na bora ambao unaendana na uhifadhi, utunzaji wa mazingira na utamaduni wetu. Kwa kufanya hivyo Tanzania itakuwa inapata faida halisi kutoka kwenye shughuli mbalimbali za utalii.

Tanzania ni mahali pa pekee katika Afrika, ambapo bado hapajagundulika na wengi. Ni nchi yenye maajabu ya mimea na viumbe visivyopatikana kwingine. Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika wenye theluji; visiwa vya maajabu vya Zanzibar; hifadhi za wanyama za Seregeti; ziwa Tanganyika; ziwa Manyara; kileta ya Ngorongoro; magofu ya karne ya 14 na 16 ya Kilwa Kisiwani; goji la Olduvai; nyayo za Laitoti; hifadhi za Baharini Kisiwa cha Mafia ni machache tu ya sehemu za kuvutia utalii. Mandhari na topografia ya nchi na watu wake wakarimu, wana uwezo mkubwa wa kukuza utalii na utamaduni, likizo za ufukweni, uwindaji, shughuli za akiolojia, na upigaji picha mzuri kulilo wote barani. Kwa habari zaidi ya vivutio vya utalii, tazama www.tanzania-web-com/home2.Htm

Sera ya Utalii

Sera ya Utalii ya Septemba 1999 ina malengo yafuatayo: 

 • Kuongeza uchumi na kuleta hali nzuri kwa wananchi kwa kupunguza umaskini, kwa kuendeleza utalii ulio endelevu na wa hali ya juu kiutamaduni, unaokubalika na watu, unaokubalika kiikolojia, wenye kuzingatia mazingira mazuri na unaolipa kiuchumi. 
 • Kutangaza Tanzania kama kituo muhimu cha utalii na nchi yenye utajiri wa utamaduni na fukwe nyingi. 
 • Kuongeza mchango wa sekta kutoka asilimia 16 hadi 25 na 30 ifikapo mwaka 2010. 
 • Kuweka msingi wa rasilimali ya utalii kwa kiwango cha kutosha kama sehemu ya rasilimali ya umma.
 • Kuboresha miundombinu ya utalii na kuiendeleza zaidi ili kupata pato kubwa kutoka kwenye sekta.
Mkakati wa kutekeleza Sera ni pamoja:
 • ¨ Kuboresha miundombinu kama vile barabara, usafiri wa anga nk.
 • ¨ Kuongeza huduma zaidi kama hoteli na migahawa.
 • ¨ Kuongeza ubora na ufanisi katika kutoa huduma
 • ¨ Kuchukua hatua za kuitangaza bayana tasnia na kuweka mipango ya masoko ya ndani na kimataifa.
 • ¨ Kuboresha maeneo ya utalii kwa kutunza uasilia wa mahali.
 • ¨ Kuimarisha taasisi mbalimbali zinazohusika na utalii na kuongeza uratibu wa huduma mbalimbali za kitalii
 • ¨ Kuchochea uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wa miundombinu na huduma za utalii
 • ¨ Kuendeleza uwezo wa wafanyakazi kulingana na mahitaji ya utalii.
 • ¨ Serikali itahusika katika kuweka miundombinu ya msingi na mazingira yanayofaa kwa washika dau wakati sekta binafsi itaachiwa kuendeleza sekta ya utalii.
Tanzania iko kwenye mazingira ya ushindani katika utoaji wa bidhaa bora na huduma za utalii, dhidi ya idadi ya vituo vingine vya utalii na uchaguzi mkubwa walio nao watalii. Katika hali hii, sera imeweka wazi haja ya kuwa na sheria na taratibu zinazowezesha mazingira ya ushindani.


Washikadau wa Sekta ya Utalii:

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
Bodi ya Utalii Tanzania inakuza maendeleo ya utalii.

Kazi zake

 • ¨ Kutangaza utalii ndani na nje ya nchi
 • ¨ Kufanya kampeni (matangazo, uhusiano wa umma.maonyesho) kwa lengo la kuvutia utalii.
 • ¨ Kutayarisha na kuchapisha vipeperushi na makala za kujitangaza
 • ¨ Kutoa habari za kitalii
 • ¨ Kutafiti na kuweka kumbukumbu za kisasa za utalii.

No comments:

Post a Comment