NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, February 5, 2013

MWENGE ILIVYOTEKETEA KWA MOTO JANA

Baadhi ya wafanyabiashara eneo la Mwenge stendi ya daladala wakijaribu kuokoa mali zao baada ya maduka yao kuungua moto.
MADUKA kadhaa ya vipodozi, nguo yameungua moto na kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wake.
Moto huo umetokea mishale ya saa 5.20 leo asubuhi baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye moja ya kibanda cha biashara.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto huo ulianza taratibu kisha kupamba moto.
Wafanyabiashara wa maduka ya vipodozi ndiyo waliopata hasara kubwa kwa mali zao kuharibika kufuatia kutaka kuziokoa.

Hata hivyo, Kikosi cha Zima moto kilichofika eneo la tukio kwa wakati na kimepongezwa kwa kufanya kazi nzuri na kuweza kuudhibiti moto huo.
Adha, jeshi la polisi limepongezwa kwa kazi nzuri lililoifanya ya kudhibiti vibaka ambao walijiandaa kufanya uhalifu wa kuiba mali katika kurupushani hizo za uokoaji.
Askari wa Kikosi cha Zima moto akizima moto huo uliokuwa ukiunguza maduka ya vipodozi.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya maduka ya vipodozi yakiungua moto.
Wanausalama wakidumisha amani eneo hilo.

BREAKING NEWS: MSANII WA BONGO FLEVA BUI BUI APATA AJALI

No comments:

Post a Comment