NJOMBE

NJOMBE

Monday, June 18, 2012

Ugiriki yapata kiongozi mpya

Kiongozi wa chama cha New Democracy nchini Ugiriki, chenye sera za mrengo wa kulia, Antonis Samaras, ameshinda katika uchaguzi mkuu wa pili ambao umefanyika wiki sita baada ya ule wa kwanza.
Bwana Samaras amesema wananchi wa Ugiriki wameeleza nia yao ya kutaka kubakia katika muungano wa nchi za Ulaya na kuheshimu nia ya nchi hiyo katika kuimarisha uchumi wake.
uchaguzi ugiriki
Wanaopinga mpango wa EU wameshindwa
Naye Kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza, Alexis Tsipras, amesema chama chake hakitajiunga katika serikali ya pamoja.
Bwana Tsipras amesema chama chake bado kinapinga hatua zilizopendekezwa na nchi wanachama wa Euro kuimarisha uchumi wa Ugiriki.
Akiwahutubia wafuasi wake mjini Athens, Bwana Tsipras amesema kukiunga mkono chama cha Syriza kumezionyesha nchi za Ulaya na viongozi wa siasa wa Ugiriki kwamba hawawezi kuweka masharti ya kunusuru uchumi wa nchi hiyo bila kukubaliwa na wananchi.
Viongozi wa nchi za Ulaya walionya kuwa ikiwa raia wa Ugiriki watapinga mpango huo uliopendekezwa wa kufufua uchumi wao, basi nchi hiyo italazimika kuacha kutumia sarafu ya Euro.
Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble amesema matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha nia ya raia wa nchi hiyo kuendelea na mpango wakunusuru uchumi wa nchi yao.
Mawaziri wa fedha kutoka nchi wanachama wa umoja wa ulaya, katika taarifa ya pamoja wameelezea kuwa wawakilishi wa benki kuu ya umoja huo, shirika la fedha duniani (IMF) na tume ya umoja huo watazuru nchi hiyo punde tu serikali mpya itakapoundwa.

Wanafunzi waandamana mjini Khartoum

Polisi wa kupambana na fujo mjini Khartoum, Sudan, wametumia moshi wa kutoza machozi na virungu kuzima maandamano ya wanafunzi wanaopinga kupanda kwa gharama za maisha.
Rais bashir wa Sudan

Mamia ya waandamanaji waliokusanyika katika Chuo Kikuu cha Khartoum, walifukuzwa na polisi.
Piya kuna ripoti kuwa maandamano yamefanywa katika miji mingine kama miwili.
Uchumi wa Sudan umezorota tangu Sudan Kusini yenye utajiri wa mafuta, ilipojitenga na kaskazini mwezi Julai mwaka jana.

Ulipizaji kisasi watokea Nigeria

Mashambulio kadha ya mabomu yamefanywa dhidi ya makanisa katika jimbo la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria.
Shambulio la bomu la karibuni mjini Kaduna
Ripoti zinasema watu zaidi ya 10 wamekufa.
Miripuko miwili ililenga makanisa karibu na mji wa Zaria, wakati ibada zinaendelea.
Katika mji wa Kaduna, mashambulio ya karibuni yamezusha ulipizaji kisasi dhidi ya Waislamu, ambapo waislamu walibururwa kutoka magari yao na kuuwawa.
Wakuu wa Kaduna wameweka amri ya kutotoka nje kwa saa 24, na wanajeshi na polisi wanajaribu kurejesha utulivu.
Hii ni Jumapili ya tatu mfululizo ambapo makanisa yameshambuliwa kwa mabomu katikati mwa Nigeria.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, lilikiri kufanya mashambulio ya siku za nyuma.

Sunday, June 17, 2012

AY NDANI YA BIG BROTHER LEO


Msanii wa music wa kizazi kipya unaojulikana sana hapa Bongo kama bongo flavar Ambwene Allen Yesaya maarufu kama AY.Leo siku ya jumapili atakuwa na shoo kali la kutisha katika jumba la Big Brother evision pale kati ni jamaa atatompwinyo.Msanii huyu hivi juzi ametoka kutambulisha ngoma yake mpya Inayokwenda kwa jina Part Zone.Cheki kwenye ukurasa wako wa Burudani unagumiana nayo.

Bunge la Misri lafutwa


Halmashauri ya kijeshi inayoongoza Misri imethibitisha kuwa bunge la nchi limefutwa.
Bunge la Misri
Afisa mkuu kwenye bunge la Misri, aliiambia BBC kwamba amepokea barua kutoka halmashauri ya kijeshi kumuarifu rasmi kuwa bunge limefutwa.
Siku ya Alkhamisi, Mahakama ya Katiba yaliamua kuwa uchaguzi wa bunge uliofanywa mwaka jana ulikwenda kinyume na katiba.
Tangazo hilo limetolewa wakati Wamisri wanapiga kura kumchagua rais mpya atayechukua nafasi ya Hosni Mubarak, ambaye alitolewa madarakani mwaka uliopiota.
Upigaji kura huo wa siku mbili ni wa kuchagua rais kati ya waziri mkuu wa zamani wa Mubarak, Ahmed Shafiq, na Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema inaonesha watu waliojitokeza kupiga kura ni kidogo ikilinganishwa na duru ya kwanza, na vijana wengi wanaonesha wamevunjika moyo na wagombea hao wawili, na hawataki kupiga kura.

Wachunguzi wa UN wasimamisha kazi Syria

Mkuu wa ujumbe wa wachunguzi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Jenerali Robert Mood, ametangaza kuwa wanasimamisha kazi yao kwa sababu ghasia zinazidi.
Kofi Annan akimpa mkono Jenerali Mood

Meja Jenerali Robert Mood alisema wachunguzi hawatapiga doria, na watabaki kwenye vituo vyao hadi kutolewe tangazo jengine.
Hapo Ijumaa Jenerali Mood alisema pande zote mbili katika mzozo zinalenga mafanikio ya kijeshi, na hakuna hamu ya kutafuta kipindi cha mpito cha amani.
Alizisihi pande zote kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa, ambao alisema bado unaweza kusaidia kuleta suluhu ya amani.

Saturday, June 16, 2012

Mti wa Moringa afueni ya chakula Niger

Mwendesha mashtaka mkuu mpya wa ICC

Fatou Bensouda
Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya kukabiliana na Uhalifu wa Kivita ameapishwa mjini Hague hii leo.
Bi Fatou Bensouda, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Haki nchini Gambia,ndiye Mwafrika na pia mwanamke wa kwanza kushikilia cheo hicho.
Mojawapo wa wajibu wake wa mwanzo ni kumleta Hague mwana wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muamar Gaddafi, Saif al-Islam Gadaffi, ambaye ameshtakiwa kwa makosa dhidi ya binadamu na wakati huohuo kuongoza mashtaka yanayomkabili aliyekuwa kiongozi wa Ivory Coast, Laurant Gbagbo.
Fatou Bensouda amechukua nafasi ya mtangulizi wake aliyeondoka, Luis Moreno Ocampo, ambaye ameongoza mahakama hiyo kwa zaidi ya mwongo mmoja.
Kesi ya rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor, ilisikizwa na mahakama mahakama ya Umoja wa mataifa inayosikiliza kesi za waliohusika na vita vya wenyewe kwa wenyewe
Sierra Leone.
Bi Bensouda amekuwa akihudumu kama naibu wa Luis Moreno-Ocampo anayemaliza kazi yake katika mahakama ya ICC.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa licha ya kwamba Bi Bensouda sio mgeni kwa mambo ya Hague, uteuzi wake unakuja wakati mfumo wa sheria ya kimataifa unahojiwa sana.
Pia anachukua jukumu hilo wakati kuna mtafaruku katika mahakama hiyo huku maafisa wanne wa mahakama hiyo wakiwa wanazuiliwa nchini Libya.
Thomas Lubanga

Mwandishi wa BBC anasema kuwa Bi Bensouda anasifika kwa kuwa mtulivu kitu ambacho huenda kimemsaidia katika kazi yake.
Ikizingatiwa kuwa washukiwa wengi ambao sezi zao ziko katika mahakama ya ICC ni waafrika na hili limekosolewa huku ofisi ya mwendesha mkuu wa mashtaka ikisemekana kuwalenga zaidi waafrika.
Inatarajiwa kuwa kwa sababu Bi Bensouda mwenyewe ni Mwafrika tena wakili, huenda akasaidiwa na hili kunyamazisha wakosoaji wake, kulinagana na wadadisi.
Mwezi Machi mbabe wa kivita kutoka DRC, Thomas Lubanga alipokea hukumu ya kwanza ya kesi yake ikiwa hukumu ya kwanza kuwahi kutolewa na mahakama hiyo tangu kuundwa kwake miaka kumi iliuopita.
Kikosi cha viongozi wa mashtaka wanataka Lubanga apokee miaka 30 jela kwa makosa ya kutumia watoto kama wanajeshi wakati wa vita mashariki mwa nchi yo kati ya mwaka 2002 na 2003.

Uonevu katika idara ya uhamiaji Uingereza


Afisaa wa uhamiaji Uingereza
Maafisa wa idara ya uhamiaji ya Uingereza, wanaotayarisha visa za watu kutoka barani Afrika, huwa na uonevu na huwanyima raia wa kiafrika wanaotafuta visa kuingia nchini Uingereza.
Madai haya yako kwenye ripoti iliyotolewa na shirika moja binafsi kuhusu utaratibu wa idara ya uhamiaji ya Uingereza.
Inspekta mkuu wa idara ya uhamiaji ya Uingereza Bwana John VINE amesema kuwa idadi kubwa ya waombaji wa Visa za uingereza hukataliwa kimakosa.
Idara hiyo imesema imechukulia ripoti hiyo kwa uzitio na inatazamia kubadilisha utaratibu wake.
Amsema sababu kubwa sio makosa yanayotokana na waombaji wenyewe bali nikutokana na maafisa wanaoshughulika na maombi hayo.
Bwana John Vine anasema mara nyingi maombi hukataliwa kwa kukosekana stakabadhi ambazo hapo awali muombaji hakuambiwa zinatakikana.
Afisa huyoa nasema hali hii imeaharibu sifa za uingereza na kuwafanya baadhi ya watu waaamini kwamba kuna ubaguzi fyulani unaofanywa.
Japo uchunguzi huo ulifanywa katika nchi za Kenya, Afrika kusini na Nigeria lakini ripoti hiyo inasema uonevu huo katika utoaji wa Visa umesambaa katika nchi nyingi barani afrika.
Katika ripoti yake Inspekta huyo mkuu huyo wa idara ya uhamiaji amesema kwamba imegyundulika kuwa kuna watu kadhaa hasa kutoka Nigeria waliopewa visa ya Uingereza ya kudumu .
Kutokana na ulegevu huo sasa kumependekezwa kuwa maafisa wote katika idara hiyo ya uhamiaji ya uingereza nimuhimu wapewe mafunzo upya.

Friday, June 15, 2012

Uamuzi wa mahakama Misri wazua wasiwasi


Mahakama kuu ya katiba nchini Misri imesababisha hali ya wasiwasi nchini humo baada ya kutangaza kuwa uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwaka jana ulikuwa kinyume cha katiba na kutaka ufanyike upya.
Maandamano Misri

Uamuzi huo wa mahakama uliotolewa siku mbili kabla ya kufanyika duru ya pili ya kinyang'anyiro cha urais, unalipa baraza la utawala wa kijeshi nguvu za bunge.
Wanaharakati na wanasiasa wamelishutumu jeshi kwa kufanya mapinduzi.
Kulingana na wachambuzi wa masuala ya kisiasa, uamuzi huo una athari kubwa hasa kwa kuwa umetolewa kabla ya kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi mwishoni mwa juma, na inamaanisha sasa kwamba mamlaka ya bunge nchini humo yamo chini ya baraza kuu la Kijeshi ambalo lilipewa jukumu la kuongoza Misri katika kipindi cha mpito baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak kung'olewa madarakani.
Pia kwa msingi wa uamuzi huo, Misri haina katiba kwa sasa na haina bunge.
Chama cha Muslim Brotherhood tayari kimeelezea hofu yake kuwa hatua chache ambazo nchi hiyo ilikuwa imepiga kidemokrasia zinazidi kutoweka.
Chama hicho kimeonya kuwa huenda kukazuka vurumai nchini humo hasa iwapo madaraka ya nchi hiyo yatakabidhiwa kwa watu walio na uhusiano na serikali iliopita ya Hosni Mubarak.
Mgombea wa rais kwa tiketi ya chama cha Muslim Brotherhood, Mohammed Mursi, anakabiliana na aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kwenye duru ya pili ya uchaguzi inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma na ameelezea kwamba hajaridhishwa na uamuzi huo, akisema,"tutaendelea na safari yetu na tutakuwa waangalifu sana kuhakikisha kwamba hakuna udanganyifu wakati wa shughuli ya upigaji kura. Na iwapo kutakuwepo na udanganyifu, kutakuwa na mapinduzi makubwa dhidi ya wahuni....mapinduzi makubwa dhidi ya wale wanaotetea wahuni...mapinduzi makubwa hadi tutakapopata malengo yetu.''
Hofu kubwa kisiasa kuhusiana na uchaguzi wa mwishoni mwa wiki ni kwamba uamuzi huo wa mahakama utamwacha rais atakayechukua madaraka bila bunge na bila katiba.

Raia wa Iran wahukumiwa kunyongwa Saudia

Iran imefutuilia mbalia ziara ya afisaa wake mmoja mkuu wa wizara ya mambo aliyetarajiwa kusafiri nchini Saudi Arabia.
Hii inafuatia mzozo kati ya nchi hizo mbili kuhusu kunyongwa kwa raia wawili wa Iran waliokamatwa nchini humo kwa makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Shirika la habari la Mehr nchini Iran limesema kuwa afisaa huyo alitarajiwa kumwalika waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Saud al-Faisal, kwa mkutano maalum nchini Iran.
Tehran imewasilisha malalamiko kuhusu hukumu hiyo ya kunyongwa kwa raia hao.
Inasema kuwa walizuiliwa kwa miaka mitano na kutoruhisiwa kuwasiliana na maafisa wa ubalozi pamoja na mawakili au hata wakalimani.

Thursday, June 14, 2012

Tanzania yamkamata Erdogan


Mtu mmoja anayeshukiwa kuwa ana uhusiano na shambulio la mwezi uliopita katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi amekamatwa nchini Tanzania.
Athari za mlipuko Nairobi
Athari za mlipuko Nairobi
Polisi ya Kenya inasema kuwa Emrah Erdogan ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki.
Kenya inadai kuwa alivuka mpaka mapema mwezi Mayi kutoka Somalia ambako alishiriki mapigano kwa niaba ya kundi la Al Shabab.
Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika mlipuko ambao wakuu wa Kenya wanasema ulisababishwa na bomu hilo.
Kumekuepo na sintofahamu juu ya chanzo cha mlipuko huo- ambapo Maofisa wa Polisi walianza kwa kusema kuwa mlipuko huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.
Mara kwa mara kundi la Al Shabab limetishia kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi nchini Kenya kwa sababu nchi hio ilituma vikosi nchini Somalia.
Serikali ya Kenya inalituhumu kundi la wapiganaji wa Al Shabab kuhusiana na utekaji nyara wa watu kadhaa kwenye ardhi yake pamoja na kusababisha hali ya wasiwasi kwenye mpaka baina yake na Somalia.
Polisi ya Tanzania imethibitisha kwa BBC kuwa Bw.Erdogan alikamatwa na kuahidi maelezo zaidi baadaya mda mfupi.
Erdogan ni miongoni mwa watu wanne ambao Polisi ya Kenya imekua ikiwasaka tangu kutokea kwa mlipuko huo.
Ilisambaza picha yake na kuomba habari kuhusu mahali alipo.
Bw.Erdogan, anayejulikana pia kama Salahuddin al-Kurdi, inaaminika kuwa aliwahi kusafiri kwenda Waziristan huko Pakistan ya kaskazini magharibi mwaka 2010 ambako alijiunga na kundi la wakereketwa wenye imani kali kabla ya kuelekea Somalia mwaka jana, kwa mujibu wa shirika la habari Reuters.
Mapema mwaka huu, vikosi vya AU vinavyounga mkono serikali ya mseto nchini Somalia viliongezea idadi ya askari wake kutoka 12,000 hadi 18,000 kujumuisha vikosi vya Kenya vilivyoingia nchi hio mnamo mwezi Oktoba mwaka jana kuwasaka wapiganaji wa Al Shabab.
Kundi la Al-Shabab, lililojiunga na mtandao wa al-Qaeda mapema mwaka huu imefahamika lilisajili wapiganaji wa kigeni kadhaa -wengi ambao wamewahi kupigana huko Iraq na Afghanistan.

Ahmed Shafiq kuendelea kugombea urais

Ahmed Shafiq

Mahakama ya katiba nchini Misri imesema aliyekuwa Waziri Mkuu wakati wa utawala wa rais wa zamani Hosin Mubarak, Ahmed Shafiq anaweza kushiriki katika marudio ya uchaguzi wa urais mwishoni mwa wiki.
Katika hukumu hiyo mahakama pia imetengua ushindi wa theluthi moja ya wabunge katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Mwezi Aprili mwaka huu Misri ilipitisha sheria ambayo inapiga marufuku wanasiasa wa serikali wa zamani kugombea uongozi.
Hata hivyo katika hukumu yake mahakama imesema sheria hiyo ilikuwa kinyume cha katiba.
Pamoja na ulinzi kuimarishwa mahakamani, waandamanaji walikusanyika nje ya wakiwa na mabango huku wakipiga kelele.
Kushiriki kwa bwana Shafiq katika uchaguzi huo kulikuwa hakujulikani kutokana na uhusiano wake na utawala wa rais aliyetimuliwa madarakani Hosni Mubarak.
Mahakama hiyo kadhalika imetoa uamuzi kwamba uchaguzi wa thuluthi moja ya wabunge ulikiuka katiba.
Bwana Shafiq ametoa jibu lake kwa hatua hiyo kwa kupongeza mahakama kwa uamuzi wake.

Thursday, May 31, 2012

Kuvuja kwa nyaraka za siri za papa

Papa Benedict
Papa Benedict
Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican, amesema kuvuja kwa nyaraka za siri za kiongozi wa kanisa hilo duniani ni kitendo cha kikatili dhidi ya Papa Benedict.
Afisa huyo ambaye ni naibu waziri wa mambo ya nje wa Vatican Angelo Becciu, amesema nyaraka hizo ni pamoja na fikra binafsi, na pia shutuma kali kutoka kwa watu waliomwandikia Papa barua za siri kutokana na nafasi yake ya kipekee.
Nyaraka hizo zinashutumu vitendo vya rushwa na kushindania madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki.
Mwandishi wa BBC mjini Vatican amesema hii ni kashfa kubwa kuliko zote dhidi ya Papa Benedict tangu apate wadhifa wake huo miaka saba iliyopita, na ni tukio lililochafua Kanisa Katoliki nyakati hizi.
Mhudumu mkuu wa Papa, Paolo Gabriele, amekamatwa na tume ya Vatican inachunguza watu wengine ambao wamehusika katika kashfa hiyo.

HIVI NDIVYO ILEVYOPELEKEA TAYLOR KUTUPWA JELA

Kesi dhidi ya Charles Taylor

Charles Taylor
Charles Taylor
Waendesha mashtaka katika kesi ya rais wa zamani wa Liberia Charles Charles Taylor, wameomba adhabu ya kifungo cha miaka 8 jela itolewe dhidi yake.
Bw Taylor alipatikana na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa mjini The Hague, wiki iliyopita.
Katika pendekezo lao lililowasilishwa mbele ya mahakama hiyo maalum inayosikiza kesi ya Seirra Leone, waedesha mashtaka walisema hukumu hiyo inamfaa kutokana na uzito wa uhalifu wa kivita alioufanya bwana Taylor.

makosa

Mahakama hiyo inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa ilimpata bwana Taylor na hatia ya kuuga mkono makundi ya waasi waliofanya mauaji ya kikatili, ubakaji, na kukata viungo vya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi na moja nchini Sierra Leone.
Kiongozi huyo wa zamani wa Liberia anatarajiwa kuhukumiwa Mei 30.
Mahakama hiyo haitoi hukumu ya kifo.