Waziri wa kawi nchini Nigeria, Barth Nnaji amejiuzulu baada ya kuhusishwa na kashfa ya kandarasi ya uzalishaji umeme.
Serikali ya Nigeria iko katika harakati za
kubinafsisha makampuni yake katika juhudi za kumaliza tatizo kubwa la
upungufu wa umeme.Msemaji wa bwana Nnaji alisema kuwa waziri huyo amelimbikiziwa makosa hayo visivyo.
Ni nadra kwa wanasiasa nchini Nigeria ambako ufisadi ni tatizo kubwa kujiuzulu baada ya kuhusishwa na kashfa yoyote kwa mujibu wa wadadisi wa siasa za nchi hiyo.
Rais Goodluck Jonathan,aliyeahidi kupambana na tatizo la upungufu wa umeme alipoingia madarakani mwaka 2010, alisema kuwa anakubali kujiuzulu kwa bwana Nnaji.
'Maslahi ya kibinafsi'
Msemaji wa Nnaji alithibitisha kuwa alikuwa na maslahi katika mojawapo ya makampuni yaliyotoa maombi yao ya kununua mali hizo.
Aliongeza kuwa bwana Nnaji hakufurahia hata kidogo kuhusu tuhuma hizo na kwamba alionelea ni bora kwake kuendelea na shughuli zake za binafsi.
Mwandisi wa BBC Fidelis Mbah anasema kuwa tangu kuingia ofisini mwezi Julai mwaka 2011,bwana Nnaji amekabiliwa na changamoto kubwa kwa sababu ya mageuzi anayojaribu kuleta.
Amekuwa akijaribu kukabiliana na ufisadi na utenda kazi duni wa sekta ya kawi , hatua ambayo imeghadhabisha wafanyakazi wa umma ambao huenda wakapoteza kazi zao.
Nigeria ndio nchi inayozalisha pakubwa mafuta pamoja na kuwa na visima vingi vya gesi.
No comments:
Post a Comment