Shirika la kimataifa la kutetea
haki za kibinaadamu, Amnesty International, linasema limeambiwa kwamba
Gambia imewanyonga wafungwa tisa kati ya 47 ambao wamehukumiwa kifo.
"Tumepata taarifa za kuaminika kuwa watu 9 walinyongwa jana usiku.
Nimezungumza na baadhi ya jamaa zao, ambao bila ya shaka wako kwenye majonzi, na wametuomba tuchukue hatua.
Wamegusia kuwa kuna wengine watanyongwa leo usiku.
Tunajaribu kuzitawanya habari hizi ulimwenguni na serikali ya Gambia inafaa kujua kuwa macho ya ulimwengu na serikali za nchi za nje yameelekezwa juu ya nchi hiyo."
Hapo awali, shirika la raia la nchi hiyo lilimlaumu rais wa Gambia, Yahya Jammeh, na lilisema kwamba wengi waliohukumiwa kifo ni wafungwa wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment