Waziri wa dini wa Sudan Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim ni miongoni mwa watu 31 waliouwawa katika jali ya ndege.
Shirika la habari la Sudan limesema kuwa
mawaziri wengine wawili na pia viongozi wa chama kinachotawala la Omar
el-Bashir pia waliuwawa.Ndege hiyo ilikuwa ikielekea eneo la South Kordofan kwa sherehe za Eid al-Fitr ili kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mbali na waziri huyo wa maswala ya kidini Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim wegine waliofariki katika jali hiyo ni Justice mwenyekiti wa chama Makki Ali Balayil, Waziri wa vijana na michezo na Issa Daifallah, waziri wa utalii na wanyma pori.
Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Talodi huko South Kordofan, ikiwa imetoka mji mkuu Khartoum
Mji huo wa Talodi, uko kilomita 50 kutoka mpaka wa Sudan Kusini.
Taarifa za runinga ya taifa zinasema kuwa hali mbaya ya anga iliizuia ndege hiyo kutoa na ilipojaribu mara ya pili iligonga mlima.
Afisa mmoja wa shughuli za ndege alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ya iana ya Antonov.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ajali kadhaa mbaya za ndege. Na maafisa wa Sudan wamekuwa wakilalamika kuwa imekuwa vigumu wao kupata vipuri kwa sababu ya vikwazo vya Marekani.
No comments:
Post a Comment