Rais Obama ameongoza katika
sifa na rambi-rambi zilizotolewa baada ya kifo cha Neil Armstrong, mwana
anga wa kwanza kutua kwenye mwezi, ambaye amefariki akiwa na umri wa
miaka 82 kutokana na matatizo aliyopata baada ya upasuaji aliofanyiwa
kwenye moyo.
Rais Obama alimuelezea Neil
Armstrong kwamba ni mmoja kati ya mashujaa wakubwa wa Marekani, siyo
wakati wake tu, lakini katika historia ya nchi hiyo piya.
Mwenzake Armstrong katika safari ya kihistoria
ya kwenda mwezini mwaka wa 1969 alikuwa Buzz Aldrin, ambaye alisema
Armstrong alikuwa rubani na kamanda mahiri.
Familia ya Neil Armstrong imetoa wito kwa
Wamarekani kuonesha heshima zao kwa kufuata mfano wake wa kutumika,
kufanikiwa na bila ya majivuno.
Taarifa ya familia iliwaambia wale washabiki wake: "ukitembea nje usiku ukaona mwezi unakuchekea, mfikirie Neil na umkonyeze."
No comments:
Post a Comment