Mkuu wa ujumbe wa wachunguzi wa
Umoja wa Mataifa nchini Syria, Jenerali Robert Mood, ametangaza kuwa
wanasimamisha kazi yao kwa sababu ghasia zinazidi.
Hapo Ijumaa Jenerali Mood alisema pande zote mbili katika mzozo zinalenga mafanikio ya kijeshi, na hakuna hamu ya kutafuta kipindi cha mpito cha amani.
Alizisihi pande zote kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa, ambao alisema bado unaweza kusaidia kuleta suluhu ya amani.
No comments:
Post a Comment