Maafisa wa Nigeria wametangaza
sheria ya kutotoka nje katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Damaturu
kufuatia makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa kisiilamu na
pia sheria hiyo imerejeshwa tena katika jimbo la Kaduna.
Makabiliano kati ya jeshi na wapiganaji wa
kiisilamu eneo la Damaturu yalianza Jumatatu, siku moja baada ya kutokea
mashambulio ya mabomu yaliyolenga makanisa jimbo la Kaduna na kudaiwa
kutekelezwa na kundi la Boko Haram.Polisi wa Nigeria wamelaumu Boko Haram kwa kulenga vituo vyao na jeshi ambapo maafisa watano waliuawa eneo la Damaturu hapo Jumatatu.
Rubaa za karibuni zinasema milio ya risasi imepungua katika jimbo la Yobe. Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa polisi jimbo hilo Patrick Egbuniwe.
Damaturu,ni makao makuu ya jimbo la Yobe ambalo , Magharibi mwa jimbo la Maiduguri na ngome kuu ya Boko Haram.
Jina la Boko Haram linamaanisha kwamba elimu ya kisasa ni haramu. Kundi hilo linashinikiza sheria ya kiislamu {Sharia} kutangazwa kote nchini Nigeria na limetekeleza mashambulio makali nchini humo.
No comments:
Post a Comment