Kitu kipya kinajitokeza katika
upembe mmoja ambao ni kame magharibi mwa Niger. Mmea wa ajabu wa
Moringa ndio umeanza kuwa kama silaha ya kupigana na njaa ambayo
hujitokeza katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika mara kwa mara
kina mama katika kijiji kimoja nchini Niger,
wameungana kuanzisha mradi wa upanzi wa mti wa Moringa ambao kuweza
kuutumia kama chakula.
Akina mama hawa hulima, kuupanda na kupalilia mti huo ambao huwa tayari kutumika kama chakula katika miezi miwili tu.
Wengi hawakujua kama mti huu ungewza kutumika
kwa namna hiyo kama mboga na sasa akina mama hao wanataka kuhakikisha
kuwa wanakabiliana vilivyo na uhaba wa chakula.
No comments:
Post a Comment