Melfu ya waandamanaji wamefurika
katika medani ya Tahrir mjini Cairo, Misri kulaani watawala wa kijeshi
kwa kujiongezea madaraka makubwa. Wiki iliyopita watawala wa kijeshi
walifuta bunge na kujilimbikizia mamlaka ya kutunga sheria.
Raia wa Misri wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa
Urais ambao mgombea wa mrengo wa Muslim Brotherhood Mohammed Mursi
anataka yatolewe mara moja.Baraza hilo halijataja lolote kuhusu mgombea wa chama cha Freedom and Justice ambacho hapo Jumanne kilisema bw Mursi alikua ameshinda uchaguzi kwa asili mia 51.7.
Mpinzani wake Ahmed Shafiq ambaye aliwahi kua Waziri Mkuu ametangaza pia kushinda.Makundi yanayotetea sera isiyofuata dini na wanaharakati wa kiisilamu wameitikia maandamano yaliyoitishwa na Muslim Brotherhood baada ya sala ya Ijumaa.
Viongozi wa kidini walioongoza maombi katika medani ya Tahrir walisema Mohammed Mursi ndiye mshindi katika raundi ya pili ya uchaguzi wa pili.Akihutubia waandishi wa habari Mursi alisema atakubali matokeo ikiwa shughuli nzima itafanyika kwa njia ya uwazi.
Aliongeza endapo atatangazwa Rais atahakikisha Misri inapata Waziri Mkuu anayeungwa na pande zote.
Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema mzozo wa sasa unavunja matumaini ya kuyakabidhi madaraka kwa raia nchini Misri na hivyo kuyumbisha mchakato wa demokrasia.
No comments:
Post a Comment