NJOMBE

NJOMBE

Thursday, June 14, 2012

Ahmed Shafiq kuendelea kugombea urais

Ahmed Shafiq

Mahakama ya katiba nchini Misri imesema aliyekuwa Waziri Mkuu wakati wa utawala wa rais wa zamani Hosin Mubarak, Ahmed Shafiq anaweza kushiriki katika marudio ya uchaguzi wa urais mwishoni mwa wiki.
Katika hukumu hiyo mahakama pia imetengua ushindi wa theluthi moja ya wabunge katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Mwezi Aprili mwaka huu Misri ilipitisha sheria ambayo inapiga marufuku wanasiasa wa serikali wa zamani kugombea uongozi.
Hata hivyo katika hukumu yake mahakama imesema sheria hiyo ilikuwa kinyume cha katiba.
Pamoja na ulinzi kuimarishwa mahakamani, waandamanaji walikusanyika nje ya wakiwa na mabango huku wakipiga kelele.
Kushiriki kwa bwana Shafiq katika uchaguzi huo kulikuwa hakujulikani kutokana na uhusiano wake na utawala wa rais aliyetimuliwa madarakani Hosni Mubarak.
Mahakama hiyo kadhalika imetoa uamuzi kwamba uchaguzi wa thuluthi moja ya wabunge ulikiuka katiba.
Bwana Shafiq ametoa jibu lake kwa hatua hiyo kwa kupongeza mahakama kwa uamuzi wake.

No comments:

Post a Comment