Kapumzike kwa amani Wille wa Ogunde
Salaamu wasomaji, Moyo naupiga konde,
Sihitaji hata maji, kama viazi mviponde,
Nimejawa na simanzi, Kifo cha kaka Ogunde,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Tusimlaumu Mungu, sote tulio waungwana,
Najua tuna uchungu, yowe ni kwamaulana,
Mola angetupa fungu, kifo siwe cha kijana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Twasema kasitukizwa, Wille kaenda kijana,
Alipo kuja hatukuulizwa, tulimwona tu mvulana,
Mungu we ndo muweza, kifo leo twakimbizana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Mwaka ule 74 machi saba, Wille ukaiona dunia,
Leo amegonga siku ya saba, ukamtwaa hii dunia,
Tena tarehe kumi na saba, Wille kaiga dunia,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Wille ulilia kaka, siku uliyo iona dunia,
Pinto, Mroki na Kisaka, sasa zamuyetu kulia,
Wengi wanatafuta kichaka, lini nao watatwaliwa,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Pigo la wana habari, Tanzania na Afrika pia
Hakika kifo ni bahari, hakuna ajuae ilikoanzia,
Kifo ni jemedari, Wille amesha twalia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Salamu kawape jalia, wote walo kutangulia,
Mwakiteleko alotulia, na wote wana familia,
Wanahabari tunalia, Wille Ogunde kutangulia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Father Kidevu tamatia, nangoja nami kufuatia,
Siku itapo fikia, hakuna atakae bakia,
Kifo kitendawili, Mola ndie atakae kitegua,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
No comments:
Post a Comment