KAMATI ya Siasa ya Wilaya ya Simanjiro kesho inatarajia kukutana na
kumjadili aliyekuwa Katibu wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro, Alhaj Omar
Kariaki anayedaiwa kutokomea na fedha zilizochangwa kwenye harambee
maalumu ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya vijana wilayani humo.
Hayo
yalisemwa jana na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro, Kiria Laizer
ikiwa ni siku moja baada ya Kariaki kuibuka na kukiri kutokabidhi fedha
hizo.
Laizer alithibitisha jana kufanyika kwa kikao hicho
alichosema pia kitahudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo, Khalid Mandya
ambaye amevalia njuga upatikanaji wa fedha hizo zilizopatikana kwenye
harambee iliyoongozwa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Shamsi Vuai Nahodha.
Nahodha ambaye
sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Muungano, binafsi
alichangia Sh2 milioni katika harambee hiyo iliyofanyika katika ukumbi
wa hoteli ya kitalii ya Manyara Inn ulioko mji mdogo wa Mererani
wilayani Simanjiro.
“Kwanza nachukua fursa hii kukupongeza wewe
binafsi na gazeti lako la Mwananchi kwa jinsi mlivyofuatilia kwa karibu
suala hili hadi mtuhumiwa ambaye tumemtafuta kwa kipindi kirefu
kujitokeza hadharani na kukiri kuondoka na fedha zetu. Jumamosi
tunakutana kwenye kamati ya siasa wilaya kujadili hili,” alisema Laizer.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka Simanjiro jana asubuhi, Mwenyekiti huyo wa
vijana alisema kila siku anamwomba Mungu suala hilo lipate ufumbuzi
kwani licha ya kuwapa picha mbaya mbele ya waliojitolea kuchanga fedha
zao kuinua hali ya maisha ya vijana kwa kuanzisha mradi wa mahari ya
kusafirisha abiria, yeye binafsi amekuwa akihusishwa na upotevu wa fedha
hizo.
Habari zaidi katika Mwananchi.
Kwa habari za burudani na michezo makaliery-t ndio blog yako nitumie na kutoa taarifa kwa email makalimachechi@yahoo.com ipate tangazwa hata biashara pia
Friday, February 17, 2012
Thursday, February 16, 2012
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr. Mohammed Gharib Bilal atembelea mradi mkubwa wa Uranium Tanzania
Makamu wa Rais Mh.Dr.Mohammedi Gharib Bilal na Assa Mwaipopo Country manager alipowasili katika eneo la Kambi ya Mradi wa Mto Mkuju.
Makamu wa Rais Dr.Mohammed Gharib Bilal jana alitembea mkoa wa
Ruvuma nakisha kutembelea mradi wa utafiti wa Uraniam mkoani hapo.Mradi huo wa
utafiti wa madini ya Uranium unaojulika kama mradi mto Mkuju uliopondani ya
Mkoa wa Ruvuma,Wilayani Namtumbo katika hifadhi ya wanyama ya Selou.Mradi huo
ni mradi unaomilikiwa na Kampuni ya Mantra Tanzania Limited wanomilikiwa na
Uranium One waliochini ya ARMZ.Uranium One ni Kampuni kutoka nchini Canada na
ni kampuni inayojishughulisha sana na madini hayo humu ulimwenguni.ARMZ ni
kampuni ya kirusi ndio inayoisimamia Uranium One na kufanya Uranium One na
Mantra Tanzania Limited kuwa chini yao.
Makamu wa Rais Mh.Bilal aliweza kutembelea mradi huo
kufahamishwa shughuli zinazoendelea mahali hapo.Mh Makamu wa Rais pia alionyeshwa
baadhi ya mambo na shughuli zinazofanyika katika mradi huo wa mkuju river project eneo la
Nyota,Pia Mh.Bilal alielezwa kwamba utafiti huo sio kama ndio unaendelea mahali
hapo tu bali bado kuna maeneo mengine ambayo Mantra Tanzania Limited imefanya
utafiti na inaendelea kufanya maeneo mengine kama bonde la
Mbarang’andu,Mbambabei pamoja na Bahi.
Baada ya hayo yote Makamu wa Rais Mh.Gharib Bilal alipata fursa
yakuongea jambo juu ya mradi huo.Mh makamu wa Rais alisema amefurahishwa sana
na mradi huo wa utafiti wa madini ya Uranium Tanzania yaliopeleka mradi huo
kufika kiwango cha kufunguliwa mgodi wa madini hayo.Alisema mradi huo utakapofunguliwa na kuwa mgodi utaiweka Tanzania katika hali ya juu ya kimataifa katika uzalishaji wa madini ya Uranium,pia alizungumizia hali na
mazingira ya mahali hapo kuwa nieneo zuri kwakuwa utafiti umeonyesha madini
hayo hayapo mbali na sura ya dunia hivyo kufanya uchimbaji kuwa rahisi na wa
gharama ndogo,Licha ya gharama za uendeshaji wa mgodi bali hata namna ya kutuza
na kuweka mabaki ya udongo uliotokana na uchimbaji pia kuwarahisi na kusaidia
utunzaji wa mazingira kwa kiasi kikubwa na kutokusababisha madhara kwa watu
watakokuwepo eneo hilo.
Mh. Makamu wa Rais awapongeza pia Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC) kwa kazi nzuri
wanayoifanya kushirikiana vizuri na Mantra Tanzania Limited katika swala zima
la mionzi itokanayo na madini hayo ili kuweka hali ya usalama kwa wafanyakazi
wa eneo hilo la mradi.TAEC ni taasisi ya Tanzania inayojishughulisha na
mionzi,.Pia Mh. Bilal alifuraishwa
sana na Kampuni ya Uranium One na ARMZ
kuisimamia kampuni ya Mantra katika mradi huo hadi hapo utakapo kuwa
mgodi na kuwakaribisha katika nchi ya Tanzania wawekezaji hao kutoka Canada na
Urusi na kusema mradi huo utaonyesha njia na maendeleo katika nchi ya Tanzania
na mkoa wa Ruvuma na hata wilaya ya Namtumbo kwa kutoa ajira na zisizo pungua
4000 katika Tanzania.Alisema hayo kufuatia utafiti ulioonyesha kuwa madini ya
Uranium katika eneo hilo ni ratili 119.4 million katika hizo 93.3 million ndio
measured na indicated zipo tayari kwa uchimbaji.Pia alizungumzia kiasi cha fedha ambayo nchi itazipata kwa maisha ya mgodi kutokana na mrahaba na kodi za wafanyakazi na mengineyo ni $ 630
million dollar,Mgodi unatarajiwa kuwa na maisha yapatayo miaka 12 pindi tu utakapo anzishwa.Mpaka
sasa kinachosubiriwa ni kibali tu ili kufungua mgodi.Mh.Makamu wa Rais alisema
serikali imefurahishwa sana na mradi huo hata kuwa mgodi.
Habari na Makali Machechi,Mkuju, Picha na Nurah Kalegea,Said Mateso na Makali machechi.
Habari na Makali Machechi,Mkuju, Picha na Nurah Kalegea,Said Mateso na Makali machechi.
Makamu wa Rais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Gharib Bilal akisalimiana na Chief Oparating Officer wa Uranium One Bw.Steve Magnuson.
Mh.Bilal akisalimiana na Administrator wa kambi ya Mkuju River Project Bw.Peter Kaluwa
Makamu wa Rais akisalimiana na Manager Mausihano Bw.Benard Mihayo
Makamu wa Rais akisalimiana na Senior Technician Bw.Collins Salakana
Manager Utafiti Bw.Emmanuel Nyamusika kaielezea juu ya geology ya mradi wa mto Mkuju.
Manager Mazingira Bw.John Ntukula akielezea juu ya mazingira katika eneo la mradi namna yanavyopewa kipaumbele na kutunzwa.
Afisa Usalama Bw.Nassoro Said akielezea juu ya usalama wa wafanyakazi na viumbe vinavyozunguka mradi huo.
Makamu wa Rais pamoja wengine wakielekea sehemu za maonyesho juu ya shughuli zinazoendelea katika mradi.
Afisa mazingira pia Bw.Said Mateso akielezea namna na jinsi wanavyovitumia vifaa katika kufanya kazi likiwa ni swali kutoka kwa Mh.Makamu wa Rais Dr.Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais Mh.Ali Bilal katika picha ya pamoja na uongozi katika mradi wa mto Mkuju kabla ya kuondoka.
Masafara wa Makamu wa Rais Mh.Ali Bilal ukiondoka katika kambi ya Mradi wa Mto Mkuju(Mkuju River Project).
Mawaziri watano hoi
Waandishi wetu
WAKATI tetesi za kupanguliwa Baraza la Mawaziri zikizidi kupamba moto, hali ya afya ya baadhi ya mawaziri imeelezwa kuwa tete hivyo kulazimika kupelekwa India kwa matibabu.Miongoni mwa Mawaziri hao ni wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami ambaye jana aliibuka na kuwataka watu aliowaita wanye uchu wa kuchukua nafasi yake, waache mara moja kutumia afya yake kupiga propaganda chafu za kisiasa.
Hadi sasa, mawaziri ambao taarifa za kuugua kwao zinafahamika ni pamoja na Profesa Mark Mwandosya mwenye dhamana ya Maji, Naibu Waziri Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk Chami. Wengine ambao taarifa zinaonyesha kuwa walikuwa nje ya nchi kwa matibabu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.
Waziri Profesa Mark Mwandosya
Ingawa haijafahamika maradhi yanayowasumbua hadi sasa, wadadisi wa mambo ya kisiasa wamekuwa wakichukulia hali ya afya ya baadhi yao kama moja ya sababu inayoweza kuwafanya wawekwe kando pale Rais Jakaya Kikwete atakapoamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kuwapa fursa ya kupumzika na kuendelea na matibabu.
Dk Chami
Waziri Dr. Harison Mwakyembe
Dk Chami alisema jana kwamba tangu arejee kutoka India alikokwenda kutibiwa, afya yake imeimarika na hakuna siku aliyoshindwa kutekeleza majukumu yake huku akisema wanaoeneza uvumi huo ni mahasimu wake kisiasa wanaonyemelea nafasi yake.
Waziri Mathias Chikawe
Alisema mbali ya kufika ofisini kwake kila siku, alishiriki kikamilifu kwenye Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uliomalizika hivi karibuni Mjini Dodoma na kujibu hoja mbalimbali zilizoelekezwa kwa wizara yake.
Aliwalinganisha maadui zake kisiasa na fisi mwenye uchu anayemfuatilia mtu kwa nyuma bila kujali umbali wa safari kwa matumaini ya kuneemeka mkono ukidondoka huku akisema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri wake kwa vigezo anavyoona vinafaa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
Waziri Celina Kombani
“Nashangaa sana, afya yangu ni njema, imeimarika. Tangu nimerejea kutoka India, sijawahi kwenda hospitali wala zahanati yoyote, naingia ofisini kila siku kuanzia asubuhi na kutoka jioni, nimehudhuria Mkutano wa Bunge, Dodoma na leo nina kazi ya kutembelea viwanda, sasa huku ndiko afya yangu kuzidi kudorora?,” alihoji Dk Chami na kuongeza:
“Suala kubwa hapa ni uwaziri, lakini mtu unaposema fulani anaumwa sana au haumwi lazima usimame katika ukweli.
Hizi ni propaganda chafu za kisiasa zinazoenezwa na baadhi ya watu wenye uchu wa kutaka nafasi hii. Rais ana mamlaka yake ya kuteua mtu kwa vigezo anavyoona vinafaa na mamlaka hiyo haitegemei afya ya mtu. Anaweza kuwa mzima au mgonjwa lakini anateua kwa kadri itakavyompendeza yeye.”
Dk Chami aliwataka wananchi wa jimbo lake la Moshi Vijijini kutokuwa na hofu kuhusu afya yake akisema imeimarika na amejipanga kuongoza mapambano ya kuleta maendeleo.
Chami alirejea nchini mwishoni mwa mwaka jana kutoka India alikotibiwa kwa miezi miwili akiwashukuru Watanzania kwa moyo wa upendo walioonyesha kwake kwa baadhi yao kufunga na kufanya mikesha, kumuombea ili apone.
Kinachomsibu
Akizungumzia ugonjwa uliompeleka India, Waziri huyo alisema alikuwa akisumbuliwa na maumivu upande wa kulia wa kifua chake na alipofika India, ilibidi madaktari wamkate kipande cha nyama na kukisindika ili kutambua bakteria husika baada ya awali, kushindwa kuwabaini.
Alisema wakati akiendelea na tiba hiyo, dawa alizokuwa akizitumia zilimletea athari, iliyosababisha mwili kuvimba. Alisema kifua kilipata ahueni mapema na muda mrefu ulitumika kutibu uvimbe aliopata.
Akiwa katika ziara kutembelea kiwanda cha MMI Steel, Dk Chami alitumia fursa hiyo kuelezea pia afya yake akitamba yupo 'fiti' na hana mgogoro wa kiafya kama baadhi ya watu wanavyojaribu kumshinikiza Rais Kikwete afanye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
“Nipo vizuri sana na uzito umeongezeka kwa kilo 15. Sasa wale ambao wanafikiria kuwaona wengine katika masanduku (majeneza) watasubiri sana” alisema.
Kombani na Chikawe
WaziriKombani alipelekwa nje ya nchi kutibiwa na sasa amerejea nchini. Awali, taarifa zilisema alipaswa kwenda kufanyiwa upasuaji ambao hata hivyo, haukuwekwa wazi.
Waziri huyo hakuonekana katika Mkutano wa Sita wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema ndiye aliyekuwa akijibu maswali ya Wizara Katiba na Sheria.
Jana, taarifa zilizopatikana wizarani kwake zilisema Kombani hajaonekana ofisini kwa takribani wiki tatu.
Baadhi ya vigogo wa wizara hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, walisema waziri huyo hayupo ofisini kutokana na kuumwa na kwamba alikuwa nje ya nchi wa matibabu kwa takriban wiki tatu.
Msemaji wa wizara hiyo, Omega Ng’ole alisema hajui kama Waziri Kombani alikuwa anaumwa huku akisema waziri kwenda nje au kutokwenda kwa ajili ya matibabu ni suala binafsi hivyo kushauri atafutwe mwenyewe.
Akizungumza kwa simu, kuhusu afya yake Kombani alihoji: “Unataka kufahamu kama mwandishi au ndugu?” baada ya kujibiwa alisema si jambo baya kwa kiongozi kwenda au kupelekwa nje ya nchi kutibiwa.
“Hivi mtu kuumwa ni jambo la kutangaza kweli… nini cha kushangaza kama mtu akiumwa?,” alihoji.
Alisisitiza kwamba, hakuna ubaya kwa kiongozi yoyote kwenda nje ya nchi kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
“Mtu akienda nje kufanyiwa uchunguzi hiyo nayo ni habari? Hilo jambo kwangu ni mambo madogo tu, hiyo siyo habari bwana,” alisema Kombani na kuongeza kuwa hawezi kusema kama ni mgonjwa au la kwa kuwa hilo ni jambo lake binafsi... “Mimi nakwenda nje kila siku, kila wakati katika shughuli zangu za kikazi na hata siku moja sijawahi kuulizwa na mtu.”
Kwa upande wake, Waziri Chikawe naye anadaiwa kwamba hivi karibuni alikwenda India kupata matibabu. Hata hivyo, haikuelezwa kinachomsibu kutokana na usiri mkubwa uliopo serikalini juu ya matibabu ya viongozi hao.
Dk Mwakyembe
Dk Mwakyembe ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi na kupelekwa India Oktoba 9 mwaka jana, anatarajiwa kwenda tena nchini humo wakati wowote kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.
Mmoja wa watu wa karibu na Dk Mwakyembe alisema juzi kwamba Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anatarajiwa kurudi katika Hospitali ya Appolo kwa ajili ya kuangalia kama matibabu aliyopata yamemsaidia kwa kiwango gani.
Ingawa Dk Mwakyembe alijitokeza hadharani katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe hivi karibuni, hali ya afya yake haikuwa ya kuridhisha kutokana na ngozi yake kuonekana imeathirika.
Profesa Mwandosya
Profesa Mwandosya ambaye amekuwa akitajwa kama mmoja wa makada wa CCM ambao wangeweza kuwa tishio katika mbio za urais ndani ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Appolo kwa zaidi ya miezi mitatu. Sasa hivi, Waziri Mwandosya nchini India ambako anaendelea kupata matibabu.
Ikulu
Kuhusu taarifa za kuwepo kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Kurugenzi ya Mawasiliano imesema wajibu wa kubadilisha baraza hilo uko kwa Rais ikiwa ataona kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana jioni alipokuwa akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds FM na kusisitiza: “Rais atakapoamua kufanya hivyo atafanya kwa matakwa yake mwenyewe.”
Polisi: Hatutambui maridhiano ya kuwanusuru wanaharakati
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni
JESHI la Polisi Wilaya ya Kinondoni limesema halitambui maridhiano ya madaktari na Serikali ya kuwaachia huru wanaharakati walioandamana kushinikiza Serikali kutatua madai ya madaktari.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyera alisema wanaharakati hao watafikishwa mahakamani kama watuhumiwa wengine.
Alisema Jeshi la Polisi ni Taasisi inayojitegemea na haiwezi kufanya kazi kwa shinikizo la madaktari.
Kenyera alisema wanaharakati 16 waliokamatwa na Jeshi hilo watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa iwapo mwanasheria wa Serikali ataona kuna umuhimu wa kupelekwa mahakamani.
“Ninachoweza kusema hapa, upelelezi umekamilika na tumeshapeleka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) ndiye mwenye uamuzi wa kuwafikisha mahakamani,” alisema. Jana jeshi hilo lilishindwa ama kuwaachia au kuwafikisha mahakamani wanaharakati 16 waolitiwa mbaroni Alhamisi iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakidaiwa kutaka kuandamana kuishinikiza Serikali kumaliza haraka mgogoro wake na madaktari.
Pia wanaharakati hao wanadaiwa kukutwa na mabango 30 yenye ujumbe tofauti wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na madaktari ambao walikuwa katika mgomo na kudaiwa kufunga baadhi ya barabara za jjiji la Dar es Salaam siku moja kabla ya kukamatwa kwao.
Wanaharakati hao waliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam jana (Jumanne) lakini walipofika kituoni hapo walielekezwa kuonana na Ofisa Upelelezi Makosa ya Jinai Wilaya ya Ilala (RCO), Kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa ajili ya maelekezo zaidi.
"Wametutaka turipoti kwa RCO Ilala, wanasema kwa kuwa tulikamatwa Muhimbili suala letu linatakiwa kwenda Ilala na hapa Oysterbay limeletwa kimakosa," alisema Mkurugenzi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo-Bisimba.
Akizungumza na wanaharakati hao ofisini kwake, Ofisa Upelelezi Ilala, Duwali Dila aliwaambia kuwa suala lao lipo katika ngazi nyingine linashughulikiwa na warudi tena kituoni hapo Jumatatu wiki ijayo ambapo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kujua kinachoendelea.
"Nafikiri tuonane Jumatatu, labda tukubaliane muda kwani suala hili kulingana na taratibu zetu siku hizi za jeshi la polisi lazima lipitie ofisi ya DPP kabla ya kufika kwetu," alisema na kuongeza kuwa sio wao polisi ambao wanatakiwa kuandaa mashtaka.
Alisema ofisi hiyo ndio ambayo inapaswa kuandaa shtaka kama lipo baada ya kupitia vielelezo vyote na kujiridhisha kuwa kuna tuhuma ambazo zinapaswa kupelekwa mahakamani au vingine kisha kuwasilisha polisi.
Dila aliwahakikishia kuwa Jumatatu ndio itakuwa siku ya mwisho kwani mchakato utakuwa umekamilika, hoja ambayo ilikubaliwa na wanaharakati hao ambao waliondoka ofisini hapo na kuendelea na shughuli zao zingine.
Wanaharakati hao walikamatwa wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa na mkutano na madaktari waliokuwa katika mgomo na walipopekuliwa katika magari yao, ambapo walikutwa na mabango 30 yenye jumbe mbalimbali ambayo yalikuwa yanaishinikiza serikali kumaliza mgogoro wake na madaktari.
Pia siku moja kabla wanaharakati hao walifanya maandamano ya kutaka kwenda Ikulu ambayo yalisababisha kufungwa kwa barabara ya Ocean na Ali Hassan Mwinyi eneo la Palm Beach, jijini Dar es Salaam kabla hawajaamriwa kutawanyika na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasi (FFU).

Wednesday, February 15, 2012
Tamko Chadema Uchaguzi mdogo Arumeru
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza ratiba yake ya kushiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha huku wanachama wake wanne wakiwa tayari wamejitokeza kuomba kuteuliwa.
"Chama cha Chadema kinawahakikishia … kitashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Arumeru Mashariki, kwa lengo la kushinda,” alisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika katika taarifa yake jana.
Alisema fomu zilianza kutolewa tangu jana na kwamba mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Februari 25.
Mnyika alisema fomu zinatolewa katika Ofisi ya Chadema ya Wilaya ya Arumeru, Maji ya Chai-USA River na pia katika Ofisi za Chadema za Mkoa wa Arusha.
“Baada ya hapo vikao vya chama vinavyohusika na uteuzi vitafanyika ili kumpata mgombea mmoja,” alisema.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo hilo, Jeremia Sumari.
Mnyika alisema anaamini umakini na uimara ambao kimeendelea kuudhihirisha katika kuwatumikia na kuwawakilisha Watanzania, kitashinda.
Mchakato wa uteuzi ngazi ya jimbo na wilaya utafanyika kati ya Februari 26 na 29, mwaka huu wakati uteuzi ngazi ya taifa utafanyika Machi 3 Machi mpaka 4.
Waliochukua fomu
Wanachama wa Chadema waliojitokeza kutaka kupeperusha bendera ya chama hicho ni Joshua Nasari, Samweli Shami, Francis Tembo na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Wilaya ya Arumeru (Bawacha), Anna Mwagirwa.
Kujitokeza kwa wanachama hao wanne wa Chadema, kunafanya idadi ya waliojitokeza kuwania kiti hicho kufikia sita. Juzi, wanachama wawili wa CCM walichukua fomu kupitia chama hicho.
Waliojitokeza ni pamoja na mtoto wa Sumari, , Sioi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, William Ndeoya Sarakikya.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema Mkoa wa Arusha, Ephata Nanyaro alisema wanachama hao wanatarajiwa kuanza kupewa fomu za kugombea leo.
Alisema utaratibu wa kura kumpata mgombea wa chama hicho, unatarajiwa kutangazwa mara baada ya kukamilisha kikao cha sekretarieti ya Chadema, Dar es Salaam.
Sarakikya akana
Katika hatua nyingine, William Sarakikya aliyechukua fomu juzi kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, amesema kwamba si mtoto wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali, Mirisho Sarakikya.
Akizungumza jana mjini Arusha, Sarakikya alisema kwamba wote ni wa ukoo mmoja lakini hajazaliwa na Mkuu huyo wa majeshi wa zamani.
Wakati William akikanusha, Jenerali Sarakikya naye alisema jana kwamba mgombea huyo anatokea katika ukoo wake, lakini siyo mtoto wake wa kumzaa.
“Kimsingi ukoo wote wa Sarakikya ni ndugu lakini William siyo mtoto wangu wa kumzaa, ni mtoto wa jamaa yangu. Mimi nina watoto wanne ambao hawako kabisa kwenye siasa,” alisema Mstaafu huyo wa jeshi na kutaja kazi za wanaye hao kuwa ni udaktari, uhandisi ualimu na taaluma ya benki.
Dk Mwakyembe kurejea India kwa matibabu
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe anatarajia kuondoka nchini
wakati wowote kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu.
Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo Oktoba 9 mwaka jana, alilazimika kupelekwa katika Hospitali ya Appolo nchini India kwa matibabu zaidi.
Jana, vyanzo vya karibu na Dk Mwakyembe vilidokeza gazeti hili kwamba naibu Waziri huyo na Mbunge wa Kyela anatarajiwa kurudi Appolo, kwa ajili ya kuangalia kama matibabu aliyopata yameweza kumsaidia kwa kiwango gani.
Vyanzo hivyo vilivyo karibu na Dk Mwakyembe, vilifafanua kwamba anachokwenda kufanya India ni "Uchunguzi tu wa kawaida kuona maendeleo ya matibabu."
"Atarudi katika uangalizi wa kawaida, kwasababu amekuwa akipata matibabu hivyo lazima achunguzwe kuona dawa alizokuwa akitumia zimemsaidia kwa kiwango gani," alisema.
Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, hivi karibuni alijitokeza na kutoa kauli nzito kuhusu chanzo cha maradhi yanayomsibu, huku Serikali ikiendelea kukaa kimya hata baada ya washirika wake wa karibu kusisitiza kwamba alipewa sumu.
Itakumbukwa kwamba, mwaka jana, Dk Mwakyembe akiwa na hali mbaya alipelekwa katika Hospitali ya Appolo, nchini India kwa matibabu baada ya kuugua maradhi yaliyosababisha ngozi yake kuharibika. Tangu arejee mwanzoni mwa mwezi uliopita alikuwa hajaonekana hadharani, mbali na kutoa tamko kwamba afya yake ilikuwa inaendelea vizuri.
Hata hivyo, muda wote huo aliokuwa nchini India na baada ya kurudi nchini, mazungumzo ya watu maofisini, nyumbani, mitaani na vijiweni yalitawaliwa na utata wa suala la afya ya Dk Mwakyembe, huku uvumi, tetesi na minong’ono kwamba maradhi yake yalisababishwa na hujuma za kisiasa vikitawala hisia za wananchi.
Hisia hizo zilikuzwa na kauli ya mmoja wa washirika wake kisiasa, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta ambaye alimtembelea hospitalini nchini India na baadaye kutoboa hadharani kwamba Dk Mwakyembe alikuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake dhidi ya mafisadi.

Kiongozi atokomea na mamilioni ya fedha UVCCM
Peter , Arusha
MMOJA wa wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, anadaiwa kutoroka na zaidi ya Sh26 milioni za jumuiya hiyo zilizochangwa kwenye harambee iliyofanyika Mei 9, mwaka juzi na kuongozwa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha. Akizungumza kwa simu kutoka Mererani, Simanjiro, Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo, Kiria Laizer alithibitisha kuwa fedha hizo zilizochangwa kwa lengo la kutunisha mfuko wa maendeleo ya vijana Simanjiro ziliyeyuka muda mfupi baada ya harambee hiyo.
Katika harambee hiyo, Nahodha ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alichanga fedha taslimu Sh2 milioni.
Ilielezwa kwamba wageni wawili waliohudhuria shughuli hiyo kwa mwaliko wa mtuhumiwa huyo ambao walitambulishwa ukumbini kuwa dada wa Rais Kikwete, walichangia 400,000.
Kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za shughuli hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu ambaye sasa ni Mbunge wa Lushoto (CCM), alichangia Sh500,000.
Viongozi wengine waliohudhuria na kiasi walichochanga kwenye mabano ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Khalid Mandya (200,000), Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka (Sh1.5 milioni), na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas Ole Mukusi (Sh100,000).
Laizer alisema tukio la wizi huo limebaki kuwa kama mchezo wa kuigiza huku baadhi ya wanachama na viongozi wenzake wakimtuhumu hata yeye wakidhani alihusika kwa njia moja au nyingine.
“Baada ya mgeni rasmi (Nahodha) kunikabidhi mfuko wenye fedha usiku ule pale ukumbini, nilimwita (mtuhumiwa jina tunalo) na kumkabidhi mbele na wajumbe wawili wa kamati ya utekelezaji wilaya na tangu siku ile, sijawahi kumwona wala kupata mawasiliano naye,” alisema Laizer.
Aliwataja Wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshuhudia makabidhiano hayo kuwa ni Bonny Shongo na Paul Sipitet.
“Siku tatu baadaye tulimtafuta (mtuhumiwa), bila mafanikio na tulipompata kwa njia ya simu alidai yuko Mjini Arusha kwa shughuli binafsi lakini baada ya muda mfupi alitutumia ujumbe mfupi wa simu akitutaka kutafuta mtu mwingine (wa kujaza nafasi yake) kwani yeye ameondoka,” alisema Sipitet.
Katibu wa UVCCM wilayani humo, Mwanakombo Amiri alisema kwa simu hakuna kumbukumbu yoyote kwenye majalada ya kiofisi inayohusu kikao cha maandalizi wala fedha zilizopatikana kwenye harambee hiyo.
“Hakuna chochote kwenye faili kuhusu jambo hilo unalouliza. Kikao kilichopita cha kamati ya utekelezaji kilizungumzia suala hilo ingawa haikuwa moja ya ajenda. Ila kikao kijacho ambacho siwezi kukutajia kitafanyika lini hilo ni moja ya ajenda muhimu na tutatoa uamuzi kulingana na kanuni zetu,” alisema Mwanakombo.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, ambaye ni miongoni mwa waliotafuniwa fedha zao walizochangia alithibitisha ofisi yake kupokea taarifa za fedha za kuyeyuka kwake na kusema tayari ameziagiza ngazi husika (UVCCM), kuchukua hatua kulingana na kanuni na taratibu zao na pia kutoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.
“Sisi kama Serikali, chama kikichukua hatua na kuwasilisha taarifa, nitaagiza polisi wachukue hatua za kisheria kwa kuchunguza na kumtia mbaroni mtuhumiwa. Nakushauri pia uwasiliane na katibu wa CCM wilaya ambaye ndiye mlezi wa jumuiya zote za chama ngazi ya wilaya,” alisema Mandya.
Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya ofisi yake kutopata taarifa za utekelezaji wa amri yake ya mhusika kuchukuliwa hatua hadi sasa, ameamua kuuandikia barua rasmi uongozi wa UVCCM na chama wilaya kudai utekelezaji wa agizo lake kutokana na wahusika kuonekana wazito katika jambo hilo.
Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Jamila Mjungu alikataa kuzungumzia suala hilo akisema UVCCM ni jumuiya inayojitegemea, yenye viongozi na wasemaji na kanuni za kutatua matatizo yao.
Uchunguzi wa kina umebaini kuwa mtuhumiwa huyo sasa ni diwani katika moja ya kata za Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambako aligombea na kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema ingawa jambo hilo halijaripotiwa kwake na uongozi wa wilaya ya Simanjiro, atafuatilia na kuhakikisha mhusika anachukuliwa hatua kulingana na kanuni za jumuiya hiyo na sheria za nchi bila kujali cheo, umaarufu wala nasaba yake na viongozi.
“Kwanza inawezekana mtuhumiwa ni tapeli mzoefu anayetumia jina la mheshimiwa Rais na familia yake kuwatisha
60 Serikalini kuhakikiwa mali zao,Sitta ndani
TUME ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeanza mchakato wa kuhakiki mali
za viongozi wa umma nchi nzima ambapo kwa awamu ya kwanza itaanza na
vigogo 60 akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel
Sitta na Waziri Samia Suluhu Hassan wa Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano). Wengine ni wakuu wa mikoa na wilaya, Meya wa majiji,
madiwani, wabunge na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za Serikali. Zoezi la uhakiki wa mali za viongozi hao litaanza Februari 20 hadi Machi mosi mwaka huu ambapo linafanyika baada ya kukamilika kwa zoezi la urejeshaji wa fomu za utajaji mali na madeni kutoka kwa watumishi mbalimbali wa Serikali. Mbali na Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, wabunge wengine watakahakikiwa mali zao katika awamu hiyo ni John Mnyika(Ubungo), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Jerome Bwanansi (Lulindi), Faith Mitambo (Liwale) na Stella Manyanya (Viti Maalum).
Katika orodha hiyo yumo pia Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovock Mwananzila, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Didas Masaburi na Meya wa Jiji la Tanga, Guledi Mohamed. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Charles Nyamrunda, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemia Mchechu, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Placidus Luoga na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda alisema kuwa uhakiki huo ni nguzo bora ya kuijenga jamii ya Watanzania, hasa viongozi wa umma katika kuishi kwa kufuata misingi ya uadilifu, iliyowekwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Alisema kwa kuwa idadi ya viongozi ni kubwa na kwamba tume hiyo itaanza na uhakiki wa viongozi 60 wenye nyadhifa mbalimbali.
“Sisi tunachokiomba kutoka kwao ni kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wetu wakati wa zoezi zima la uhakiki wa mali zao,” alisema Kaganda. Alisema wananchi wanatakiwa kushirikiana na tume hiyo kutoa taarifa zitakazowasaidia kugundua mali zilizofichwa, ambazo zinadhaniwa kuwa ni za viongozi wa umma wanaoguswa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Aliwataka viongozi wanaohakikiwa kutokuwa na hofu kwa kuwa zoezi hilo ni la kawaida.
“Hawa hawana tuhuma zozote ni utaratibu wa kawaida tu,”alisema. Jaji mstaafu Kaganda aliliambia gazeti hili kuwa si kosa kwa kiongozi yoyote wa Serikali kuwa na mali na kwamba kosa ni mali hizo kupatikana kinyume na sheria. “Mbunge akiwa mfanyabiashara na biashara yenyewe inafuata sheria hilo sio tatizo ila tukigundua mali hizo au biashara inafanyika kinyume na sheria tunaweza kuwaeleza Takukuru" alisema Kaganda.
Alisema kuwa kwa sasa uadilifu kwa viongozi wa umma umeshuka hivyo zoezi kama hilo kwa kiasi kikubwa linaweza kurudisha uadilifu huo. Katika hatua nyingine, Jaji Kaganda alisema anafanya utafiti wa sheria ya kutenganisha biashara na uongozi. “Nafanya utafiti kuhusu sheria hii ila kwa sasa ni mapema mno kueleza nilipofikia,” alisema Kaganda.
Tuesday, February 14, 2012
Mnyika alalamikia vitu kupanda bei
MBUNGE wa Ubungo (Chadema) John Mnyika ameitaka Serikali kuchukua
hatua za haraka ili kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kutokana na
ongezeko kubwa la mfumuko wa bei uliopo sasa.
Mbunge huyo aliyasema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo alisema hali ngumu ya maisha iliyopo sasa inatokana na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu hali ambayo ni tishio kwa uchumi na wa nchi na maisha ya wananchi.
Alisema serikali inapaswa kutambua mfumuko wa bei uliopo sasa ni kama janga kwa taifa kwani hali hiyo inasababisha wananchi kuishi katika hali ngumu jambo ambalo linaweza kuchangia kushusha uchumi wa Taifa.
“Kwa sasa mfumuko wa bei umeongezeka kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linafanya maisha ya watanzania kuendelea kuwa magumu kwani wanashindwa kumudu bei za bidhaa hali inayozidi kuwasababishia ugumu wa maisha,” alisema Mnyika na kuongeza kwamba
“Kwa sasa serikali inatakiwa kulichukulia jambo hili kama dharura kwa kupeleka mpango wa dharura bungeni ili wabunge waweze kujadili na kulitolewa maamuzi ambao utasaidia kupunguza ugumu wa maisha kwa masilahi ya watanzania na kwa taifa ,” alisema
Alisema mfumuko wa bei ulipo nchini unasababishwa kupunguza uzalishaji wa bidhaa za ndani jambo ambalo kwa taifa linaweza kuleta madhara makubwa kiuchumi.
“Uchumi wa taifa unaweza kuporomoka kwa kiasi kikubwa kama jambo hili la mfumuko wa bei halitapewa kipaumbele kwani kwa sasa udhalishaji wa bidhaa za ndani unapungua hasa kwa bidhaa zinazotokana na kilimo,” alisema.
Alisema serikali inapaswa kuangalia kwa umakini matumizi ya fedha za serikali pamoja na kuporomoka kwa sarafu kunatokana na ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni pamoja na uagizaji wa mafuta na malighafi nyingine toka nje jambo ambalo ilitawezesha kupunguza mfumuko wa bei .
Kwa mujibu wa ripoti ya bei za bidhaailiyotolewa na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonyesha kwamba mfumuko wa bei nchini kuanzia Disemba 2011 umeongezeka hadi kufikia asilimia 19.8 ikilinganisha na asilimia 19.2 Novemba 2011

Katiba mpya CCM kuwang'oa mafisadi
KINGUNGE ADAIWA KUPINGA, ASEMA HAYALENGI KUBORESHA MFUMO WA CHAMA
SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitisha mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1977 juu ya namna ya kuwapata wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), imeelezwa kuwa mabadiliko hayo yanatarajiwa kuwa kitanzi kwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho tawala kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Juzi, Nec ya CCM ilibariki mabadiliko muhimu ya katiba ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa ndani ambayo ni pamoja na kuanzisha utaratibu ambao wajumbe wa NEC waliokuwa wanatoka mikoani, sasa watakuwa wanachaguliwa kutoka wilayani na wabunge, wawakilishi na madiwani sasa hawataruhusiwa kushika nyadhifa za chama.
Katika marekebisho hayo, viongozi wakuu wastaafu wakiwamo Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marais wa Zanzibar na makamu wenyeviti wa chama hicho, wameundiwa Baraza la Ushauri na sasa hawatakuwa wajumbe wa NEC.
Hata hivyo, uamuzi huo umepingwa vikali na baadhi ya wajumbe ambao walisema marekebisho hayo hayana tija zaidi ya kutaka kudhoofisha upande mmoja ambao uko kwenye harakati za urais mwaka 2015 na kuutaja kwamba, ni genge la watuhumiwa wa ufisadi.
“Wamejaribu kuondoa wazee wastaafu ili Kamati Kuu isiwe na watu ‘strong’, lakini yote hayo yanalenga kwa mtu siyo mfumo. Chama kinatakiwa kufanya marekebisho yake kwa mfumo siyo mtu... ngoja twende tutaona itakavyokuwa,” alisema mjumbe mmoja wa NEC ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Mjumbe mwingine ambaye pia hakutaja kutambushwa jina lake gazetini alisema uamuzi huo wa kurejesha nafasi hizo wilayani, unalenga kuwazuia baadhi ya watu wasiingie katika vikao hivyo vya uamuzi na kuwazuia watuhumiwa wa ufisadi kuweka watu wao katika wilaya zote nchini hata kama wana fedha.
Alisema hata kama watuhumiwa wa ufisadi wana fedha nyingi, itakuwa vigumu kwao kuweza kupandikiza watu wao katika wilaya zote nchini.
“Kwa hiyo sasa hivi angalau kutakuwa na mkakati wa kuhakikisha mafisadi hawaweki watu wao wengi wilayani. Kwani itakuwa vigumu kumudu kuweka wajumbe wa NEC wilaya zote nchini, lakini pia, wao wenyewe itawawia vigumu kupenya.”
Mwishoni mwa mwaka jana, mpango wa kujivua gamba ndani ya CCM uligonga ukuta katika kikao cha NEC hatua ambayo ilimfanya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kutumia busara na kurejesha utekelezaji wa mpango huo kwenye Kamati Kuu (CC) kwa utekelezaji.
Kingunge apinga
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru, ndiye mjumbe pekee aliyepinga marekebisho hayo, huku akiituhumu sekretarieti kwa kukiuka katiba ya chama hicho.
Kingunge anadaiwa kuwatuhumu Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kwa kuvunja katiba hiyo kutokana na Halmashauri Kuu kutokuwa na uwezo wa kupitisha marekebisho hayo zaidi ya kupendekeza kwa Mkutano Mkuu ambao ndiyo wenye mamlaka hayo.
"Mzee ametueleza wazi kabisa kwamba marekebisho hayo hayana maudhui zaidi ya kumlenga mtu mmoja, aliuza sekretarieti imepata wapi kwamba Halmashauri Kuu ina uwezo wa kufanya marekebisho haya?,” alisema mtoa habari hayo.
Lakini, katika utetezi wake, Sekretarieti ilisema kuna kifungu kinachotoa mamlaka hayo kwa NEC kupitisha marekebisho hayo na kutoa taarifa kwa Mkutano Mkuu. Hata hivyo, Kingunge hakukubaliana na hoja hiyo.
Ilielezwa pia kwamba marekebisho hayo yaliyopitishwa kwa kupigiwa kura na wajumbe kwa kupata theluthi tatu kutoka Tanzania Bara na nyingine tatu kutoka Visiwani, wote walikubali isipokuwa Kingunge pekee.
“Ila tulichojifunza kwa Mzee (Kingunge) ni kwamba lazima utetee unachokiamini hadi mwisho na alimtaka Katibu Mkuu kuandika kuwa amepiga kura ya hapana ili iwe kwenye kumbukumbu,” chanzo chetu kilieleza.
Hata hivyo, Kingunge alipotafutwa jana kwa simu kufafanua msimamo wake hakutaka kuzungumza chochote akisema kwamba alikuwa kikaoni...”Samahani niko kwenye kikao, asante.”
Yapokea taarifa ya Katiba Mpya
Katika hatua nyingine, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema Nec imepokea taarifa ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Tanzania na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa lakini ikaitaka Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, huku akitaka wanachama wao kujitokeza kutoa maoni pindi tume itakapoundwa.
Nape alisema mjadala ulikuwa iwapo Tume ya Maadili iundwe au la lakini kutokana na katiba kuruhusu kuundwa kwa tume mbalimbali wajumbe walikubaliana iundwe.
Aidha, alisema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alitoa taarifa ya mgomo wa madaktari na wajumbe waliitaka Serikali kuharakisha makubaliano yaliyofikiwa na iwe inachukua hatua kabla ya migomo kusababisha madhara kama ilivyotokea.
Uchaguzi Mdogo Arumeru
Alisema NEC imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM kwenye uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki na viti vinane vya udiwani vilivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, utaratibu utakaotumika katika nafasi ya ubunge ni ule wa kura za maoni kwenye mkutano mkuu wa jimbo na kwamba Februari 13 hadi 18 wagombea watachukua na kurejesha fomu. Februari 20, mkutano mkuu wa jimbo utapiga kura na kesho yake, kamati ya siasa ya Wilaya ya Arumeru itajadili wagombea na kutoa mapendekezo kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa ambayo itakutana Februari 24 na kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu ya CCM ambayo itakutana Februari 27.

Muhimbili katika kashfa tena
Habari zilitolewa na wazazi wa Imrani, zilisema mtoto huyo amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, katika hospitali hiyo.
Wazazi hao walisema mtoto wao amekuwa katika chumba hicho muda wa miezi sita sasa huku akiwa anapoteza fahamu. Kwa mujibu wa habari hizo, mtoto huyo alichomwa sindano hiyo na mmoja wa madaktari katika Kitengo cha Upasuaji.
Hii ni mara ya pili kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kukumbwa na kashfa ya aina hiyo ndani ya kipindi cha takriban miaka mitano iliyopita. Novemba mosi mwaka 2007, wagonjwa wawili waliokuwa wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), iliyoko katika hospitali hiyo, walifanyiwa upasuaji kinyume cha matatizo yaliyokuwa yakiwakabili.
Katika upasuaji huo tata, Immanuel Didas aliyekuwa anasumbuliwa na goti baada ya kupata ajali ya pikipiki, alifanyiwa upasuaji wa kichwa na Immanuel Mgaya aliyepaswa kufanyiwa upasuaji wa kichwa , alifanyiwa upasuaji wa mguu. Katika tukio la mwaka huu lililothibitishwa na wazazi mtoto huyo wa umri wa miaka mitatu, Iramni alichomwa sindano hiyo Julai 28 mwaka jana.
Mama wa mtoto huyo Amina Mwerangi ambaye aliwahi kuwa mshindi wa mashindano ya ulimbwende katika Mkoa wa Ruvuma mwaka 2003/04, alisema alimpeleka mtoto huyo Muhimbili ili akafanyiwe upasuaji mdogo wa nyama zilizoota puani.
"Baada ya kuchomwa sindano hiyo, mtoto alipatwa na mshtuko uliosababisha mapigo ya moyo wake kusimama. Tatizo hilo sasa limemletea mtindio wa ubongo na kupooza mwili wote," alisema Mwerangi.
Mwerangi alisema jitihada zake za kumpata daktari aliyemchoma sindano hiyo Imrani, hazikuzaa matunda na kwamba Dk Edwin aliyekuwa amfanyie upasuaji huo, hataki kujihusisha na tatizo hilo.
“Mtoto amelazwa ICU kwa miezi sita sasa huku kukiwa hakuna matumaini ya kupata nafuu, jambo la kushangaza ni kuona madaktari wakiwa hawataki kumpa rufaa ili apelekwe nje kwa matibabu zaidi,” alisema mama wa mtoto huyo.
Alisema katika upasuaji aliopaswa kufanyiwa, Imrani alifunguliwa jalada lenye namba IP.No.A586301 lililoeleza kuwa alikuwa na tatizo la kuota nyama kwenye njia ya hewa puani na kwamba nyama hizo zilikuwa zinamfanya apate shida katika kupumua.
Alisema mtoto huyo ambaye kabla ya kusababishiwa tatizo hilo jipya alikuwa anasomo katika Shule ya Awali ya Mtakatifu ya mjini Dodoma, alibainika kuwa na ugonjwa huo wakati alipoanza kutambaa.
“Baada ya kumpeleka Hospitali ya Muhimbili katika kliniki ya kawaida, waliniambia kuwa mtoto anapaswa kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuondoa nyama hizo na Julai 28 mwaka jana, nilikwenda hospitalini hapo kupata huduma hiyo,” alisema Mwerangi.
“Nilipokewa na mtoto na siku iliyofuata kwa maana ya Julai 29 alipelekwa katika chumba cha upasuaji kufanyiwa huduma hiyo, lakini kabla ya hapo alipigwa sindano ya usingizi iliyomsababisha apate mshituko,” alidai mama huyo.
Alisema kutokana hali hiyo, mapigo ya moyo ya mtoto yalionyesha dalili za kusimama na hivyo akahamishiwa katika chumba cha wagonjwa wa moyo wanaohitaji uangalizi maalumu.
“Mtoto alilazwa katika chumba hicho hadi Januari 24 mwaka huu, alipohamishiwa katika ICU ya kawaida ambako ndiko aliko hadi sasa,” alisema.
Mwerangi alisema taarifa ya kitabibu iliyotolewa baada ya kufanyiwa vipimo vya CT Scan, ilionyesha kuwa mtoto huyo amesababishiwa mtindio wa ubongo na kwamba mwili wote umepooza.
“Kila nikiuliza ni daktari gani aliyempiga sindano mtoto, sipewi jibu, kila mmoja anasema hajui na kwamba walimkuta tu ndani ya chumba cha upasuaji akiwa hivyo. Badala yake wananiuliza kuwa kwani dereva akisababisha ajali na watu wakafa yeye akapona atasimama,” alisema mama wa Imrani.
Mwerangi alisema mbali na kumficha daktari aliyemchoma sindano mtoto, pia amekuwa akinyimwa ruhusa ya kumpeleka nje ya nchi kwa matatibu zaidi.
“Nilikwenda kwa Mkurugenzi wa huduma za tiba ya ugonjwa nyama, akasema hakuwa na taarifa na akashangaa sana kusikia eti mtoto amekuwa ICU kwa muda wote huo,”alisema.
“Aliniambia angezungumza na madaktari waliotaka kumfanyia upasuaji mtoto. Lakini hadi sasa hakuna taarifa wala hatua zozote zilizochukuliwa,” alisisitiza mama Imrani.
Hata hivyo alimshukuru Dk Ulisubisya kwa kumpa ushirikiano wa karibu licha ya ukweli kwamba si daktari aliyemhudumia mtoto.
Alisema pamoja na mambo mengine, daktari huyo ndiye aliyewezesha kupatikana kwa taarifa ya kitabibu za mtoto huyo.
Uongozi wa hospitali
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili, Dk Merina Njelekela, na Ofisa Uhusiano wake, Aminiel Aligaeshi, hawakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo, licha ya juhudi za kuwatafuta.
Juzi mwandishi wa habari hii alikwenda kwa ofisa uhusiano ili kupata ufafanuzi wa madai hayo, lakini jitihada hizo zililigonga mwamba baada ya kukataliwa kumuona.
Juhudi kama hizo ziligonga mwamba pia katika kumpta Dk Njelekele ofisini kwake, kufuatia kitendo cha wasaidizi wake kumzuia mwandishi kuonana naye kwa maelezo kuwa ana kazi nyingi.
Hata hivyo, Ofisa Uhusiano Msaidizi wa hospitalini hiyo, Jeza Waziri, ambaye awali alisema hawezi kuzungumza lolote, alisema hakuwa na taarifa kuhusu tukio hilo.
Monday, February 13, 2012
Wana Chipolopolo wafanya maajabu Gaboni
Zambia
Habari zaidi katika michezo/Sports
| Habari zaidi katika michezo/Sports |
Subscribe to:
Posts (Atom)