NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, July 10, 2012

Dk. Migiro augwaya urais



NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, aliyemaliza muda wake, Dk. Asha-Rose Migiro, amegoma kuweka bayana kama ana mpango wa kuwania wadhifa wa urais kama ambavyo amekuwa akibashiriwa na badala yake alisema kwamba ataendelea na kazi yake ya ualimu.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea nchini jana akitokea Marekani, Dk. Migiro alisema kuwa kwa sasa anapumzika kwa muda kabla ya kurudi tena kwenye ulingo wa siasa.
Mwanasiasa huyo, amekuwa akitajwa sana siku za hivi karibuni kama mmoja wa watu wanaoweza kusimamishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kurithi mikoba ya Rais Jakaya Kikwete.
Bila kukubali wala kukataa, Dk. Migiro aliyeitangaza nchi kwenye ramani ya dunia, alisema, “Kwa taarifa yenu nchi hii tayari ina Rais na mimi baada ya kumaliza kipindi changu cha miaka mitano UN nina hamu ya kurejea nchini…nimerejea kama mama wa familia, kama dada na kama mwalimu.
“Nitakuwa nje ya siasa kwa muda; unajua baada ya kumaliza utumishi wako UN ziko taratibu unazotakiwa kufuata; pia siku mbili kabla ya kumaliza muda wangu Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, aliniteua kuwa mjumbe wa Kamati ya Ukimwi, hivyo sijajua majukumu yangu yatakuwaje,” alisema Dk. Migiro.
Dk. Migiro ambaye kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, aliwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9:28 alasiri na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Nafurahi kumaliza miaka mitano kwa mafanikio; nitarudi Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kutoa taarifa kwamba nimerejea nchini… kwa sababu wakati naondoka nilichukua likizo bila malipo ambayo imekwisha mwaka jana… nilikuwa mwalimu kwenye Kitivo cha Sheria,” alisema Dk. Migiro.
Kabla ya kurejea Tanzania naibu katibu mkuu huyo, aliandika waraka maalum na kuutuma kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ukiwa na kichwa kisemacho ‘Hakika, kila chenye mwanzo hakikosi mwisho na kila mwisho wa jambo moja huwa mwanzo wa jingine.’
Kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya, Dk. Migiro alipongeza na kusema miongoni mwa mambo aliyoyasimamia alipokua UN ni utawala wa sheria na haki za binadamu huku akisisitiza kwamba upatikanaji wa Katiba mpya ni jambo muhimu.
Chanzo cha habari Tanzania Daima

Monday, July 9, 2012

Wanavijiji Wakristo Nigeria wauwawa

Jeshi la Nigeria linasema kuwa watu 37 wameuwawa kwenye mashambulio katika vijiji vya Wakristo karibu na mji wa Jos, katikati mwa nchi.
Mashambulio kadha yameshawahi kufanywa Nigeria


Msemaji wa jeshi, Mustapha Salisu, alisema askari wa usalama walipigana vikali kwa saa kadha, na wale aliosema walikuwa washambuliaji wajuzi.
Alisema zaidi ya washambuliaji 20 waliuwawa.
Msemaji wa kikundi cha Wakristo alisema vijiji 13 vilishambuliwa.

Morsi akaidi amri ya jeshi

 
Katika hatua ya kulikaidi jeshi lenye nguvu nchini Misri, rais mpya Mohammed Morsi, ametoa amri kuwa bunge likutane.
Rais Mohammed Morsi wa Misri

Amri yake inakwenda kinyume na hukumu iliyotolewa mwezi uliopita na mahakama ya katiba, kwamba bunge la sasa siyo halali.
Bunge hilo lina wajumbe wengi wa vyama vya Kiislamu.
Hukumu ya mahakama ilitekelezwa na jeshi, ambalo lilifuta bunge na kujipa madaraka ya kutunga sheria.
Televisheni ya taifa inasema halmashauri ya jeshi itafanya kikao cha dharura kujadili amri ya Rais Morsi.

Wafungwa Malawi watimka

    Wafungwa kwenye gereza moja ya Malawi wamefanya ghasia kupinga msamaha waliopewa baadhi ya wafungwa wenzao, ambao wanaona haukuwa wa haki.
Rais Joyce Banda

Rais Joyce Banda, siku ya Ijumaa aliwasamehe wafungwa karibu 400, lakini siyo wale waliofungwa kwa sababu ya mauaji au ubakaji.
Wafungwa katika gereza ya Zomba, mashariki mwa nchi, walitoroka kwenye seli zao na kuwabughudhi wasimamizi, wakisema wafungwa wawili waliosamehewa ni wahalifu wa mauaji na ubakaji.
Bibi Banda alisema wabakaji wanafaa kufa jela, hasa wale waliowabaka watoto.
Ubakaji wa aina hiyo unatokea mara kadha Malawi, kwa sababu kuna wanaoamini kuwa kufanya mapenzi na msichana bikira kunaleta mali na kunatibu HIV na UKIMWI.

Hizi ni kali hebu tazama hizi


Kilipofika kile kiwango cha kupendana sanaaaa jamaa analala kitanda kimoja na farasi wake...

jamaa kachoka ...kaamua kupata hapo hapo!
...Kimekuwa kipando tena!..

Friday, July 6, 2012

UN haitafadhili jeshi kukomboa Mali

Wapiganaji wa Kiisilamu wakiharibu makaburi ya kale
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema haliko tayari kuunga mkono harakati za jeshi la kanda ya Afrika Magharibi katika kukabiliana na wapiganaji wa Kiisilamu ambao wameteka kaskazini mwa Mali.
Baraza hilo limelaani uharibifu,wa makuburi na minara ya kale katika mji wa Timbuktu ambao umewekwa chini ya urithi wa dunia na kusema uharibifu huo ni sawa na uhalifu wa kivita. Muungano wa kanda ya Afrika Magharibi, ECOWAS unanuia kutuma wanajeshi 3,00 nchini Mali.
Hata hivyo afisa wa kibalozi wa Umoja wa Mataifa ameambia BBC kwamba Baraza hilo limeomba kupata taarifa zaidi, ili kujua malengo ya harakati za jeshi la ECOWAS kabla ya kufadhili. Majirani wa Mali wametaka Umoja wa Mataifa kuunga mkono pendekezo lao kwa hofu ya maasi kusambaa katika maeneo mengine nje na Mali.
Kundi la Ansar Dine lenye uhusiano na mtandao wa Al Qaeda liliuteka mji wa Timbuktu mapema mwaka huu.Kundi hilo tayari limeharibu madhabahu ambayo linasema yamejengwa kinyume na imani ya Kiisilamu.
Msemaji wa Ansar Dine Sanda Ould Bamana aliambia BBC Sharia ya Kiisilamu hairuhusu makaburi yaliyojengwa kwa urefu wa zaidi ya inchi sita. Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni{UNESCO} pamoja na serikali ya Mali zimeomba kundi la Ansar Dine kusitisha harakati za kuharibu turathi hizo.
UNESCO pia imeelezea wasi wasi kwamba nyaraka za kale na vifaa vingine muhimu huenda vikaporwa na kuvukishwa kimagendo na imeziomba nchi jirani kuzuia kosa hilo kufanyika.
Timbuktu imepata sifa za kimataifa kutokana na eneo hilo kua moja wapo ya kitovu cha mafunzo ya imani ya Kiisilamu hususan misikiti yake iliyojengwa karne za 15 na 16. Timbuktu pia wanatoka Mawalii 333 ambao wanaheshimiwa sana katika madhehebu ya Sufi.
Ansar Dine ambao wana msimamo mkali{Salafist} wanapinga heshima kwa Mawalii.Waliuteka mji wa Timbuktu baada ya mapinduzi ya kijeshi kutokea. Katika mwanzo wa harakati za kutwaa kaskazini mwa Mali Ansar Dine walishirikiana na wapiganaji wa Tuareg waliotaka kujitenga na Mali.
Hata hivyo makundi hayo yametofautiana katika siku za karibuni hali iliyosababisha makabiliano makali katika maeneo matatu muhimu ya Mali ikiwemo Timbuktu, Gao na Kidal.

Kenya haitanunua mafuta tena Iran


Kiwanda cha mafuta Iran
Kenya imefutilia mbali mipango ya kununua mafuta ghafi kutoka nchini Iran, baada ya kutishiwa kuwekewa vikwazo. Hii ni kwa mujibu wa afisaa mkuu katika wizara ya kawi ya Kenya.
Kulingana na mkataba uliokuwa umefikiwa kati ya Kenya na Iran mwezi jana , nchi hiyo ilinuia kununua tani milioni nne za mafuta kutoka kwa kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Iran.
Lakini ubalozi wa Marekani nchini Kenya ulionya kuwa ni muhimu kusitisha mpango wowote utakaoipa mapato zaidi serikali ya Iran.
Marekani kwa ushirikiano na muungano wa ulaya wameweka vikwazo zaidi dhidi ya Iran kufuatia wasiwasi kuhusu mpango wake wa nuclear.
"Kwa sababu ya shinikizo za kimataifa , tumelazimika kusitisha mpango wetu" alinukuliwa akisema katibu katika wizara ya kawi nchini humo, Patrick Nyoike.
Mnamo siku ya jumapili, Muungano wa Ulaya uliwekea Iran vikwazo kamili vya kuuza nje mafuta, kuambatana na sheria ya Marekani ambayo inawekea vikwazo mshirika yeyote anayejihusisha na benki kuu ya Iran.
"Kuna vikwazo sasa dhidi watu watakaonunua mafuta na bidhaa zingine za mafuta kutoka kwa Iran, watachukuliwa hatua" alisema balozi anayeondoka wa Marekani nchini Kenya Scott Gration mnamo Jumatano kuhusu mipango ya Kenya kununua mafuta kutoka Iran.
Mwezi jana, maafisa katika mtambo wa pekee wa kusafisha mafuta nchini Kenya, walisema kuwa wataanza kununua mafuta ghafi.

Swahili Kwenye simu Habari Teknolojia mpya kutumika katika Premier

 Teknolojia ya kuthibitisha kama mpira umevuka msitari na kuingia wavuni, inayofahamika kama 'Goal-line technology', huenda ikatumiwa katikati ya msimu wa ligi kuu ya Premier ya England, ya mwaka 2012 hadi 2013, baada ya utaalamu huo kuidhinishwa na halmashauri ya kimataifa ya mchezo wa kandanda, IFAB, Alhamisi, mjini Zurich.
Teknolojia mbili ziliidhinishwa, moja ikifahamika kama 'Hawk-Eye', yaani 'jicho la mwewe', na ya pili inafahamika kama 'GoalRef', ikimaanisha 'mwamuzi wa goli'.
Habari zaida katika Michezo

Thursday, July 5, 2012

Korea Kusini kuvua Nyangumi


Uvuvi wa Nyangumi nchini Korea Kusini
Uvuvi wa Nyangumi nchini Korea Kusini
Korea Kusini imetangaza kuwa inataka kuanza uwindaji wa nyangumi chini ya sheria inayoruhusu uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya utafiti wa kisayansi, kama vile serikali ya Japan inavyofanya kwa sasa.
Serikali ya Korea Kusini, ilifichua hayo wakati wa mkutano wa kimataifa wa baraza linalosimamia na kulinda maslahi ya nyangumi nchini Panama, ambako walikuwa wakiwasilisha mipango yao kwa kamati ya sayansi ili kuchunguzwa.
Nyangumi hao watawindwa karibu na pwani ya Korea lakini haijulikana ni wangapi.
Uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya biashara imepigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa, lakini uwindaji wa nyangumi kwa minajili ya utafiti unaruhusiwa, hata kama nyama yake italiwa baadaye.
Korea ina historia ya ulaji wa nyama ya nyangumi kuliko eneo lolote ulimwenguni, na inakisiwa kuwa urauibu huo ulianza takriban miaka elfu nane iliyopita.

Shirika laonya baa la njaa Somalia


Mtoto mgonjwa anayekabiliwa na tishio la kuangamia nchini Somalia
Mtoto mgonjwa anayekabiliwa na tishio la kuangamia nchini Somalia
Shirika la Save the Children, limeonya kuwa ukosefu wa mvua ya kutosha na kuendelea kwa mzozo nchini Somalia, kunatishia kusambaratisha mafanikio yaliyoafikiwa tangu mwaka uliopita, wakati taifa hilo ilipokumbwa na baa la njaa.
Shirika hilo limesema ikiwa hali hiyo itaendelea, maisha ya maelfu ya watoto imo hatarini.
Shirika hilo la save the children, limesema idadi kubwa ya familia nchini Somalia, hawana uwezo wa kukabiliana na athari za ukame na kutoa wito wa kuongezwa kwa misaada zaidi ya dharura nchini Somalia.
Wakati huo huo, shirika hilo limetoa wito wa kubuniwa wa mikakati mipya ili kutambua na kusaidia taifa hilo kukabialana na athari za baa la njaa.
Mashirika kadhaa ya kutoa misaada ya kibinadam pia yametoa wito wa kuongezwa kwa misaada zaidi nchini Somalia, ambako maelfu ya watu waliangamia kutokana na baa la Njaa mwaka uliopita.

Kuhesabu kura kurudiwa Mexico


Shughuli ya kuhesabu kura nchini Mexico
Shughuli ya kuhesabu kura nchini Mexico
Maafisa wa tume ya Uchaguzi nchini Mexico wameamuru shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais katika zaidi ya asilimia hamsini ya vituo kote nchini kurudiwa.
Hii ni baada ya makosa kupatikana wakati wa kujumuisha kura kutoka vituo hivyo.
Mgombea wa Urais anayeongoza, Enrique Pena Nieto, ameiambia BBC kuwa chama chake cha PRI, hakikununua kura wala kufanya makosa yoyote.
Wakati mgombea wa Urais, Lopez Obrador, alipowasilisha malalamishi yake kuhusu utaratibu wa uchaguzi huo wa Urais mapema wiki hii, hata wafuasi wake sugu hawakutarajia tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali kiasi hicho.
Maafisa hao wametoa amri kura kutoka vituo 143,000 kuhesabiwa tena.
Hatua hiyo inatarajiwa kuwaridhisha wafuasi wa Bw. Lopez, lakini itamsumbua mgombea anayeongoza, Enrique Pena Nieto.
Bw. Pena Nieto, amekuwa na matumaini ya kutangazwa rais wa Mexico katika muda wa siku chache baada ya uchaguzi wa Jumapili.
Hata hivyo madai kuwa chama chake kilinunua kura katika baadhi ya maeneo, yamesababisha kura kuhesabiwa upya.
Akizungumza na BBC Bw Pena Nieto amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa chama chake kilifuata utaratibu unaofaa.

Tuesday, July 3, 2012

Makanisa ya Garissa yashambuliwa ten


Watu 16 wameripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuvamia makanisa mawili katika mji wa Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya hii leo.
Majeruhi wakitibiwa katika shambulio la zamani mjini garissa
Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu walifika eneo hilo, na haraka waliwapeleka majeruhi hospitali.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi nchini Kenya, Muhoro Ndegwa, watu waliouawa saba ni raia na maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda maeneo ya ibada katika kanisa la Africa Inland Church, AIC.
Kanisa jengine lililoshambuliwa ni Kanisa Katoliki ambapo magruneti mawili yalirushwa, ambapo moja liliripuka na kujeruhi watu kadha.
Hakuna mtu wala kikundi kilichodai kuhusika na mashambulio hayo, japo katika mashambulio kadhaa ya siku zilizopita yalihusishwa na wanamgambo wa Kiislam wa Somalia wa kundi la Al-Shabaab.
Kenya ilipeleka vikosi vyake nchini Somalia mwaka jana kuwasaka wapiganaji wa Al-Shabaab ambao wametajwa kutishia usalama wa nchi.
Matukio ya mashambulio dhidi ya maeneo ya ibada na yenye mikusanyiko ya watu wengi yamekuwa yakiripotiwa katika siku za karibuni nchini Kenya, na mwishoni mwa wiki iliyopita watu watatu waliuwawa katika klabu moja mjini Mombasa, baada ya kushambuliwa kwa magruneti.
Aliyeshuhudia tukio hilo, aliiambia BBC kwamba barabara sasa hazina watu, isipokuwa tu askari wa usalama.

Afisa mkuu mtendaji wa Barclays ajiuzulu

Bob Diamond
Bob Diamond
Afisa mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Bob Diamond hatimaye amejiuzulu.
Mwenyekiti anayeondoka Marcus Agius, ambaye alitangaza kujiuzulu kwake hiyo jana, sasa atakuwa mwenyekiti wa kudumu wa benki hiyo na ataongoza mikakati ya kumtafuta afisa mkuu mtendaji mpya.
Benki ya Barclays, imekumbwa na kashfa ya kuongeza viwango vya riba kinyume cha sheria.

Syria yadaiwa kukiuka haki za kibinadam

Shirika la Human rights watch  Shirika la Human rights watch
Shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights watch, ambalo limechapisha ripoti kuhusu kile kilichotaja kama sera ya serikali ya Syria, ambayo ni sawa na uhalifu na ukatili dhidi ya binadam.
Ripoti hiyo imenakaili mahala ambako serikali ya nchi hiyo imejenga vituo vya kuwazuia wapinzani wake na mbinu ya mateso inayotumika.
Shirika hilo limetoa wito kwa wale wanaohusika kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Haque, amesema viwango vya vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na serikali ya Syria Dhidi ya raia wake ni vya kushangaza.
Amesema wahusika wote wanapaswa kuwajibishwa.
Awali afisa mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na haki za kibinadam Navi Pillay ameonya kuwa viwango vya ukiukwaji wa haki za kibinadam vinaendelea kuongezeka nchini Syria.
Pillay, amesema ghasia nchini Syria, zinaendelea kuchochewa na kuongezeka kwa idadi ya silaha miongoni mwa wanajeshi wa serikali na upinzani.
Navi Pillay
Navi Pillay
Hatab hivyo Bi. Pillay, hakusema mahala ambako silaha hizo zinatoka lakini waandishi wa habari wanasema serikali ya Syria, inapokea msaada wa silaha kutoka kwa serikali za Iran na urusi.
Upinzani nao ukipewa silaha na serikali za Qatar na Saudi arabia.
Awali Muungano wa nchi za Kiarabu, ulitoa wito kwa upinzani kuungana na kuafikiana kuhusu mpango kwa kipindi cha mpito nchini humo.
Kiongozi wa Muungano huo, Nabil Al Arabi, ameliambia kongamano la wanaharakati wa upinzani mjini Cairo, Misri, kuwa Syria, inahitaji mfumo wa Kidemokrasia ambao hautabagua mtu yeyote.
Wakati huo huo, vyombo vya habari nchini Uturuki, vimesema kuwa wanajeshi 85 wa syria wakiwemo generali mmoja na maafisa wengine 7 waandamizi wamevuka mpaka na kuingia nchini humo.
Mashirika hayo ya habari yametaja kundi hilo kama kubwa zaidi la kijeshi ambalo limeasi na kuingia nchini Uturuki tangu machafuko ya kisiasa kuanza nchini Syria.
Kundi hilo linaripotiwa kutumwa katika kambi moja ya wakimbizi Kusini mwa Uturuki.
Wiki iliyopita, kundi lingine la ziadi ya wanajeshi 30 na familia zao wakiwemo maafisa kadhaa wakuu walivuka mpaka na kuingia Uturuki.

Daktari wa Ikulu akamatwa Venezuela


Rais wa Venezuela
Rais wa Venezuela

Daktari mmoja ambaye anafanya kazi katika ikulu ya rais nchini Venezuela, amekamatwa baada ya kushukiwa kuwa anafichua siri za serikali.
Waendesha mashtaka nchini humo wanasema Daktari Ana Maria Abreu, alifichua siri za kijeshi na kisiasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Hata hivyo taarifa hiyo rasmi haikumtaja rais wa nchi hiyo Hugo Chavez, ambaye anaendelea kupokea matibabu ya ugonjwa wa saratani ambao hautatajwa.
Daktari Abreu, sio daktari wa kibinafsi wa rais Chavez, ambaye mwezi Oktoba mwaka huu anawania muhula mwingine kuwa rais wa nchi hiyo.