NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, May 22, 2012

mahusiano, tamaduni, maumivu, hisia na ashiki

Naam katika mahusiano tamaduni na miiko mbali mbali huingilia kati. Vijana hukutana na vizingiti zaidi katika hili. Dini za kigeni zinamaoni yake katika hili wakati tamaduni na dini za kiasili nazo huwa na mitizamo yake.
Tamaduni nyingi za kiafrika zilipinga sana upatikanaji wa Mimba kwa binti kabla ya kuoelewa. Katika jamii za wahaya kwa mfano, binti aliyepata mimba katika kipindi hicho alikabiliwa na hadhabu kali ya kifo cha kikatili. Mchumba alitafutwa na kukubaliana kati ya wazazi husika na wanandoa kukutanishwa baadae
Dini nyingi za kigeni kama vile ukristo na uisilamu nazo zina tamadmuni zake kwa wachumba na wanandoa. Wale waliobahatika kupata mimba kabla ya kufungishwa ndoa na kiongozi wa dini, hupewa adhabu Fulani Fulani za kiimani kama kutoshiriki kiitwacho chakula cha bwana au hata kutengwa mbali kabisa na nyumba za ibada
Katika mahusiano ya kisasa vijana nao huja na mambo yao. Huu utumika kama wakati wa kujifunza mapenzi yenye ashiki na hisia kali. Hapa wengi hawaambiliki na hujiona wamefika na wanajua kila kitu katika massuala ya mahusiano. Kumbuka tunapokua na kujijua na kutoka nje ya nyumba za wazazi/walezi wetu, jambo kubwa huwa ni mahusiano ya kimapenzi a watu wa jinsia tofauti na za kwetu.
Huwa ni kipindi kigumu cha kujifunza masmuala haya magumu bila kufata utaratibu wowote namwisho huwa ni maumivu ya kuachana na Yule ambaye mtu aliamini ni wa milele. Hata hivyo maumivu haya huwa sio halisi kwani huko mbeleni huja kukutana na wapenzi wengine ambao hupendani sana kuliko wale wa zamani. Kuna wanaozunguka na kurudiana na wale wa zamani
Wazazi wengi hawawasaidii vijana wao katika masuala ya mahusiano isipokuwa wengi huwaingilia na kutaka kuwa tafutia wenza au hata kuwapiga mkwara juu ya mambo haya.
Ndoa hunukia kwa mbali

Tetemeko la ardhi Italia

Maelfu ya watu walioachwa bila makao kufuatia tetemeko kubwa la ardhi Kaskazini mwa Italia watalazimika kulala kwenye mahema kufuatia wasiwasi wa kuzuka tetemeko jingine.
Watu sita walifariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika tetemeko hilo la ardhi lililotokea Jumapili.
Serikali imetoa mahema mengi kwa wananchi hao walioathirika na tetemeko la ardhi ingawa wengine wameamua kulala katika magari yao.
Wataalamu walisema tetemeko hilo lilifikia kipimo ya Richa 6.
Waziri Mkuu wa Italia, Mario Monti, atakatiza mkutano wake na viongozi wenzake wa NATO unaoendelea Marekani kwa ajili ya hali ilivyo nchini mwake.

Sunday, May 20, 2012

Malawi kubatilisha sheria ya mapenzi

Rais Joyce Banda

Rais wa Malawi,Joyce Banda amesema kuwa anataka nchi hiyo ibatilishe sheria inayoharamisha ndoa za jinsia moja na kuifanya nchi ya kwanza ya kiafrika kufanya hivyo tangu mwaka 1994.
Wananume wawili raia wa nchi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani mwaka 2010 baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana.
Baadhi ya viongozi wa nchi za magharibi, hivi karibuni wametishia kusitisha msaada kwa nchi za kiafrika ambazo hazitatambua haki za mashoga.
Rais Banda alichukua hatamu za uongozi mwezi jana kutoka kwa mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, aliyeaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo.
Hadi sasa rais huyo amegeuza baadhi ya sera zake ikiwemo kushusha thamani ya sarafau ya nchi kwa lengo la kuanza kupata msaada .
Wafadhili wengi walisitisha msaada chini ya utawala wa Mutharika, wakimtuhumu kwa uongozi duni pamoja na ukandamizaji.
Katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge la anchi Banda alisema kuwa baadhi ya sheria zilizopitishwa na bunge, zitafutiliwa mbali kama hatua ya dharura ikiwemo sheria zinazopinga vitendo visivyo vya kawaida.
Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani mjini Blantyre, anasema kuwa rais anaungwa mkono na wabunge wengi, na kwa hivyo ataweza kuwashawishi wabunge kubatilisha sheria hiyo.

Friday, May 18, 2012

Baa la njaa la sambaa nchini Niger

Hata baada ya kutahadharishwa kwa miezi kadhaa kwamba baa la njaa linakuja ,sasa Niger inakumbwa na kiwango kikubwa cha utapiamlo.
Akina mama na watoto wao wakisubiri chakula nchini NigeR

Shirika la Save the Children katika taarifa yake limesema hali huko Niger inazidi kuwa mbaya zaidi.
Shirika hilo linasema kuwa watu zaidi ya milioni sita wanakabiliwa na njaa. Na katika eneo zima la Sahel karibu watu milioni 18 wanakabiliwa na tishio la njaa.
Taarifa hiyo inasema kuwa idadi ya watoto wanaohitaji matibabu kutoka na maradhi yanayotokana na ukosefu wa chakula imefikia kiwango cha kutisha.
Onyo hilo la Save the Children linakuja wakati mataifa tajiri zaidi duniani G8 yanakutana kujadili hali ya chakula duniani.
Shirika hilo linasema kuwa kwa wakati huu wanafanya mipango ya dharura kukabiliana na hali hiyo.
Tangu mwaka jana wakati mvua ya masika iliyotarajiwa haikunyesha vizuri jamii ya kimataifa ilianza kutoa ilani kuwa hali huenda ikawa mbaya katika eneo la Sahel na hasa Niger.
Kijumla asilimia 25 ya watoto wote duniani wanakabiliwa na matatizo ya utapiamlo. Wengi ya watoto hao wako bara la Afrika.
Sasa shirika la Save the Children limeomba vingozi wa nchi za G8 wanaokutana Marekani washughulikie hali hiyo.

Kikosi cha Ecowas chawasili Guinea

Mkutano wa viongozi ECOWAS

Kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa usalama kutoka Afrika Magharibi, kimewasili nchini Guinea-Bissau kusaidia kuleta uthabiti nchini humo. Hii ni baada ya tukio la mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi jana.
Takriban wanajeshi 70 wote kutoka Burkina Faso ni sehemu ya vikosi vya usalama vilivyopangiwa kufika nchini humo na jumuiya ya Ecowas.
Takriban wanajeshi 600 wanatarajiwa kufika nchini humo katika siku chache zijazo kulingana na taarifa iliyotolewa na Ecowas.
Guinea-Bissau ilikuwa imesalia na wiki kadhaa kuandaa duru ya pili ya uchaguzi wa urais, wakati jeshi lilipofanya mapinduzi.
Wanajeshi hao waliwasili siku moja na waziri mkuu wa serikali ya mpito, Rui Duarte Barros, aliyetawazwa baada ya mapinduzi.
Viongozi wa mapinduzi hayo, walikubaliana hapo awali kuhusu kipindi cha mwaka mmoja wa ukabidhi wa mamlaka, kama ilivyotakiwa na jumuiya ya Ecowas.
Vikosi hivyo vya usalama, vinapelekwa nchini humo kuweza kusaidiana na wanajeshi kutoka Angola na vile vile kuweza kusaidia harakati za kurejesha utawala wa kikatiba.

Thursday, May 17, 2012

Bosco Ntaganda aingiza watoto jeshini

Jenerali mtoro Bosco Ntaganda, ambae anasakwa na mahakama ya kimatiafa ya jinai -ICC bado anajumuisha watoto katika jeshi lake.
Watoto wapiganaji wa Bosco Ntaganda

Shirika la Human Rights Watch (HRW) linasema kuwa katika mwezi uliopita watoto wapatao 150 wa kike na wakiume wamejumuisha jeshini.
Watoto hao wote wanatoka katika eno la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
wale ambao wamefaulu kutoroka wanaelezea kuwa wengi wao walichukuliwa toka shuleni na vijijini na kuamrishwa kwa bunduki kiunga na wapiganaji wa Bosco Ntaganda.
Mahakama ya ICC mwaka wa 2006 iliamuru Jenerali Bosco Ntaganda akamatwe na kushitakiwa.
Sasa Shirika la Human Rights Watch lenye makao yake New York, Marekani limesema kuwa watoto wanaolazimishwa kuingia jeshini ni wa kati ya umri wa miaka 12 hadi 20.
Uchunguzi wa Human Rights watch unasema kuwa shughuli hiyo ya kuwakamata watoto na kuwaingiza jeshini lilianza kutekelezwa pale wafuasi wa Bosco Ntaganda kuasi jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wafuasi hao walikuwa chini ya kikosi cha Ntaganda cha CNDP ambao walijumuishwa katka jeshi la Congo.
Lakini kufikia sasa Jenerali Ntaganda amekanusha kuchochea maasi katika jeshi la Jamhuri ya Congo.
Inaaminika kuwa Jenerali Bosco Ntaganda anajificha katika mbuga ya Virunga , sehemu iliyo maarufu sana kwa sokwe.
Hata hivyo serikali ya Congo imeahidi kumsalimisha Bosco Ntaganda katika mahakama ya kimatiafa ya jinai -ICC -iwapo itamtia nguvuni.

Wednesday, May 16, 2012

Hoteli yashambuliwa na magaidi Mombasa

Hoteli moja maarufu visiwani Mombasa imeshambuliwa kwa maguruneti na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Magaidi washambulia hoteli kando ya mahali hapa

Hoteli hiyo ,Bella Vista Restaurant,ni maarufu sana kwa watalii na wenyeji na iko kando ya barabara kuu itokayo bandari ya Mombasa.
Mkuu wa kitengo cha polisi wa jinai mjini Mombasa Bwana Ambrose Munyasya aliambia BBC kuwa watu watano walijeruhiwa vibaya katika kisa hicho.
Polisi wanasema kuwa uchunguzi wao wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na milipuko mitatu katika klabu hicho cha Bella Vista Restaurant.
Milipuko hiyo ilisababisha uharibifu wa magari sita yaliokuwa yameegeshwa kando ya hoteli hiyo.
Mkuu huyo wa polisi alisema kufikia sasa wanahofia kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na magaidi.
Inadaiwa kuwa watu wawili walikwenda katika Klabu hicho wakitaka kuruhusiwa kuingia.
Lakini walipotakiwa kupekeliwa na maaskari wa hoteli hiyo walikataa na ndipo wakarusha maguruneti hayo.
Walioshuhudia mkasa huo wanasema kuwa magaidi hao walifyatua risasi ovyo ovyo wakati walipokuwa wakitoroka.
Hata hivyo polisi wanasema hawaja mkamata mtu yeyote kutokana na kisa hicho.

Tuesday, May 15, 2012

Rais mpya wa Ufarnsa Hollande aapishwa


Rais Francois Hollande

Francois Hollande ametawazwa kama rais mpya wa Ufaransa, na kumfanya kuwa rais wa kwanza wa kisosholisti kuapishwa katika miaka kumi na saba.
Bwana Hollande alisema kuwa anafahamu vyema changamoto ambazo Ufaransa inakabiliana nazo ikiwemo, madeni na uchumi unaojikokota.
Baadaye hii leo rais Hollande atamteua waziri mkuu na kisha kwenda nchini Ujerumani kwa mazungumzo na Chansella Angela Merkel.
Bwana Hollande angependa kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mpango wa Ujerumani wa kutafuta suluhu kwa mgogoro wa kiuchumi unaokumba bara la Ulaya.
Hapo jana thamani ya Euro ilishuka masoko ya hisa nayo yakishuka huku hali ya kisiasa nchini Ugiriki ikiendelea kuwa tete.
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa fedha wa ulaya, Jean-Claude Juncker, alisisitiza hapo jana kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Ugiriki inasalia katika muungano wa Ulaya.
Bwana Juncker anasubiri kuundwa haraka kwa serikali mpya ya Ugiriki siku tisa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Lakini pia alionya kuwa Ugiriki haina budi ila kuendelea na juhudi muhimu zilizoanzishwa kuweza kuokoa uchumi wake licha ya sera hizo kupingwa na wapiga kura wengi.
Wengi mjini Berlin wanamshuku bwana Hollande. Hawapendi kuwa wakati wa kampeini zake alionekana kupinga mipango ya kupunguza matumizi ya serikali kwa lengo la kuokoa uchumi pamoja na kuukuza.
Wengi walitafsiri hilo kama juhudi za Ufaransa kutaka kuongoza tena muungano wa Ulaya.

Raia wa Sudan Kusini wafika nyumbani

Raia wa Sudan Kusini

Ndege ya kwanza iliyowabeba wakimbizi waliokwama kwa miezi kadhaa nchini Sudan imewasili mjini Juba Sudan Kusini. Raia hao wapatao 164 wanatarajia kusafirishwa kwa barabara hadi katika kambi mpya wakisubiri kutafutiwa jamaa zao.
Kundi hili ni la raia laki tano ambao walipoteza uraia wao baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake mwaka jana. Nchi hizo nusura kuingia vitani kutokana na mzozo wa raslimali za mafuta na mipaka.
Raia waliofika leo wamekuwa katika jimbo la Nile ambapo walipewa hadi Mei 20 kuamua ikiwa watachukua uraia wa Sudan au kurejea Sudan Kusini.
Maafisa wa Sudan wamepinga hatua ya kuwasafirisha raia hao kwa wingi kwa hofu ya usalama.
Punde baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake maelfu ya raia wake waliofanya kazi katika iliyokuwa serikali ya taifa moja la Sudan waliachishwa kazi na utawala wa Khartoum.
Kuna kambi maalum mjini Juba ya raia hao kabla ya kutafuta maeneo yao ya asilia.
Maelfu ya raia wa Sudan Kusini walihamia Kaskazini wakati wa vita na kutafuta ajira.

Sunday, May 13, 2012

Honi kali zitatumiwa kwenye Olimpiki


Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa chombo kama honi, kitatumiwa kama silaha mjini London wakati wa michezo ya Olimpiki.
Mazoezi ya ulinzi kwenye Mto Thames, London

Kelele za chombo hicho zinaweza kuvuma kwa masafa marefu na kuumiza masikio.
Chombo hicho kimetumiwa sehemu kadha za dunia kutawanya mkusanyiko wa watu; na kinatengenezwa Marekani ambako kimearifiwa kuharibu masikio daima.
Lakini Wizara ya Ulinzi inasema kitatumiwa tu kwenye vipaza sauti kuzuwia misafara kwenye Mto Thames; na ni sehemu ya zana kadha zitazotumiwa kuhakikisha usalama wa Olimpiki.
Chombo hicho kinatumiwa kupambana na maharamia wa Somalia.

Gaidi asakwa Kenya


Maafisa wa polisi nchini Kenya wamesema wanamsaka raia mmoja kutoka Ujerumani anayetuhumiwa kuhusika na mashambulio ya hivi karibuni nchini humo.
Raia wa Uingereza aliyefikishwa mahakamani Mombasa kwa tuhuma za ugaidi
Mtu huyo kwa jina Ahmed Khaled Mueller anadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la al- Shabaab.
Kenya imeshambuliwa mara kadhaa tangu majeshi yake kuingia nchini Somalia kuwasaka wapiganaji wa Al shabaab.
Mmwandishi wa BBC mjini Nairobi anaarifu kuwa maafisa wa polisi nchini Kenya wametoa picha ya raia huyo kwa jina la Ahmed Khaled Mueller na kusema ana uhusiano wa karibu na kundi la al- Shabaab.
Japo maafisa wa polisi hawasemi ni lini aliingia nchini Kenya, wanasema aliingia nchini kinyume cha sheria na kwamba amejihami.
Aidha, polisi imesema mtu huyo anadaiwa kuhusika na mashabulizi ya hivi karibuni nchini.
Hii sio mara ya kwanza kwa polisi kutoa picha ya mtu anayeshukiwa kuhusika na kupanga mashambulizi nchini Kenya.
Mapema mwaka huu, polisi ilitoa picha ya raia mmoja wa Uingereza ambaye anadaiwa kuhusika na kupanga mashambulizi pwani mwa Kenya, na wiki iliyopita maafisa wa polisi walichapisha picha nyengine ya mtu anayedaiwa kuhusika na shambulio la guruneti la mwezi wa Aprili, katika kanisa moja mjini Nairobi, mbapo watu wawili waliuwawa na zaidi ya 15 kujeruhiwa.

Friday, May 11, 2012

Kukosa mwangaza wa jua hatari

Utafiti uliofanywa hivi karibuni juu ya kupungua kwa nuru ya macho kumeonyesha kua hadi asili mia 90 ya wanafunzi wanaohitimu masomo huathiriwa na tatizo la kuona

Jua muhimu kwa macho Macho yahitaji kutunzwa vizuri.

Wataalamu wanasema kua ongezeko hili la kutisha juu ya tatizo la macho limesababishwa na wanafunzi kusoma sana na kukosa mwangaza wa jua.
Wataalamu wameliambia jarida la kiafya la Lancet kua mmoja kati ya wanafunzi watano anaweza kukabiliwa na mapungufu ya macho na hata kupofuka macho.
Kulingana na Professor Ian Morgan wa Chuo Kikuu cha Australian National University, aliyeongoza utafiti huu,asili miaka 20-30% waliwahi kua watu wa kawaida wasiokua na matatizo huko Bara Asia kusini mashariki.
Idadi ya wagonjwa wa maradhi haya ya macho imepanda kutoka asili mia 20 waliopungukiwa na nuru ya kuona na kuzidi asili mia 80 na kuelekea asili mia 90 miongoni mwa vijana na watakapoingia umri wa watu wazima maradhi hayo yataenea zaidi miongoni mwa jamii nzima.Bila shaka hili ni tatizo kubwa la kiafya.
Wataalamu wa masuala ya macho wanasema kua una mapungufu ya macho ikiwa unachotazama hukiona vizuri kutoka umbali wa mita 2 yaani futi sita.
Tatizo hili husababishwa na kurefuka kwa mboni ambako hutokea mtu akiwa na umri mdogo.
Kwa mujibu wa utafiti, tatizo hili husababishwa na masuala kadhaa- kusoma kwa kupindukia na kukosa mwangaza wa jua.
Professor Morgan anasema kua watoto wengi huko Asia ya kusini mashariki hutumia mda mrefu wakisoma shuleni na baadaye kudurusu nyumbani. Hili huwazidishia shinikizo kwenye macho yao, lakini wangeweza kutoka nje kwa mda wa saa mbili hadi tatu ili kurekebisha mapungufu na umuhimu wa mwqangaza inawezekana kulinda afya ya macho yao.
Jicho
Jicho bandia

Wataalamu wana imani kua aina ya kemikali ijulikanayo kama dopamine ambayo huenda ina mchango katika hili. Kukaaa katika mwangaza wa nje huongeza viwango vya kemikali hii ya dopamine ndani ya jicho na hilo huzuia kurefuka kwa mboni.
Nyenzo za kitamaduni nazo zinachangia. Watoto wengi wa Bara Asia kusini mashariki, hupenda sana kupumzika nyakati za adhuhuri. Kulingana na Professor Morgan tabia hii huwakosesha mwangaza wa jua la mchana ambao ni muhimu katika kuzuia maradhi haya ya kupungua kwa nuru ya macho, myopia.
Pamoja na shinikizo za kutaka kufanikiwa katika elimu na kupangiwa siku kwa watoto, mda ambao mtoto hukaa nje kunufaika kwa mwangaza wa jua unapunguwa. Wasiwasi mkubwa ni idadi ya wanafunzi ambao wanazidi kupatwa na maradhi ya myopia.
Kwa miongo kadhaa wataalamu wameamini kua kuna uhusiano mkubwa wa jeni au urithi kutoka kwa wazazi kuhusiana na hali hii ya ugonjwa wa macho.Ikiaminika kua watu kutoka Uchina,Japan,Korea na nchi nyingine wanaweza kukumbwa na myopia.Lakini utafiti huu unaonyesha mtazamo tofauti.
Hili litahitaji utafiti zaidi lakini la muhimu ni kuwatia moyo watoto watumie mda mwingi nje ya nyumba jua linapochomoza. Huenda likapunguza madhara ya macho.

Je Umoja wa Mataifa umeshindwa Syria

Mapigano yanaendelea Syria

Tume ya UN SYRIA
Tume ya UN Syria
Idadi ya watu waliofariki kufuatia mashambulio ya bomu inazidi kuzua masuali juu ya jukumu la waangalizi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo.
Jukumu lao ni kusimamia na kuona kua mapigano yanasimamishwa. Lakini ingawa hilo limetimizwa katika baadhi ya maeneo ukweli ni kwamba mapigano bado hayajamalizika.
Mapigano bado yapo
Mapigano bado yapo
Na hili linazua suali nyeti juu ya umuhimu na uwajibikaji wa tume ya Umoja wa Mataifa.
Imani iliyokuepo ilikua kwamba endapo watatumwa wasimamizi kutoka nje huenda wakasaidia kushawishi wakuu wa serikali kutimiza ahadi zao za kukomesha ghasia.
Lakini tangu mwanzo, kuwepo kwa wasimamizi hawa kulizua suali jipya kuu: Endapo mashambulizi dhidi ya raia yataendelea Je nini kitafuata?
Umoja wa Mataifa utachukua hatua gani zaidi ya hio? Na ni mazingira gani yatafanya Umoja wa Mataifa ukubali kua mpango wake umeshindwa?
Tatizo ni kua hakukuepo mpango mbadala endapo huu utashindwa.
Mpango pekee ambao Jumuia ya kimataifa uliweza kukubaliana kwa sauti moja ni huu wa kutuma wasimamizi. Pamoja na maneno mazuri ya kuvutia ya njia za kupitia kunusuru maisha bila bughdha au njia nyingine za upatanishi, hakuna yeyote aliyetaka kuhusika moja kwa moja na matatzio ya Syria.
Makundi yananufaika kwa ghasia
Makundi yananufaika kwa ghasia
Ingawaje kuhusika kupitia makundi ni njia nyingine. Bila shaka silaha zimekua zikitiririshwa kutoka nje ya nchi. Kukiwa na makundi ndani ya nchi ambayo yanafurahia kuzusha fujo kwa manufaa yao.
Mgogoro wa Syria umeanza kujenga sura ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na Umoja wa Mataifa haujajiweka tayari kutangaza ujumbe wa tume yake umeshindwa kwa sababu hakuna yeyote anayyeweza kujibu suali - Nini kitafanyika sasa.

Waasi washambulia gereza nchini Nigeria

  Watu wenye silaha wamevamia gereza nchini Nigeria, katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno, na kuua walinzi wawili wa gereza hilo na kuwafungulia wafungwa.

Polisi wamesema wapiganaji kutoka kikundi la Kiislam la Boko Haram, kwanza walikishambulia kituo cha polisi katika mji wa Banki, kabla ya kwenda kuvamia gereza karibu na kijiji cha Kunshi.
Msemaji wa polisi amesema wamewakamata watu 23.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo lakini kikundi cha Boko Haram kimelaumiwa kwa kuhusika na matukio ya aina hii kaskazini mwa Nigeria.

Wednesday, May 9, 2012

JAMANI HIVI HATUJUI MAZINGIRA YETU : Ubaya na Uzuri wake…

Jamii zetu zinazoendelea zinahitaji sana Elimu.  Elimu itakayotusaidia kupambana na maadui kama : kutojua kupanga muda (Time Management) tatizo linalotufanya tuchelewe, tusiwe na mpangilio wa maisha ; halafu, kutoyajali mazingira yetu (vyoo vichafu na kutupa taka ovyo).Uchafu wa mazingira DarWataalamu wameshatuonya kuwa makaratasi ya plastiki tunayoyaacha kiholela kila mahali (yenye madawa hatari) yanaharibu rutuba na uhai ; yatakaa ardhini miaka 500 !!!
Bougainvillea -Silversands
Si mbali  na palipotupwa plastiki hizi pana hoteli hii marufu na nzuri ya Silversands ambapo watalii na wenye uwezo wanakaribishwa kwa maua  mazuri yenye asili ya Kimarekani yaitwayo Bougainvillea.  Ikiwa tunaweza kuyapamba mazingira ki-azizi,  hatushindwi kuyaacha safi…
Madafu
Nilishangazwa nilipoelezwa na muuza madafu mmoja Dar kuwa kinywaji (chakula) hicho muhimu siku hizi hakipatikani kirahisi. “Minazi inakatwa ovyo…” akalalama.
Minazi ya Dole
Nilipokuwa kitongoji hiki cha Dole, Unguja, nikawa nawaza lile balaa la minazi kukatwa bandari  ya Dari Salama. Minazi imesimama dede mithili ya twiga au mbuni malishoni.  Je, itadumu?
Matunda ya Afrika  Sehemu nyingi Zanzibar bado vyakula asilia vinathaminiwa. Cheki  matunda, mboga na makulaji : mjini na vijijini. Ama kweli inatia moyo…maana chakula ni utamaduni wa nchi; kama huna au unaiga (huthamini chako) huna jicho…
Chakula cha Zanzibar
Huku unakula huku unafikiria namna ambavyo bado wananchi wengi tunatupa chupa za maji ovyo nje; tunavyofungia bado vyakula vyetu kwa magazeti badala ya mifuko isiyokuwa na sumu na madawa…
Chupa ya maji- uchafu
Kinamasi hiki kimejaza si tu plastiki  na dawa zenye sumu bali pia wadudu kama mbu. Kila anayeweza (kutumia mtandao na kompyuta ni uwezo na nafasi) kuelemisha watu wetu ajitahidi na kujaribu…maana hizi blogu hazisomwi na wengi.
Silversands-2
Hapa natia tizi katika moja ya bichi za Dar…ukweli si rahisi siku hizi kupata ufukwe msafi mjini hapa. Na hata zile safi baada ya kuogelea unahisi macho yakikuwasha washa. Watalaam wameonya kuhusu kutupa taka ovyo baharini, kunya (na kukojoa) ovyo ufukweni, kuchafua michanga kwa vyupa vya vinywaji tunapostarehe kando ya bahari mama ya Hindi.
Jani la Mnazi
Pwani ya Dar