NJOMBE

NJOMBE

Thursday, March 15, 2012

Je wajua faida ya Juice ya komamanga?


Inasemekana; Ukinywa juice ya tunda la komamanga (pomegranate) nusu lita  kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni. 
Pia komamanga inasaidia kuzuia kansa ya matiti isitambae mwilini. 
  Wale wenye vitambi mpooo? na wale kina mama je? Naanzaje kua mteja no.1 wa haya matunda? xoxoxoxooo

Operesheni ya Magufuli Safisha jiji yatikisa Dar


Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli
OPERESHENI  ya kusafisha jiji la Dar es iliyotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli imeshika kasi baada ya tingatinga kubomoa vibanda vya biashara kando ya barabara ya Dar- Morogoro, eneo la Kimara jana.
Tukio hilo lilizua taharuki kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki mabanda hayo, ambao walihaha kuokoa mali zilizokuwa ndani, bila mafanikio.

Msimamizi mwandamizi wa operesheni hiyo, Hamis Abdul alisema kazi hiyo ni endelevu na kwamba baada ya kutoka Kimara, watahamia barabara ya Bagamoyo eneo la Tegeta huku akiwatahadharisha wafanyabiashara waliovamia maeneo hayo, kuhama mara moja.

Abdul aliwataka wafanyabiashara wote wanaofanya shughuli zao katika hifadhi za barabara kuondoka maeneo hayo kwa hiari yao kuepuka hasara ya kubomolewa mabanda yao.

 “Zoezi hili ni endelevu na kwamba baada tu ya kumaliza barabara hii ya Morogoro,  operesheni hii itahamia katika maeneo ya  Tegeta, kwa hiyo ningependa kutumia fursa hii kuwapa tahadhari wafanyabiashara waliovamia  maeneo ya barabara kuondoka kabla hatujafika huko,” alionya.

Wenye vibanda
Baadhi ya waliobomolewa vibanda, walilieleza gazeti hili kuwa pamoja na kufanyika ubomoaji huo, hawako tayari kuondoka.
Walisisitiza kuwa watarudi katika maeneo yao hayo ya awali mara tu baada ya operesheni hiyo kukamilika.
Rwezaura Gerasian mfanyabiashara wa nguo na viatu eneo la Kimara mwisho, alisema Serikali imeshindwa kuwahudumia wananchi na kwamba inakiuka haki za binadamu.

Alisema  kitendo cha Waziri Magufuli kutoa amri ya kuwaondoa katika maeneo hayo si cha  kiungwana, kwani  kinawakandamiza wananchi wa chini na kuendeleza uonevu kwa jamii.

“Sielewi lengo la Serikali yetu, maana inatenda mambo ya ajabu kwa wananchi wake bila hata huruma, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu, tunahaki ya kufanyabishara kwa uhuru katika nchi yetu, kwanini tuishi kama wakimbizi?” Alihoji Gerasian.

Zoezi hilo la bomoabomoa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Magufuli kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania         (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam, kuwaondoa katika  hifadhi za barabara wafanyabiasha wote waliovamia maeneo hayo.
Dk Magufuli alitoa amri hiyo hivi karibuni wakati akizindua  kituo cha daladala cha Mbezi Mwisho.

Agizo la Magufuli na foleni Dar
Machi 4 mwaka huu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa stendi hiyo mpya ya mabasi Mbezi mwisho, Dk Magufuli alisema hakuna sababu ya watu hao kubaki katika hifadhi za barabara wakati sheria zipo na kusisitiza, "Hata kama mkikuta milingoti ya bendera ya CCM vunjeni."

Dk Magufuli alisema, Sheria ya Barabara ya mwaka 1987 inasema wazi kuwa mtu ambaye atakutwa anafanya biashara, kuegesha gari, kumwaga mafuta au uvamizi mwingine wa namna yoyote katika hifadhi ya barabara, adhabu yake ni faini ya Sh1 Milioni.

Alimwagiza meneja huyo kuwa Tanroads haipo kisiasa na wao wapo kusimamia sheria na sio vingine. "Mpo kusimamia sheria, acheni kupiga siasa," alisisitiza.


Dk Magufuli alitoa mfano wa wafanyabiashara wa eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam ambao wamekuwa wakikwaza ujenzi wa barabara ya Bagamoyo kutokana na kupanga bidhaa zao barabarani.

''Ukienda Tegeta watu wamepanga biashara barabarani, Mkuu wa Mkoa upo, Mbunge yupo, Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) yupo, diwani yupo, mkuu wa wilaya naye pia na wote hao wanaangalia tu, ndio Tanzania hiyo?," alihoji na kusisitiza kuwa ifike mahali sheria iachwe ifanye kazi.
Habari na Mwananchi.

Breast firming machine; mtambo wa kuinua matiti

                                                  mambo hayoooo
                 kitu kikitoka hapo kishakua saa 6 chezea
hilo ndo jimashine lol
baada ya zoezi la kuongeza matako nchini tanzania kutawala na kuhusudiwa sana na wadada mbalimbali wa mujini  sasa  kuna mashine mpya zilizoingizwa na wachina za kusimamisha maziwa ya kina dada au kina mama.  zoezi hilo linafanyika katika saloon tofauti tofauti jijini dar-es-salaam na limetokea kupata wateja lukuki na kuonesha kulifurahia.. hahah milki iz standing ndo mpango mzima...kuwa  ndala inahuuuuuu????

Nani mkali: Genevieve v/s Omotola nigerian actress



genevieve

genevieve

omotola

omotola
hawa wote ni waigizaji wa nigeria na hapa tunaongelea full package uzuri,shape na uigizaji nani kamkandamiza mwenzake?

Nafasi ya mwanaume na baba katika maisha ya ndoa na familia

Ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, ninapenda kuchukua fursa hii kukaribisha tena katika makala hii ya ndoa na familia. Juma lililopita tuliangalia kwa pamoja nafasi ya mwanamke na mama katika Familia. Tukahitimisha kwa kukumbusha kwamba, Bikira Maria, Malkia wa Familia ni mfano bora wa kuigwa kwani, kutokana na kuukubali mpango wa Mungu katika maisha yake, amekuwa ni Tabernakulo ya kwanza ya Neno wa Mungu.
Leo tunaendelea kupembua kuhusu hati ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa pili kuhusu wajibu wa familia za kikristo katika ulimwengu mamboleo. Hati hii ya familiaris consortio no. 25 inasema katika muungano wa ndoa mume anaitwa pia kuwa baba katika familia yake.
Upendo wa kweli wa Wanandoa unadai mwanamume atambue kuwa mke wake ni msaidizi ambaye katika sura na mfano wa Mungu wako sawa sio mtumwa wake hivyo ampokee kwa upendo, kama zawadi na awe na shukurani kwa zawadi ya hii. Mfano wa upendo unaodaiwa kati yao ni kama ule wa Kristo kwa kanisa lake (Efeso 5:21-33)
Mwanamume anapaswa kuwa baba wa watoto kibalojia, kisaikolojia, kijamii na kiroho hivyo huyu ni mlezi halisi wa watoto wake katika nafasi yake. Mwana shairi mmoja analinganisha nafasi ya baba katika malezi ya watoto na mwalimu anayemfundisha mwanafunzi wake kuogelea. Anasema endapo mwalimu atamshikilia sana mwanafunzi kwa hofu ya kuzama basi mwanafunzi hatajifunza kuogelea kabisa.Lakini endapo atamwachia sana bila kumpa uangalizi katika maji basi mwanafunzi atazama.
Ndivyo ilivyo kwa baba endapo atakuwa mkali mno mtoto wake hataweza kujifunza kujitegemea kabisa kwani atashindwa kutumia uhuru wake. Lakini akimwachia tu bila kumwelekeza uhuru utazidi na mtoto wake atakuwa mtoto aliyekosa malezi ambayo ni hatari sana kwa makuzi yake.
Tujifunze nini katika hayo yote tuliyosema? Kwanza kila mmoja ajitahidi kuimarisha upendo kwa mwenzake katika nafasi yake.
Pili ni ukweli kwamba katika familia nyingi kuna kilio cha kutoweka kwa akinababa. Wapo akina baba ambao wamebaki baba wa uzazi tu lakini ukiwauliza kuhusu watoto wao watasema mama yao ndiye anajua. Na bahati mbaya zaidi wapo watoto ambao hata hawawafahamu baba zao. Tukumbuke mtoto aliyekosa malezi ya baba hupungukiwa mengi. Ni vizuri akina baba tujitahidi kumwiga Mt. Yosefu ambaye wakati wote alijitahidi kuwa karibu na mama Maria katika makuzi ya mtoto Yesu.
Tumalizie tafakari yetu kwa maneno ya Yoshua bin Sira sura ya 30 anayesema, Mzazi ampendaye mwanawe, atamrudi mara kwa mara ili amwonee fahari jinsi anavyokua...hata kama baba yake akiwa amekufa atakuwa kama hakufa maana ameacha nyuma mtoto anayefanana naye.
Kutoka Studio za Radio Vatican, mimi ni Padre Raphael Mwanga, toka Jimbo Katoliki Same, mwanafunzi wa ndoa na familia, Taasisi ya Ndoa na Familia, Chuo Kikuu cha Kipapa, Laterano, Roma.
Ujumbe kutoka Radio Vatican.

"Tujaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri"

Ujumbe wa Papa Benedikto XVI, kwa ajili ya tafakari za kipindi cha Kwaresima 2012, umewasilishwa rasmi kwa wanahabari Jumanne hii katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.

Akiwasilisha ujumbe huo , Kadinali Robert Sarrah , Rais wa Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki, Cor Unum, ametaja Mada ya ujumbe huo kwamba umevuviwa na aya kutoka Waraka kwa Waeberania 10:24 “Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri".

Ameeleza, Baba Mtakatifu katika mwanga wa mafundisho ya kanisa kwa mwaka huu, anaonyesha mwelekeo wa kina zaidi, katika kazi za Kanisa kama Nabii, katika dunia ya leo, kuutangazia ulimwengu kwa namna ya kipekee, madhara ya utendaji usiomjali Mungu, akitaja hili ni chimbuko halisi la ukosefu wa haki unaoendelea kuitendea dunia

Wednesday, March 14, 2012

Bayern Munich yafanyamauwaji ligi ya Mabingwa

Timu ya Bayern Munich jana iliingia dimbani ikiwa nyuma ya bao moja dhidi ya Fc Basel.Goli hilo Munich alipigwa katika mchezo wa kwanza,Katika mchezo huwo Basel alitoka kifua mbele kwa 1-0.Lakini jana mambo yaligeuka na kuwa magumu upande wa Basel.
Habari zaidi katika michezo.

JAMANI AFRIKA, MATUNDA NA VIUNGO!!NI JAMBO LA KAWAIDA


Nadhani wote mnajua hapa ni mti wa malimao angalia jinsi yalivyo yaani nashindwa hata kuelezea hapa ni mwaka jana  Matema beach mkoani Mbeya Tanzania.

....na hapa bila kiungo hiki kachumbali hainogi ni pilipili kichaa ...swali la kizushi hivi ukila hizi unakuwa kichaa kweli? na kwanini zinaitwa pilipili kicha?..


Bado tupo Matema Beach bonge la mkungu wa ndizi mpaka nikatamani niupate na unajua nini? niliupata:-)
..Hapa ni Mdunduwalo mti wa machungwa ...naipenda Afrika yangu kwa kweli matunda na chakula ni kutoka tu nje na kuchukua.Jamani nimepakumbuka nyumbani

WANAUME BWANA, HIVI MKIONA UCHI WA MWANAMKE MNAPATA NINI?

Wanaume wengine hata wakiona hivi huchanganyikiwa!

Kuna wakati huko Berlin, nchini Ujerumani, kulikuwa na unesho ambapo wanawake walikuwa wakionesha maungo yao kwa malipo. Wanawake hao walikuwa wakionesha maungo hayo kwa wanaume ambao wanaamini kwamba, kuona sehemu uchi wa mwanamke ndicho kilichowaleta hapa duniani.
Hebu sikia ujinga huo zaidi. Waandaaji wa onesho hilo ambalo lilihusisha wanawake wapatao 100 wa umri wa miaka 19 hadi 65 walilazimika kuwaita Polisi ili kudhibiti midume iliyokuwa ikifanya fujo wakati wa kukata tiketi kila mmoja akitaka awe wa kwanza kuingia kwenye onesho hilo.

Kila mmoja alikuwa akitaka awahi yeye kuona sehemu za siri ambazo bila shaka mkewe na watu wengine wa jinsia ya kike wanaomzunguka wanazo!

Mwandaaji wa onesho hilo, Vanessa Beecroft, ambaye ndiye mgunduzi wa njia hii ya kujipatia fedha kirahisi kutoka kwa wanaume hao wasio na haya, hufanya maonesho haya kwa jina la VB55 kwa nyakati na miji tofauti Ulaya.

Msije mkashangaa siku akija na huku Afrika kujichotea mamilioni ya dola, au akajitokeza mjanja mwingine huku Afrika na kuanzisha hayo maonesho, naamini wanaume watauana wallahi.

MWANAMKE ALIYEISHANGAZA AFRIKA, ANATAKA KUOLEWA NA MWANAE WA DAMU!


Mwanamke mmoja wa Zimbabwe Betty Mbereko (40) wa kabila la Masvingo ametangaza kuolewa na mtoto wake wa damu wa kiume mwenye umri wa miaka 23.
Betty amesema sasa hivi anaujauzito wa miezi sita, ujauzito ambao amepewa na huyo mtoto wake aliemzaa mwenyewe, ambapo amekataa kuolewa na wadogo zake marehemu mumewe kama mila inavyosema.
Mama huyu ameishangaza Afrika baada ya kukubali kwamba uhusiano huo wa kimapenzi na mwanae umeanza miaka mitatu iliyopita ambapo amesema ni vizuri aolewe na mwanae ili pia ale matunda ya pesa alizozitumia kumsomesha.
Kwa upande wake mtoto huyo Farai Mbereko (23) ameridhishwa na kuwa kwenye mapenzi na mama yake na kusisitiza kwamba anajipanga kwenda kumalizia mahari ya mama yake kwa babu zake, mahari ambayo baba yake hakuimalizia.
Mwenyekiti wa kijiji wanachoishi wawili hawa, amesema kama sio sheria wangewauwa hawa watu kwa kuwapiga mawe kwa sababu hicho kitendo ni cha laana na kitaleta laana kijijini ambapo hata hivyo wawili hao imebidi wahame kijijini hapo.

Profesa Lipumba: Hatujuti kuwafukuza kina Hamad

MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama hicho hakijutii kumfukuza kwenye chama hicho Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed na washirika wake kwa kuwa ni waasi na uamuzi huo umefanywa kulinda nidhamu ndani ya chama.
Uamuzi wa kuwavua uanachama Hamad Rashid na wajumbe wenzake watatu wa Baraza Kuu la CUF, Doyo Hamis Doyo, Juma Saanani na Shoka Khamis Juma, umekuwa ukitajwa kama sababu ya kuanza kuanguka kwa himaya ya kisiasa ya chama hicho kwa upande wa bara.
Lakini, jana, Profesa Lipumba akizungumzia mwelekeo wa chama hicho alipokutana na waandishi wa habari Dar es Salaam, alisema CUF ni chama imara hivyo lazima kifanye uamuzi kwa kufuata vikao na katiba yake.
“Uamuzi wa kuwafukuza uanachama hatuujutii, ulifanywa kwa umakini kwa kufuata taratibu za kufanya uamuzi kwa njia ya vikao na katiba. Nikiwa Marekani nilikuwa nawasiliana na viongozi wenzangu na uamuzi waliofikia ulikuwa na lengo la kukiimarisha chama,” alisema Profesa Lipumba.
Kuhusu wanachama kukihama chama hicho baada ya kuwafukuza kina Hamad, Profesa Lipumba alisema: “Watu wanaweza kuchapisha kadi nyingi na kusema ni za wanachama waliohama kumbe si kweli. Hatuwezi kuchapisha kadi kama zilivyo noti kwa kuwahofia wahalifu wanaozichapisha, jambo la msingi ni kuwafahamu wanachama wetu.”
“Kuna utata katika takwimu za watu wanaokihama chama, maeneo mengine idadi ya wanachama wanaohama inaelezwa kuwa ni kubwa kuliko idadi wanachama tuliowahi kuwa nao. Hizi ni mbinu zinazotumiwa kuonyesha kwamba chama kinaelekea kufa lakini, ukweli ni kwamba kipo imara na kitaendelea kuwepo.”
Jana Hamad Rashid hakupatikana kutwa nzima kujibu tuhuma hizo. Lakini aliwahi kukaririwa akieleza kuwa uamuzi kumfukuza uanachama ulifanyika kwa mizengwe na chuki.
Alithibitisha madai yake hayo kwa kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo na kuiomba Mahakama imtake Katibu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad na Baraza la Wadhamini la chama hicho kueleza kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kukiuka amri iliyozuia mkutano wa kumfukuza.
Barua pepe
Akijibu tuhuma za Hamad Rashid kwamba aliwahi kunasa waraka wa barua pepe unaoonyesha mawasiliano kati yake na Maalim Seif, Profesa Lipumba alisema kitendo cha kuanika hadharani mawasiliano binafsi ni kosa la jinai... “Hili ni kosa la jinai mtu anatamba hadharani akionyesha mawasiliano ya barua pepe za watu kinyume na taratibu!”
Mwishoni mwa mwaka jana, Hamad Rashid wakati akiwa katika mvutano na uongozi wa juu wa chama chake, alitoa nakala kwa waandishi ukionyesha kile alichodai kuwa ni waraka wa mawasiliano ya barua pepe kati ya Profesa Lipumba na Maalim Seif ukitaja mbinu za kumng’oa katika CUF.
Azungumzia uchumi
Katika mkutano huo, Profesa Lipumba ambaye ni mchumi aliyebobea, pia alizungumzia hali ya uchumi nchini na kusema chama chake kinafanya uchambuzi na hivi karibuni kitakuja na mkakati kuitaka Serikali kuwafungulia akaunti wananchi na kuwaingizia fedha zinazotokana na rasilimali za taifa.
“Tunaamini kwamba wananchi wakiingiziwa mgawo wa fedha kwenye akaunti zao na kukatwa kodi itakuwa rahisi kufuatilia matumizi ya fedha yanayofanywa na Serikali. Watu wakikatwa kodi watakuwa na uchungu na hizo fedha, watafanya kila njia kuhakikisha kwamba zinatumika vizuri kwa ajili ya maendeleo.”
Profesa Lipumba alisema ili hayo yafanyike, ni lazima nchi iwe na utawala bora wenye kusimamia kikamilifu rasilimali za taifa.
Akizungumzia kilimo, alisema asilimia 80 ya watu wanategemea sekta hiyo lakini bado hakijamsaidia Mtanzania... “Tanzania ina ardhi kubwa, lakini wananchi wanategemea chakula cha aina moja hali ambayo inawafanya wengi wao kuugua utapiamlo.”
Profesa Lipumba alisema suala la kuendeleza kilimo lina umuhimu mkubwa kwa sababu ni eneo linaloweza kutoa ajira kwa wananchi hasa vijana.

Monday, March 12, 2012

Mkuu wa Mkoa Arusha akana hajatowa siri Chadema

PINGAMIZI lililowekwa na Chadema kwa mgombea ubunge wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Siyoi Sumari, limezua utata baada ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kudaiwa kuvujisha barua ya siri kwa chama hicho cha upinzani.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vimeeleza kwamba barua hiyo ya siri ilivujishwa na kigogo mmoja wa Serikali mkoani hapa, kwa kile kinachodaiwa, chuki za kisiasa ambapo aliwaagiza makada wa CCM kuifikisha Chadema, ili Siyoi awekewe pingamizi.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alipoulizwa na mwandishi wa gazeti hili kwa njia ya simu jana, alikanusha vikali ofisi yake kuvujisha barua hiyo kwa Chadema, huku akisema kwamba Serikali imeanza uchunguzi wa kina kubaini Chadema walikoipata barua hiyo.

“Mimi kwanza situnzi nyaraka za Serikali na siwezi kutoa nyaraka za Serikali lakini ni lazima tuchunguze Chadema wameipata wapi hiyo document (waraka),”alisema Mulongo.

Chanzo cha mvutano

Juzi wakati Chadema wakitangaza uamuzi wa kumwekea pingamizi mgombea ubunge wa CCM, Sumari, walitumia barua iliyoelezwa kuwa ya siri, ambayo Mulongo aliandikiwa na Idara ya Uhamiaji mkoani hapa kuhusiana na utata wa uraia wa mgombea huyo.

Hata hivyo katika mchakato wa kura za maoni za CCM, Mulongo anadaiwa kuwa katika kundi lililokuwa likimpinga Sumari kupitishwa kugombea na chama hicho tawala.

Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri ya Chadema, John Mrema alisema kwamba barua hiyo yenye kumbukumbu namba AR/32/ VOL.1/85 iliyoandikwa na Mkuu wa Uhamiaji mkoani Arusha, Daniel Namomba kwenda kwa Mkuu huyo wa Mkoa, ilieleza taratibu mbalimbali za kisheria za mtu kuwa raia au la.

Katika barua hiyo iliyoandikwa Febuari 29 mwaka huu, Namomba alitoa ufafanuzi wa sheria hiyo kutokana na maombi ya kufanya hivyo aliyotakiwa na Mulongo kupitia barua yenye kumbukumbu namba CFAl18l114l01l20 .

Katika barua hiyo Mkuu huyo wa Idara ya Uhamiaji alieleza kwamba mgombea huyo alizaliwa eneo la Thika nchini Kenya Mei 11 mwaka 1979 na kwenda mbali zaidi kufafanua kwamba, kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji  namba 7 ya mwaka 1995, kuna uraia wa aina tatu ambao ni wa kuzaliwa, kurithi na kuomba.

Ndani ya barua hiyo, Namomba alifafanua kifungu ambacho mtu anayezaliwa nje ya nchi kama atarithi uraia wa wazazi wake, mmoja au wote, ukomo wake ni miaka 18 na kama atakuwa amezaliwa nje ya nchi, na amefikisha miaka 18 anapaswa kuukana uraia alionao na kuomba uraia wa nchi ambayo anaishi kwa kuapa kiapo cha utii, jambo ambalo Idara hiyo haina kumbukumbu kama Siyoi aliukana uraia wa nchi alikozaliwa.

Kauli ya Mkuu wa Mkoa
Kufuatia utata wa sakata hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alipoulizwa juu ya taarifa hizo, aliendelea kukanusha madai ya ofisi yake kuvujisha barua hiyo huku akisisitiza kwamba ana uhakika barua hiyo haijatokea ofisini kwake naye hahusiki kwa namna yoyote na kuvuja barua hiyo.

“Mimi nakwambia sihusiki kabisa na hilo jambo na nina uhakika kwamba hiyo barua, Chadema hawakuitoa ofisini kwangu, waulizeni Chadema wameitoa wapi ? ”Alihoji na kusisitiza Mulongo

Alikituhumu Chadema kuzua habari hiyo na kudai kwamba wakati fulani, waliwahi kuibuka na nyaraka ambazo wanadai walizitoa Idara ya mambo ya ndani na kumbe si kweli. Alisema ofisi yake itachunguza kwa kina kujua chama hicho kilikopata barua hizo.

Hata hivyo alipotakiwa kujibu madai kwamba ndiye aliyeagiza Idara ya Uhamiaji ichunguze uraia wa Siyoi, Mulongo alisema ni lazima watu wafahamu ya kwamba CCM ilihitaji vielelezo vya mgombea yeyote ambaye alikuwa na mashaka, ili vifikishwe mbele ya chama hicho.
Habari zaidi na Mwananchi

Je ni kweli Urais ni jambo zito namna hii?Kweli Ikulu sio mahali pakukimbilia

 Rais wa kwanza nchini Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
                                RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi.
                              RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini William Mkapa.
Rais wa sasa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete.

Sunday, March 11, 2012

Dk Kawambwa atowa onyo kwa wanafunzi wadanganyifu

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Skukuru Kawambwa, amesema wanafunzi wa Elimu ya Juu watakaobainika kufanya udanganyifu ili wapate mikopo watashtakiwa.

Kitembelea Chuo Kikuu cha Ardhi na kukutana na uongozi wa chuo na Serikali ya wanafunzi jana, Dk Kawambwa alisema pia maofisa wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu watakaobainika kushiriki udanganyifu huo watashtakiwa.
“Wanafunzi watakaodang’anya na kujipatia fedha zaidi za mikopo watashtakiwa, wakiwamo watumishi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu,” alisema.

Pia, Dk Kawambwa aliwataka viongozi wa vyuo vya elimu ya juu kusimamia kwa karibu suala la mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi, ili kupunguza malalamiko yanayojitokeza hasa baada ya utaratibu wa kupitisha fedha za mikopo vyuoni badala ya kuzipeleka moja kwa moja kwenye akaunti za wanafunzi.

“Dawati la mikopo lililoanzishwa kila chuo cha elimu ya juu litumike vizuri ili kuondoa matatizo yanayojitokeza katika kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya wanafunzi, hasa kuwasiliana na bodi ya mikopo badala ya kuwaachia wanafunzi kuwasiliana moja kwa moja,” aliagiza Dk Kawambwa.

Katika hatua nyingine, Dk Kawambwa aliwataka wanafunzi wa elimu ya juu, kujiepusha na migogoro ya aina yoyote wanapokuwa vyuoni.
“Tunataka mkitoka hapa muwe wataalamu wazuri mnaoweza kushindana katika soko la ajira, tusijenge taifa la walalamikaji na wazomeaji. Taifa letu linawategemea ninyi ili kuweza kuliletea maendeleo,” alisema Dk Kawambwa.

Alisema wanafunzi watakaojiingiza katika migogoro hawatasamehewa na badala yake, watachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria za vyuo vyao.

Kauli hiyo ya Waziri Kawambwa kutaka uongozi wa chuo ufuatilie kero za wanafunzi bodi, ilikuja baada ya Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Ismail Mvungi, kumtaka kushughulikia kero ya ucheleweshaji mkopo.

Awali, Mvungi alisema ucheleweshaji wa mikopo ya wanafunzi husababisha usumbufu kwao.Wakati huohuo, Waziri Kawambwa amezindua bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tea), huku akisema bado ina changamoto zinazoikabili.

Mwenyekiti wa bodi hiyo ni Dk Naomi Katunzi, Katibu wake ni Rosemary Lulabuka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Tea, wajumbe ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei, Profesa Siriel Masawe, Profesa Emmanuel Bavu, Vuai Khamis Juma na Muwhela Kalinga.
Habari na Mwananchi

Mgombea ubunge CCM awekewa pingamizi Arumeru

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), jana kilimwekea pingamizi mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Siyoi Sumariki kikitumia barua iliyoelezwa kuwa ya siri ambayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo aliandikiwa na Idara ya Uhamiaji mkoani hapa kuhusiana na utata wa uraia mgombea huyo.

Katika kinyang’anyiro cha kura za maoni, Mkuu huyo wa Mkoa, alidaiwa kuwa katika kundi ambalo lilikuwa linampinga mgombea huyo wa CCM kupitishwa.

Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chadema, John Mrema alisema jana kwamba barua hizo ambazo mwananchi imeziona zinatoa uthibitisho juu ya utata wa uraia wa mgombea huyo wa CCM na hivyo kupoteza sifa.

Katika barua hiyo, yenye kumbukumbu namba AR/C/32/VOL.1/85 iliyoandikwa na Ofisa Uhamiaji mkoa wa Arusha, D. Namomba kwenda kwa Mkuu huyo wa Mkoa, ilieleza kuwa taratibu mbalimbali za kisheria za mtu kuwa raia au la.

Katika barua hiyo iliyoandikwa Februari 29 mwaka huu, Ofisa Uhamiaji huyo, alitoa ufafanuzi wa sheria hiyo kutokana na maombi ya kufanya hivyo, aliyotakiwa na Mkuu huyo wa mkoa, kupitia barua yenye kumbukumbu namba CFA/18/114/01/20.

Kwa mujibu wa barua hiyo, ofisa huyo ameeleza kuwa mgombea huyo alizaliwa Thika, Kenya, Mei 11, 1979.

Hata hivyo, barua hiyo ilieleza kuwa kulingana na Sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995, kuna uraia wa aina tatu, ambao ni wa kuzaliwa, kurithi na kuomba.

Akizungumzia kifungu alisema mtu ambaye anazaliwa nje ya nchi kama atarithi uraia wa wazazi wake mmoja au wote, ukomo wake ni miaka 18.

Alisema kama mtu atakuwa amezaliwa nje ya nchi na amefikisha miaka 18 anapaswa kuukana uraia alionao na kuomba uraia wa nchi ambayo anaishi kwa kuapa kiapo cha utii, jambo ambalo idara hiyo haina kumbukumbu kama Siyoi aliukana uraia wa nchi alikozaliwa au la jambo ambalo hata hivyo, limekuwa halizingatiwi na watu wengi.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Trasias Kagenzi alithibitisha jana kupokea pingamizi hilo na kuomba kupewa muda zaidi wa kuupitia kabla ya kulizungumzia jambo hilo... “Naomba tuwasiliane baadaye kidogo ndiyo nazipitia kumbukumbu hizi, nadhani tutatoa taarifa baadaye.”

Chadema kampeni leo

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, leo anatarajiwa kuzindua rasmi kampeni za chama hicho katika kuwania ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kampeni hizo zitazinduliwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Liganga, Usa River na zitahudhuriwa na wabunge wote wa chama hicho na viongozi wa kitaifa na pia zitarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Star TV kuanzia saa 9:00 alasiri.

Kuhusu uchaguzi huo, Mwigamba alisema: “Huu ni tofauti na chaguzi zote zilizopita. Kwanza tuna mtandao mkubwa wa chama hapa, tuna mgombea anayekubalika zaidi na pia tumejipanga kulinda kura zetu.”

Alisema mgombea wao, Joshua Nasari (26) ambaye pia aligombea katika uchaguzi uliopita, atafanya kampeni katika kata zote 17 za jimbo hilo ili kujihakikishia ushindi.

127,000 kupiga kura

Akizungumzia wapiga kura, Kagenzi alisema watu 127,000 wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo akisema kwamba
hao ni wale waliojiandikisha katika daftari lililotumika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Alisema katika uchaguzi huo pia kutakuwa na vituo 327 na kwamba vyote vimeandaliwa sambamba na waratibu wasaidizi wa uchaguzi.

Vyama vinane vinatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo. Mbali na CCM na Chadema, vingine ni TLP kilichomsimamisha Abraham Chipaka, SAU (Shabani Kirita); UPDP (Charles Msuya); DP, (Mohamed Abdallah) na NRA, (Hamis Kieni).

Ombi

Vyama saba vinavyoshiriki uchaguzi huo vimeliomba Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutenda haki kwa vyama vyote badala ya kukipendelea CCM ili kuepusha vurugu.

Wakizungumza wakati wa kikao cha kuwekana sawa, wawakilishi wa Chadema na UPDP walisema uzoefu unaonyesha kuwa vyombo vya dola na NEC huegemea upande wa CCM kwenye malalamiko mengi yanayowasilishwa na vyama vya upinzani, hali inayowafanya wapinzani kuhisi kupuuzwa na wanye dhamana ya kuwatetea.

“Kila mtu, vyama vya siasa, polisi, Takukuru na NEC watekeleze na kusimamia majukumu yao kwa kufuata na kuzingatia sheria na taratibu za uchaguzi. Uchaguzi ufanyike Meru na kuwaacha wananchi wakiwa na amani, umoja na mshikamano. Tusiwaache wakiwa hawasalimiani. Sote tuna jukumu la kuhakikisha tunafanya kampeni za kistaarabu,” alisema Mwakilishi wa Chadema, Basil Lema.

Lema ambaye ni Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, alisema pamoja na kuahidi siasa na kampeni za kistaarabu, kamwe hawatakubali kuonewa na kuonya kuwa chama chake kimejiandaa kukabiliana na dhuluma au hujuma yoyote.

Mwakilishi wa UPDP, Mussa Ayo aliwataka polisi kusimamia utekelezaji wa muda wa kuanza na kumaliza kampeni hasa kwa upande wa CCM ambao alidai kuwa wamekuwa wakiendelea na mikutano yao hata baada ya Saa 12:00.

“Kampeni isihusishe kashfa wala kuponda vyama vingine. Kila chama kitangaze sera zake na kuomba kura, Arumeru isiwe kama Igunga ambako watu walipambana kwa matusi, mapigano na hata kumwagiana tindikali,” alisema Ayo.
Kwa upande wake, Msimamizi wa uchaguzi huo aliwataka wadau wote kuzingatia sheria katika kila jambo wanalofanya na kuahidi kutenda haki kwa vyama vyote ili kuhakikisha unakuwa huru na haki.

Alimwomba kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru kuwarejeshea shahada zao za kupigia kura wananchi waliozitumia kuwawekea dhamana ndugu zao wenye kesi katika vituo mbalimbali vya polisi wilayani humo ili kuwawezesha kushiriki kupiga kura Aprili Mosi, mwaka huu.

Kikao hicho kiliwashirikisha, Kagenzi pamoja na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arumeru, Benedict Mapujila.

Habari hii imeandaliwa na Mussa Juma, Arumeru na
Peter Saramba, Arusha

Habari na Mwananchi